Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,634
- 697,916
Hii kitu si ramli wala utabiri wa kubahatisha bali ni mchakato wenye matokeo yasiyozuilika wala kushindwa.. Ni mchakato unaoipeleka dunia na ulimwengu mahali ambako binadamu, mimea na viumbe hai vv yote vitakuwa si vitu vya asili tena bali vya kupangwa na kutokea kwa kutumia akili bandia tuu
Mifano ni mingi kutokea ujima zama za mawe mpaka hapa tulipo leo.. Kuna mabadiliko mengi mno makubwa na madogo yametokea na yanazidi kutokea
Kwasasa Mmarekani anafanya majaribio ya ndege ambazo zinaweza kukupeleka popote duniani kwa masaa mawili tuu.. Lakini huko tuendako muda utapungua mpaka kufikia dakika chache
Inawezekana kabisa kufikia kufumba na kufumbua umefika utakapo ama bila hata kusogeza mguu sehemu uitakayo itakuwa mbele yako at a click
Tukiachana na mifano migumu na ya mbali unakumbuka namna vile Shule za msingi tulivyokuwa tunakariri table ya 1 hadi ya 12? Leo ni watoto wetu wangapi wanaweza? Vikokotoo vimechukua akili zao
JF hii ya sasa ya kuumiza kichwa ili mtu aandike mada. Afikirie sana, awe na simu yenye network na chaji halafu iwe na bundle.. Kisha aanze kuandika heading halafu maudhui.. Na wakati wa kuandika akosee hapa na pale .. Aandike afutd.. Andike afute.. Hii tabu yote haitakuwepo tena!
Kwa kujua ama kutojua JF ya sasa inatengeneza kitu kikubwa sana ambacho vizazi vijavyo miaka 50 mbele havitakuwa na uwezo wa kutengeneza na vitaiona JF na wanachama wake watu waliokuwa na akili kubwa za kipekee na za ziada
Haya mabadiliko yameshaanza kutokea kwenye taaluma ya sanaa ya picha.. Hakuna ubunifu wa kuchora tena kwa kutumia akili binafsi na mikono.. Unaiamrisha tu akili bandia kupitia application maalum kile utakacho nayo ndani ya sekunde chache inakuletea vilevile ulivyotaka
Nimeliona hili pia kwenye vitu vingine vidogo vidogo lakini ndio hivyo akili zetu asilia zinaliwa taratibu na kirusi kibaya cha akili bandia
Huko tuendako hakutakuwa na haja ya kutumia muda mwingi, kuwaza kuumiza kichwa na kuandika mada .. Itakuwa ni mwendo wa kuamrisha akili bandia ikuandikie nayo ndani ya dakika mada kwa idadi ya maneno utakayo utakuwa tayari.. Na hili wala haliko mbali