Tume ya TEHAMA: Mahakama za Tanzania zinatumia Akili Bandia tangu Mwaka 2022

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
images.jpeg
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Tehama Tanzania, Kundwe Moses Mwasaga amesema Tume imeandaa Kongamano la Saba linalotarajiwa kufanyika tarehe 16-20 Oktoba 2023

Kongamano hilo litatanguliwa na mijadala, siku ya kwanza itakuwa ni Siku ya Wanawake kwenye TEHAMA, ambapo wanatarajia kusherekea mafanikio makubwa ambayo wametapata kwenyetasnia hiyo pamoja na changamoto.

Siku ya pili itakuwa ni siku ya vijana na lengo litakuwa lilelile la kusherekea pamoja na changamoto za TEHAMA, mbali na hapo wanatarajia kuwa na mada inayohusu Matumizi mbalimbali ya Teknolijia (Teknolojia Chipukizi).

Amesema “Tunatarajia kuangalia tenkolojia hizo zinachangia vipi maendeleo kwa Wanawake na vijana, hatua hiyo imefikiwa kwa kuwa taarifa za Sensa zinaonesha vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 34 wao takribani milioni 21.

“Vijana tunawategemea wawe watumiaji wakubwa wa digitali, ambapo tutajadiliana na changamoto na kuona tunaendeleaje.”

“Teknolojia ambayo tutaingalia sana ni akili bandia kwa kuwa ni fursa ambayo imejitokeza Duniani japokuwa watu wanatakiwa kuandaliwa katika matumizi ya teknolojia kama hizo.”

Aidha, amesema wanakaribisha wadau mbalimbali ikiwemo makampuni ya watu binafsi kushiriki katika kongamano hilo kwa kuwa kuna fursa nyingi za kujitangaza na kuonesha ubunifu wa kidigitali.

Pia katika Kongamano hilo kuna washiriki wanatarajia kushiriki kutoka mataifa ya Misri, Estonia, Kenya, Rwanda, Marekani, Finland, Urusi na nyingine zinaongezeka.

Kuhusu Akili Bandia
Amesema “Kwanza tunatarajia kusaini mkataba wa makubaliano na taasisi ambayo inayoonganisha watu ambao wanafanya ubunifu wao kwa kutumia akili bandia na umoja wao una wanachama zaidi ya 300.

“Hiyo itakuwa sehemu ya kuonesha Tanzania ipo tayari katika masuala ya TEHAMA nchini, watu wengi wanafikiri Tanzania tuko nyuma katika Akili Bandia, hapana.

“Teknolojia zimewezesha mashine kuwa na uwezo wa kufikiri katika uwezo ambao unakaribia kumfikia binadamu, Akili Bandia inaweza kuweka katika kifaa chochote kwa maana mashine inaweza kufanya maamuzi yenyewe.

“Katika Kongamano hilo kunatarajiwa kuwa na ubunifu mbalimbali uliofanywa na watu katika upande wa software na hardware ambao unaonesha Akili Bandia inavyoweza kutumika

“Akili bandia inahusika katika sekta zote za uchumi kama vile uchumi na kilimo, kwa mfano Tanzania Mahakama imekuwa ya kwanza kutumia Akili Bandia kufanya maamuzi mbalimbali tangu Mwaka 2022.

“Hivyo, kongamano hili litaonesha jinsi ambavyo Akili Bandia inavyoweza kutumia kufanya kazi yake vizuri na kuwa na mafanikio makubwa na sio vile ambavyo watu wanafikiri imekuja kuchukua ajira za watu.
 
Back
Top Bottom