Faida na Tahadhari za Chuchu Bandia (Pacifiers)

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,553
Chuchu bandia zimekuwa zinatumika sana katika kurahisisha uleaji wa watoto, hasa wale wakorofi.

1173E04B-82C6-4618-93E0-12A3BCA384BB.jpeg


Huwasaidia wazazi kupata uhuru kidogo wa kufanya kazi zingine kama kupika, usafi wa nyumba au hata kukamilisha biashara na kazi zao zingine.

Faida
Chuchu bandia huwa na faida nyingi. Miongoni mwa faida hizo ni;
  • Husaidia kupunguza vifo vya ghafla vya watoto hasa wawapo usingizini.
  • Hutuliza watoto wakorofi.
  • Humbembeleza mtoto na kumsaidia katika kupata usingizi haraka.
  • Huwapunguzia nafasi ya kusumbuliwa na mabadiliko ya hali ya hewa wawapo angani katika nyakati ambazo usafiri wa ndege unatumika.

Madhara
Haya ndiyo madhara yake;
  • Kuongeza uwezekano wa mtoto kupata maambukizi kwenye sehemu ya kati ya sikio ikiwa chuchu hiyo haisafishwi au kutunzwa kwenye mazingira safi
  • Kwa baadhi ya watoto husababisha kuota kwa meno yaliyopishana.
  • Husababisha mtoto akatae kunyonya maziwa ya mama. Hii hutokea kwa watoto wanaoanzishiwa matumizi ya chuchu bandia kabla hata hawajafikisha umri wa mwezi mmoja.
  • Huleta matatizo katika kutenganisha chuchu halisi ya mama yake na ile ya bandia. Inaweza kumsababishia apate upungufu wa virutubisho muhimu ambayo hupatikana kwenye maziwa ya mama pekee
  • Husababisha kujaa kwa gesi tumboni kwa watoto wanao inyonya haraka.
Faida za chuchu bandia huanza kupungua kadri mtoto anavyozidi kuwa mkubwa.

Baadhi ya watoto huacha kutumia chuchu hizi baada ya kufikisha miaka 2, wengine huendelea kusubiri hadi miaka 4 ndipo waache kabisa kuzitumia.

Muhimu
Ni muhimu kukumbuka mambo yafuatayo wakati wa kumpatia mtoto chuchu bandia-
  • Usimlazimishe aitumie hasa kwenye nyakati ambazo hataki
  • Usiweke kitu chochote kwenye chuchu bandia kama sehemu ya kumvutia mtoto aitumie (mfano asali, sukari n.k)
  • Nunua chuchu bandia yenye ukubwa unaoendana na kinywa cha mtoto
  • Mtoto anapokuwa analia, tumia njia zingine kwanza kumbembeleza kama nyimbo, massage pamoja na kumpiga piga mgongoni. Chuchu bandia iwe ni chaguo la mwisho baada ya kushindwa kwa njia hizi
  • Hakikisha kwanza kama mtoto hana njaa kabla hujampatia chuchu bandia.
Ikiwa utaamua kutumia, hakikisha unafuata ushauri wa kiusalama hasa katika kutunza usafi pamoja na kufuata masharti sahihi ya umri wa matumizi kwa mtoto.

Chanzo: Mayo Clinic
 
Back
Top Bottom