Fainali Uzeeni!....

vijana wapungeze Muda/feza za kuendekeza heshima bar ...... sio unapofika kustaafu unakuwa ombaomba wakati ulikuwa na nafasi nzuri ya kujihakikishia maisha mazuri ya baadae.... hakuna ajuaye atafikisha umri gani isipokuwa aliye juu...... ni bora kujiandaa kuliko kuona hautafika umri fulani je ukifika na ulichemsha itakuwaje? ndio mwanzo wa kusumbua wale waliojiwekea mafao ya uzeeni
The following user The Finest says thank you to Blaki Womani for this useful post
 
Asante sana mbu kwa kutukumbusha hilo............ukiwa hujajianda unaona maisha si kitu tena....vijana tusijisahau tukabaki kujirusha na kuponda raha fainali uzeeni

cku hizi ni wachache sana wanazeeka, cjui kama hata nitafikia huo uzee, cku hizi tunaondoka mapema kweli kweli wachahce ndio wanabahatika kuona mpka wajukuu.
 
Mkuu..Thanks for the post na pia umetumbusha tena wajibu wetu…uzee!

Binadamu wote tumeumbwa na chembe chembe za uoga..yaani tunaogopa mabadiliko..ya aina yeyote. ..lakini hapa ni break! Sisi wote ni wazee watarajiwa!

Uzee unaweza kuwa asali au shubiri..Ukiangalia jinsi tunavyowadharau wazee wetu yaani tunasahau kuwa sisi ni wazee watarajiwa..Hii ndiyo maana utaona baadhi yao wanaona ni afadhali kufa kwani wanadhani hiyo ndio njia sahihi ya kupoza maumivu ya roho.

Wazee wetu wanajiona kama wao ni bure na mizigo kwa jamii ambayo waliipenda wakiwa vijana. Jamii inasahau jinsi gani wazee walivyochangia maendeleo wakati walivyokuwa vijana kama sisi. Tunasahau jinsi walivyojinyima ka akiba kao kidogo ili sisi wengine tuende shule na kukimbia umande..tunasahau hayo….

Sasa ni zamu yetu kupata kibano.. Je tunajiandaaje? Kutokana na ugumu wa maisha na umasikini wetu huku uswazi Bongo ..Kukosekana kwa Huduma za bure za umma sisi walalahoi kutumia ka akiba ketu chote kwenye mahitaji ya kupata huduma hizo na kupata mkate wa kila siku..mwishoni… Kitu utachokuwa unategemea ni ile michango ya lazima ya NSSF, PPF etc.. lakini hata hivyo mbona tuko usingizini? Nani kati yetu anafuatilia maendeleo ya mifuko hii..nani ana-debate na wadau future za investment hizi (NSSF, PPF etc) wote tunaona kufuatilia maendeleo ya mifuko hii ni suala la kisiasa.. tunajisahau sisi ni wazee watarajiwa na hapo baadaye hii mifuko itakuwa ndio kimbilio letu wakati jamii inatufukuza kwenda jalalani na kusahau machache mazuri tunayofanya sasa..
 
I adore your THINKING! Kuna maisha mengi sana yanayopotea siku hizi :: Makaburi mengi pale Kinondoni utakuta mapy mapya kabisa yameandikwa

Kuzaliwa : 1970/1980
Kufa : 2010/11

hahahah umeona eehhh, Baba E hujatulia, mie ninachokifanya sasa hivi kweli nafanya kwa ajili ya watoto wangu wacha tu niwawekezee hao coz cna uhakika wa kuzeeka kwa kweli, ikitokea nikazeeka bac nina kakibanda ntajishikiza hapo nikisubiria kutwaliwa, kuzeeka cku hizi kumekuwa kugumu sana.
 
cku hizi ni wachache sana wanazeeka, cjui kama hata nitafikia huo uzee, cku hizi tunaondoka mapema kweli kweli wachahce ndio wanabahatika kuona mpka wajukuu.
Nyamayao kwa umri ulionao sasa hivi sijui kwangu mimi nitasemaje kuoa bado watoto bado.
 
Inside Every Old Man there is a Young Man Wondering, What the Hell Happened....

Saying that inabidi as a community tusiige culture ya western people inabidi tuwajali wazee wetu.., at least wenzetu wana care homes.... Sababu uzee ukiingia its not only material things that matter hata ile thought ya kwamba people care na wewe sio mzigo...

Therefore kwa vijana hata kama story za wazee zinaboa please, pretend that you care..., and there is no substitute for experience... ambazo wazee wanazo in abundance (tusibadilike wema wetu wakuwasaidia wazee wetu hata wale ambao sio wazee wetu) because that is the only thing which we africans are better at than our western counterparts
 
vijana wapungeze Muda/feza za kuendekeza heshima bar ...... sio unapofika kustaafu unakuwa ombaomba wakati ulikuwa na nafasi nzuri ya kujihakikishia maisha mazuri ya baadae.... hakuna ajuaye atafikisha umri gani isipokuwa aliye juu...... ni bora kujiandaa kuliko kuona hautafika umri fulani je ukifika na ulichemsha itakuwaje? ndio mwanzo wa kusumbua wale waliojiwekea mafao ya uzeeni

tufanye mambo 50-50, 2wekeze na 2ufurahie ujana jamani lyfe la cku hizi la kupimia sana tofauti na zamani wazee wengi ndo walikuwa wanatwaliwa, ukickia mtoto katwaliwa ni mcba mzito kjjn, cku hizi mambo ya kawaida kabisa hayo, lyfe limebadilika sana, 2wekezw/2furahie ujana vyote pa1......
 
cku hizi ni wachache sana wanazeeka, cjui kama hata nitafikia huo uzee, cku hizi tunaondoka mapema kweli kweli wachahce ndio wanabahatika kuona mpka wajukuu.

Nyamayao huwezi jua katika hao unaosema wachache wewe ukawa mmojawao...........nii thread ya mbu imenikumbusha machungu sana .............nina ndugu yangu alikuwa ameajiriwa na mshahara na marupuru kibao lakini hakujua ipo siku atageuka ombaomba.....hakupeleka watoto shule kama inavyotakiwa alikuwa starehe na yeye.... amestaafu hakuna alichokifanya hana nyumba wala chumba anapita kila mahali kuomba msaada ukimwona unatamani kumtwanga kibao badala ya kumsaidia anatia huruma watoto nao ndivyo sivyo.....usiombe kukutana na mtu anayekumbana na hili neno FAINALI UZEENI
 
Mbu,

Umeniharibia Ijumaa yangu bana! Nahisi leo Serengeti Bia haitashuka sawa sawa!

Umenikumbusha kitabu kinachoitwa : 101 Really Important Things You Already Know, But Keeps Forgetting (By Ernie J. Zelinski)
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
tufanye mambo 50-50, 2wekeze na 2ufurahie ujana jamani lyfe la cku hizi la kupimia sana tofauti na zamani wazee wengi ndo walikuwa wanatwaliwa, ukickia mtoto katwaliwa ni mcba mzito kjjn, cku hizi mambo ya kawaida kabisa hayo, lyfe limebadilika sana, 2wekezw/2furahie ujana vyote pia....

Nakubaliana na wewe lakini wengine wanapitiliza.....wanajisahau wanaona hapo ndio mwisho
 
Halafu mambo ya kujifanya Invisible hautaki kuonekana ngoja nianze kufanya TRACE ROUTE hapa mujini nione nitaishia kukupata kwenye destination ipi i hope hawataniambia "Destination Host Unreachable"

Hahahahah
Kwanza nam-miss hapa JF na dada LD maana bila yeye mambo maisha yangu hapa JF yangekuwa magumu.
Mimi niko available sana mkuu wangu, hata Maty ananipata kisawasawa ila ratiba za Asprin na Teamo ni kali mno, zinanishinda. Isitoshe mkuu ngoja nilambe likizo utaona fujo zangu, mpaka mtasema basi wenyewe.
Wewe si unapendaga kupanda Toyo . . . hahahah
 
Nyamayao huwezi jua katika hao unaosema wachache wewe ukawa mmojawao...........nii thread ya mbu imenikumbusha machungu sana .............nina ndugu yangu alikuwa ameajiriwa na mshahara na marupuru kibao lakini hakujua ipo siku atageuka ombaomba.....hakupeleka watoto shule kama inavyotakiwa alikuwa starehe na yeye.... amestaafu hakuna alichokifanya hana nyumba wala chumba anapita kila mahali kuomba msaada ukimwona unatamani kumtwanga kibao badala ya kumsaidia anatia huruma watoto nao ndivyo sivyo.....usiombe kukutana na mtu anayekumbana na hili neno FAINALI UZEENI

nakubaliana kabisa na hiyo, cjajisahau BW, najitahidi kuwekeza yacnitokee hayo coz ki ukweli inaogopesha huo msoto wa baadae, nipo 50/50..nawekeza na nafurahia ujana pia, najitambua kuwa natakiwa niwekeze but sio kimsoto ile nina elfu 10 nina kiu ya ballantin nishindwe kunywa nikiifikiria niikusanye niongezee kwenye tofali, huo msoto siutaki na naufanyia kazi ndugu yangu.
 
Mheshimiwa mbu, salaam.

Naona umeamua kutusemea sie ambao tushazeeka.....ngoja nikapige vibati kwenye lile banda langu. Kuadhrika mjini si mchezo

Stop biting these young guys, coz malaria haikubaliki! Hawatayafurahia maisha haya matamu tunayoyaishi ya uzee. BTW ulikuwa wapi siku zote ndo uje utukumbushe leo baada ya kumeza chumvi ya kutosha?
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Hahahahah
Kwanza nam-miss hapa JF na dada LD maana bila yeye mambo maisha yangu hapa JF yangekuwa magumu.
Mimi niko available sana mkuu wangu, hata Maty ananipata kisawasawa ila ratiba za Asprin na Teamo ni kali mno, zinanishinda. Isitoshe mkuu ngoja nilambe likizo utaona fujo zangu, mpaka mtasema basi wenyewe.
Wewe si unapendaga kupanda Toyo . . . hahahah
Vijana huwa mnanipa raha sana mnaponikumbukaga hivi...... Fainali uzeeni
 
Back
Top Bottom