Boran Jakutay
Senior Member
- Apr 8, 2023
- 110
- 255
Usafiri wa bodaboda ni rahisi na nafuu hasa kwa sisi wakazi wa Dar es Salaam kutokana na foleni zilizopo.
Lakini bodaboda hizo sio salama zaidi kwa maisha yetu na tusipokuwa makini, zitamaliza kizazi chetu.
Kila kukicha, ajali za bodaboda zinaongezeka, hiyo inatokana na madereva kutokuwa makini, huku wengine wakikosa uzoefu.
Nimeshuhudia kwa macho yangu, kijana amefika mtaani, kwa kuwa hana mishe ya kufanya, akaomba afundishe kuendesha pikipiki, akafundisha kienyeji na wenzake.
Baada ya wiki moja, kaingia barabarani na chombo eti na yeye anabeba abiria.
Tazama mtu kama huyu, hana elimu yoyote ya usalama barabarani, achilia mbali cheti cha mfunzo na leseni.
Abiria akitokea kwa kuwa hamfahamu huyo kijana na amemuona tu amepaki kijiweni na pikipiki, anapanda ili afikishwe safari yake.
Bahati mbaya wanapata ajali kwa uzembe wa dereva, vifo vinatokea au ulemavu wa kudumu.
Sisemi kwamba mtu mzoefu na mwenye elimu ya udereva hawezi kupata ajali, lakini huyu anakuwa na tahadhari kubwa kumshinda asiye na elimu.
Ndugu zangu tuwe makini na hivi vyombo, tusipojilinda wenyewe, hakuna miujiza itakayoshuka kuja kutuokoa.