Faida za upimaji na usajiri wa ardhi/viwanja

YES!
Najua kupima mwenyewe na nina ramani zangu na coordinates zake na ku-verify google earth .... je wewe kama mtu uliyesajiliwa, unafanya verification na kuondoa gharama nyingine? ... ninayo hadi topographic map ya mashamba kwa sababu tu niliwahi kuchukua GIS kidogo. Ila hazijahakikiwa, unaweza fanya uhakiki? ... for a cheaper price since I did most of the $hit by myself?

JF si pa blabla, inatakiwa mtu jipange kiuhakika, unakutana na chanamoto nyingi. Kobelo umenifurahisha sana kwa hilo pengine linaweza saidia kupunguza gharama kubwa za survey.
 
Hyo bei ni pamoja na Hati? Kama Beacon tu kwa 1.8m basi gharama zipo juu,maana navyojua mie kuweka beacon gharama haizidi 600k,Visiting site na kuchukua GPS ni elfu 60 tu,gharama za usafiri what if nina kavitz kangu? Je Town Plan mnatoa ninyi?

Tunahitaji ushindani wa wajuzi wengi, tukiwa na wachache ndio hii, gharama kubwa ukijulisha na ile ya kunua ardhi wachache tu watamudu.
 
Kiwanja changu kiko Mbezi nyia ya kwenda goba ,kina upana wa mita 45,urefu mita 100. Nina hati zote za awali,namaanisha uthibitisho wa mjumbe,na serikari ya mtaa. Nimshaweka kajibanda ka kuishi kwa muda. Je unaweza kunipa tathmini ya gharama hadi kupata hati ili nipate kujiandaa kabla ya kukuita. Nijibu ninahitaji kupimiwa
 
Mkuu just nipe makadilio tu,nikihitaji kitu Mimi nalipa sina longolongo.Sidhani kama kuna haja ya kukutana ,nipe price nitamtuma kijana utaenda naye ,nitakapohitajika, yes nitakuja,hii Ndio maana ikaitwa biashara ndani ya mtandao tunamalizana humuhumu. Nakupa my personal email,pls hit to tha target, give me tha cost . ambal_zuberi2000@yahoo.com
 
Ekari moja inaweza kutoa viwanja vingapi vya Sqrm 1000? Na gharama inatozwa kulingana na idadi ya viwanja vitakavyotoka?
kwa wastani wa kawaida ni viwanja vinne vyenye upana na urefu wa 31.62 kwa 31.62, gharama lazima ibadilike kutegemeana na resources zitakazotumika.
 
kwa wastani wa kawaida ni viwanja vinne vyenye upana na urefu wa 31.62 kwa 31.62, gharama lazima ibadilike kutegemeana na resources zitakazotumika.

Nashukuru,na hili swala la sehemu ambazo hazina town plan huwa mnalimaliza vipi? Au ndio mpaka mteja asubiri hiyo town plan itoke?
 
Nashukuru,na hili swala la sehemu ambazo hazina town plan huwa mnalimaliza vipi? Au ndio mpaka mteja asubiri hiyo town plan itoke?
hakuna upimaji unaofanyika bila town plan kwasababu TP ndo muongozo ambao unampatia surveyor njia za kupita wakati wa upimaji, sasa kama TP hamna katika eneo husika basi inabidi wataalamu wa mipango miji waandae mchoro kisha upata approval kutoka wizarani kisha kazi ya kupima ndo ianze.
 
Heshima yako mkuu,nina eneo langu halijapimwa,ila nimesha chukua coordinates za kuzipeleka wizarani kucheki kama lipo ndani ya master plan.Inaonekana eneo lipo nje kidogo ya master plan,swali langu ni kwamba kiutaratibu nani anaweza kufanya kazi ya kunitengenezea plan? Je ni ardhi au town planner yoyote tu anayesajiliwa?
 
Samahani,
Nina kiwanja changu na nimeanza ujenzi je naweza kupima baada ya kumaliza kujenga?
 
hakuna upimaji unaofanyika bila town plan kwasababu TP ndo muongozo ambao unampatia surveyor njia za kupita wakati wa upimaji, sasa kama TP hamna katika eneo husika basi inabidi wataalamu wa mipango miji waandae mchoro kisha upata approval kutoka wizarani kisha kazi ya kupima ndo ianze.

Bwana GIS expert, Naomba ushauri wako na kuelimishwa. Hivi inawezekanaje TP ifanyike kwenye eno langu ambalo nalimiliki kimila na halijapimwa. Kama sikosei, TP ni kuonyesha matumizi ya ardhi kama vile makazi, viwanda, barabara etc. Sasa utawekaje mambo hayo katika eneo langu? Naomba kuelimishwa.
 
GHARAMA ZA KUPIMAADRHI KWA PLOT MOJA
INFORMATION FORSURVEY WORK:
Visiting site: Tsh.150, 000/=
Hiring tools: Tsh.300, 000/= per day
Surveyor charge: Tsh. 500, 000/=
Labor charge: Tsh.100, 000/=
Beacon Tsh.10, 000/= @1
Data + cartographic materials: Tsh.100, 000/=
Transport: Tsh.100, 000/= but it depend on the distance tobe travelled to sites
SUB TOTAL: Tsh.1, 300,000/=. Total hii imepigwa Kwa beacons tano lakini minimum beacons ni nne.
OFFICE WORK:
Licensed surveyor fee: Tsh.100, 000/=
Survey instruction: Tsh.100, 000/=
File compilation: Tsh.100, 000/=
Land officer: 50,000/=
Survey check two: Tsh.50, 000/=
Submission fee: Tsh.20, 000/=
Survey approval: Tsh.100, 000/=
GRAND TOTAL: Tsh.1, 820,000/=
Hivyo basi kwa tathimini hiyo gharama halisi inaweza rangekuanzia Tsh.1, 000,000- Tsh.2, 000, 000 kutegemeana na ugumu wa kazi na mahali site ilipo,kuhusugharama za kupima mashamba mara nyingi huwa tathimini yake inafanyika baada yamtaalamu kuangalia site ilivyo lakini kwa kawaida kwa ekari moja huwainagharimu kiasi kinachoanzia laki 700, 000 mpaka 1,000,000 kutegemeana namakubaliano ya mteja na mtaalamu baada ya utasmini wa gharama husika kufanyika.
Hiyo nimetoa kama roughly coast wana jf,kwamaelezo Zaidi napatikana kwa namba 0714238436

Du gharama zinajirudia rudia vipi
 
Back
Top Bottom