Faida za upimaji na usajiri wa ardhi/viwanja

hapo nimeanisha gharama za kupima plot moja tu ambayo ipo katika standard za mgawanyiko wa aina ya viwanja lakini kwa ukubwa za hapo basi pia huwa kuna gharama zake tofauti na hizo kutegemeana utasmini wa gharama. kuhusu kupima mashamba ni lazima uhakikishe unapata kibali au uthibitisho kutoka kwenye serikali ya kijiji husika na kuhusu upatikanaji wa hati huwa hakuna muda maalumu uliowekwa isipokuwa inategemeana na ukubwa wa kazi na foleni za watu wanaofuatilia hati wizarani. nafikri nimekujibu maswali yako?

Awali ya yote naomba nifute kauli yangu ya hapo juu japo wewe ndio uliye sababisha.Tuyaache hayo,Nafikiri nitakuwa mteja wako hivi karibuni maana nimekuwa nazitafuta hizi details muda mrefu

Awali ya yote naomba kujua hili,Kwa wastani ekari moja inaweza kutoa viwanja vingapi vya Sqrm 1000?
 
kwa wastani wa ekari moja unaweza pata wiwanja vine vyenye wastani wa upana na urefu wa 31.62*31.62 ambavyo ni low density plots.
 
YES!
Najua kupima mwenyewe na nina ramani zangu na coordinates zake na ku-verify google earth .... je wewe kama mtu uliyesajiliwa, unafanya verification na kuondoa gharama nyingine? ... ninayo hadi topographic map ya mashamba kwa sababu tu niliwahi kuchukua GIS kidogo. Ila hazijahakikiwa, unaweza fanya uhakiki? ... for a cheaper price since I did most of the $hit by myself?
kwa biashara naomba uniPM kiongozi.
 
Hyo bei ni pamoja na Hati? Kama Beacon tu kwa 1.8m basi gharama zipo juu,maana navyojua mie kuweka beacon gharama haizidi 600k,Visiting site na kuchukua GPS ni elfu 60 tu,gharama za usafiri what if nina kavitz kangu? Je Town Plan mnatoa ninyi?
 
hizo ni gharama za upimaji tu kama jinsi nilivyoziainisha hapa juu, hapo hakuna ujanja ujanja hzo ni gharama ambazo nimezifanya kwa kuzingatia vigezo muhimu pamoja na muongozo wa wizara lakini pia kuhusu usafiri kama unao itakuwa bora kwako kwasabababu gharama zinapungua.na kuhusu town plan huwa wizara ndo inatoa hzi TP ingawa pia kuna makampuni binafsi huwa wanaandaa TP kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na wizara.
 
habarini wana jf, napenda kumshukuru mungu kwa kunipatia uzima mpaka wakati huu ambao nimeamua kukaa na kuandika machache yanayohusu suala la faida za upimaji na usajiri wa ardhi au viwanja kwa ajili ya matumizi mbalimbali yakiwemo kama yale ya ufugaji, kilimo, makazi na biashara. kwa ujumla upimaji huu unafanyika kwa ajili ya kuhakikisha haki ya mmiliki wa ardhi husika inatambulika kisheria kwa kuangalia mipaka inayozunguka ardhi hiyo au kiwanja chake. leo nitasema machache juu ya faida za upimaji na usajiri wa ardhi. upimaji wa ardhi huwa unalenga mambo haya muhimu kwanza ni utambuzi kisheria kwa mmiliki husika wa ardhi hiyo, kuongeza thamani ya ardhi, kuongeza usalama katika kumiliki ardhi hiyo, pia kwa kiwanja ambacho kimepimwa mmiliki wake anaweza kutumia hatimiliki ya kiwanja katika uombaji wa mkopo benki au katika taasisi yeyote ya fedha hapa nchini. hivyo napenda kusema kwamba tupime ardhi tulizonazo kwa usalama na maendeleo yetu. kwa atakaye hitaji huduma hii ya upimaji basi naomba afanye consultation kwa kuniPM.

kutmia hati kuomba mkopo ngumu aisee
 
Gis expert asante mwa mchanganuo. Kwa mfano mimi nina Gps yangu na naweza leta data ofisin kwa co-ordinates in X n Y .csv(file) bado chaji yenu inabaki hapo hapo? Na kama hakuna ulazima nikiwa mtaalamu wa hizo maneno si unaweza niambia tu whats needed ili kupunguza mda na gharama za kufika site (I mean kumleta mtu wkt vipimo vyote naeza leta ofisini).
 
Last edited by a moderator:
hizo ni gharama za upimaji tu kama jinsi nilivyoziainisha hapa juu, hapo hakuna ujanja ujanja hzo ni gharama ambazo nimezifanya kwa kuzingatia vigezo muhimu pamoja na muongozo wa wizara lakini pia kuhusu usafiri kama unao itakuwa bora kwako kwasabababu gharama zinapungua.na kuhusu town plan huwa wizara ndo inatoa hzi TP ingawa pia kuna makampuni binafsi huwa wanaandaa TP kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na wizara.

Ok mkuu ntakutafuta kwa hyo kazi maana nina kapori kangu jirani yangu kaweka jiwe that means cost ya kulitafuta jiwe haitakuwa kubwa sana maana jiwe lipo hatua moja tu.
 
Gis expert asante mwa mchanganuo. Kwa mfano mimi nina Gps yangu na naweza leta data ofisin kwa co-ordinates in X n Y .csv(file) bado chaji yenu inabaki hapo hapo? Na kama hakuna ulazima nikiwa mtaalamu wa hizo maneno si unaweza niambia tu whats needed ili kupunguza mda na gharama za kufika site (I mean kumleta mtu wkt vipimo vyote naeza leta ofisini).

Hiyo kitu haipo ndugu. Lazima Surveyor aende site ili awe na uhakika wa vipimo. Mimi mwenyewe ni Surveyor! Surveyor lazima afuate taratibu zote including site visit unless kama ni Surveyor njaa.
 
Last edited by a moderator:
Hiyo kitu haipo ndugu. Lazima Surveyor aende site ili awe na uhakika wa vipimo.

Hahaaaha haya mkuu, lakini ukiwa Gis expert mix na Raster data wala huhitaji kufika site, ila powa kibongo bongo tu itabidi tufanye red tape tu iwepo. But surely developed countries wamesharahisisha baadhi ya basic data kama hizo kuwa precise sio mpk ufike site kwa sababu hata latest GPS ina makosa ya 6m plus or minus

Na wala sio vigumu hata kidogo, I can assure you bwana Gis expert
 
Last edited by a moderator:
Gis expert asante mwa mchanganuo. Kwa mfano mimi nina Gps yangu na naweza leta data ofisin kwa co-ordinates in X n Y .csv(file) bado chaji yenu inabaki hapo hapo? Na kama hakuna ulazima nikiwa mtaalamu wa hizo maneno si unaweza niambia tu whats needed ili kupunguza mda na gharama za kufika site (I mean kumleta mtu wkt vipimo vyote naeza leta ofisini).
kamandakazi amekupatia majibu mazuri sana, ni kweli ni lazima survor aende site ingekuwa hivyo usemavyo basi kulikuwa hakuna haja ya wataalamu kukaa kusoma miaka mine chuo. lakini pia hizi kazi ieleweke kuwa ni kazi za kitaalama sio ujanja ujanja tu.
 
GHARAMA ZA KUPIMAADRHI KWA PLOT MOJA
INFORMATION FORSURVEY WORK:
Visiting site: Tsh.150, 000/=
Hiring tools: Tsh.300, 000/= per day
Surveyor charge: Tsh. 500, 000/=
Labor charge: Tsh.100, 000/=
Beacon Tsh.10, 000/= @1
Data + cartographic materials: Tsh.100, 000/=
Transport: Tsh.100, 000/= but it depend on the distance tobe travelled to sites
SUB TOTAL: Tsh.1, 300,000/=. Total hii imepigwa Kwa beacons tano lakini minimum beacons ni nne.
OFFICE WORK:
Licensed surveyor fee: Tsh.100, 000/=
Survey instruction: Tsh.100, 000/=
File compilation: Tsh.100, 000/=
Land officer: 50,000/=
Survey check two: Tsh.50, 000/=
Submission fee: Tsh.20, 000/=
Survey approval: Tsh.100, 000/=
GRAND TOTAL: Tsh.1, 820,000/=
Hivyo basi kwa tathimini hiyo gharama halisi inaweza rangekuanzia Tsh.1, 000,000- Tsh.2, 000, 000 kutegemeana na ugumu wa kazi na mahali site ilipo,kuhusugharama za kupima mashamba mara nyingi huwa tathimini yake inafanyika baada yamtaalamu kuangalia site ilivyo lakini kwa kawaida kwa ekari moja huwainagharimu kiasi kinachoanzia laki 700, 000 mpaka 1,000,000 kutegemeana namakubaliano ya mteja na mtaalamu baada ya utasmini wa gharama husika kufanyika.
Hiyo nimetoa kama roughly coast wana jf,kwamaelezo Zaidi napatikana kwa namba 0714238436

Sijaelewa hapo red bold mkuu, ina maana kama mtu anataka hati ya shamba lake la ekari 10 itabidi azidishe hiyo 1,000,000 mara Kumi? Mbona ni ghali hivo au inakuwaje?
 
Sijaelewa hapo red bold mkuu, ina maana kama mtu anataka hati ya shamba lake la ekari 10 itabidi azidishe hiyo 1,000,000 mara Kumi? Mbona ni ghali hivo au inakuwaje?
hapana, nimesema kwa ekari moja tu lakini kama una ekari kumi basi inategemea na idadi ya beacons, umbali, ugumu wa kazi yaani namaanisha kwamba kama shamba lina vichaka na misitu mingi upimaji wake unakuwa mgumu sana na wataratibu mno hivyo haya ni baadhi ya mambo ambayo yanapelekea gharama kutambulika.
 
Thanx mkuu nimekupata, one day nitakutafuta. Unafanyia kampuni gani ili iwe rahisi zaidi kukupata
 
Back
Top Bottom