Dawa bandia ni tishio barani Afrika. Fahamu namna 3 za kuzibaini

jastertz

JF-Expert Member
Jul 4, 2020
392
743
Mwishoni mwa siku ndefu, unagundua kuwa unaanza kuhisi maumivu ya kichwa. Unachokifanya ni kunununua dawa za kutuliza maumivu kutoka kwa muuzaji wa mtaani, na unakunywa mbili. Lakini unajuaje tembe hizo ni sahihi ama sio feki? Muuzaji sio duka halisi la dawa lililothibitishwa. Hakuna kifungashio kinachoonyesha maelezo ya dawa na viwango ama vipimo vya kutumia. Je, itakuwaje ikiwa umejaribu kutibu kichwa chako kwa kutumia dawa feki ama bandia?

Neno "bandia" humaanisha dawa ambazo zimeghushiwa kimakusudi na kwa ulaghai. Pia huitwa dawa zilizo chini ya kiwango au zilizoghushiwa, ni dawa ambazo ziko chini ya vipimo na viwango vya ubora ambavyo vimeidhinishwa na mamlaka za udhibiti wa dawa.

Usizichanganye na dawa za asili - hizo ni za bei nafuu, lakini zimethibitishwa kisayansi kuwa ni salama na zenye ufanisi na zina hati miliki.

Dawa feki au bandia zinazojulikana zaidi huwa ni dawa maarufu zaidi: dawa za kutuliza maumivu, dawa za kutibu maambukizi, dawa za malaria, dawa za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi, za nguvu za kiume, au za kupunguza uzito.

Dawa bandia, feki au za kughushi ni tatizo kubwa katika nchi nyingi za Afrika. Utafiti umeonyesha kuwa nchi nyingi zinazoendelea zina kiwango kikubwa cha dawa zisizo na viwango. Kwa mfano, hadi asilimia 88.4% ya dawa za malaria katika baadhi ya masoko ya Afrika zimeripotiwa kuwa bandia. Kutumia dawa zisizo na ufanisi husababisha vifo kati ya 64,000 na 158,000 vinavyohusishwa na ugonjwa wa malaria kila mwaka katika eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Kuwapa watu dawa ambayo haitafanya kazi mwilini au haijatengenezwa vizuri kusaidia ugonjwa husika ni hatari. Zaidi ya watoto 250,000 duniani kote hufa kutokana na dawa feki kila mwaka. Katika mwaka uliopita pekee zaidi ya watoto 300 walikufa baada ya kutumia dawa feki za kikohozi au dawa za maumivu.

Juhudi za kukabiliana nazo
1. Nunua dawa katika maduka yaliyosajiliwa

Kwanza, nunua dawa zako kutoka kwa maduka ya rejareja yaliyo na leseni na kwenye zahanati - wanapaswa kubandika leseni zao kwenye kuta zao. Wafamasia na wasaidizi wao wamefunzwa jinsi ya kushughulikia dawa. Wanawajibika kisheria na kimaadili kwa dawa zilizo chini ya udhibiti wao. Hii inamaanisha kuwa watapata bidhaa kupitia njia rasmi za dawa ambazo kuna uwezekano mdogo wa kupenyezwa kwa dawa bandia.

Usinunue dawa kutoka kwa maduka ya dawa mtandaoni. Katika nchi nyingi za Kiafrika, hakuna maduka ya dawa halali mtandaoni. Mengi ni feki.

2. Ikague na kuihakiki dawa yako
dawa


Kagua bidhaa yako. Hakikisha kukagua na kusoma kifungashio cha dawa. Inapaswa kuwekewa lebo ya jina la bidhaa, maelezo ya mtengenezaji - kama vile jina lao na anwani ya mahali - na tarehe ya mwisho wa matumizi. Inapowezekana, angalia nambari ya kundi - hii ni 'serial number' ambayo inaweza kutumika kufuatilia ni lini na wapi bidhaa ilitengenezwa.

Ikiwa ni bidhaa uliyotumia hapo awali, jaribu kuilinganisha na vifungashio vya awali. Piga picha ya bidhaa ikiwa unaitumia mara kwa mara kwa kulinganisha katika siku zijazo.

3. Hakikisha bidhaa imefungwa vizuri na iko sawa
Fungua kifurushi na uhakikishe kuwa dawa iko sawa. Vidonge kwa kwenye pakti, kwa mfano, hakikisha kwamba hakuna aliyejaribu kuifungua. Kama vidonge hakikisha kwamba vinafanana bila kubadilika rangi, madoadoa (ngozi ya tembe inaonekana yenye marumaru), hazijapasuka au kuwa na ukungu.

Baadhi ya mabaki ya poda katika vidonge yanakubalika, lakini haipaswi kuwa mabaki ama poda nyingi sana. Hii inaweza kumaanisha kuwa vidonge havijabanwa vizuri. Haipaswi kuwa na harufu. Vidonge vinapaswa kung'aa na sio kupasuka, kunata au kukunjamana.

NB: Ukibaini dawa feki
Ikiwa unashuku kuwa dawa yako ni feki, haina ubora au bandia, basi unapaswa kuripoti mara moja kwenye mamlaka husika au mdhibiti wa kitaifa wa dawa. Kila nchi barani Afrika ina mamlaka ya kitaifa ya kudhibiti dawa kama mamlaka huru au ndani ya wizara ya afya.
 
Back
Top Bottom