Fahmi Dovutwa na ahadi ya kiwanda cha silaha!

nilipata taabu mwanzoni nikihisi labda "dovutwa" ndo jina la chama...
Ndani ya umaskini huu ukaweke kiwanda cha bunduki....hata ujumbe wa nyumba kumi haumfai..

yaani alisumbua watu huyu na jina lake! Baada ya kutoka kupiga kura watu wanajiuliza mbona tulisikia kuna mwanamke anagombea urais anaitwa devota sasa kwenye fomu tumeona picha za wanaume tu? Kumbe halikueleweka, badala ya dovutwa ikawa devota!
 
ha ha ha ha haaa! aliposikia tanzania kuna urenium ndipo akaja na hilo wazo! nadhani ana asili ya kikuria, maana huko kila mtu anawaza jeshi na silaha. Angeigeuza nchi kama korea kaskazini :teeth: Njaa kali lakini mna silaha za kutisha:eek:
 
Tanzania hatuhitaji kiwanda cha silaha utawala bora utakaosimamia rasilimal zetu kwa maslahi ya nchi. Huyu bila shaka alikosa sera za kushawishi watz wampigie kura
 
Jamani uchaguzi umeisha lakini ni tukio ambalo limeacha mijadala mingi vinywani mwa watanzania wote! Kuna kuchakachua! Kuchakachuliwa na mengineo mengi tu bado hayajaisha tutaendelea kujadiliana mpaka tuone mwisho wake.

Kwa upande wangu mimi ni kua katika zile ahadi lukuki kwa kila mgombea walivyoahidi bado tunasubiri tuone matekelezo yake bila ya kusahau ile ahadi ya kule kwa wakwe zangu KIGOMA kua DUBAI nyie acheni tu! Lakini ahadi zote zilikua na changamoto zake na ni zakufurahisha na kuleta matumaini kama kweli zitatekelezeka!

Kilichonipa msukumo wa kuandika hii topic ni ile ahadi ya yule mgombea kupitia chama cha UPDP Ndugu Fahmi Dovutwa kuahidi kua akipata ridhaa ya kupata kukalia kile kiti cha Urasi atajenga kiwanda cha silaha!

Jamani Greaty Thinkers naombeni mchango wenu huyu jamaa alikua anamaniisha nini kwenye taifa hili la amani tuwe na kiwanda cha silaha?

Angekuwa hajajitoa ningechangia kwa kuwa ningemuona mwenye akili ila kashindwa bahati mbaya. Ila kwa sababu alijitoa hatua za lala salama na kama mpinzani kuunga mkono chama tawala naweza kusema huyu ni wale CCM waliwaweka kuongea upuuzi ili wajenge hoja za wapinzania kuwa manunda na wasio na lolote la maana. MWISHO WAKE TUMEONA ANARUDI KUTIMILIZA ALILOTUMWA, KURA KWA KIKWETE!!!!!! MPUUZI TU HUYU NA ALIONGEA HAYA KATIKA UPUUZI WAKE
 
Ikiundwa tume huru ya uchaguzi,kabla ya kuchukua fomu za Uraisi wagombea wapimwe akili ili kutuepusha na watu kama Dovutwa
 
Dovutwa ni muumini wa dini ama madhehebu gani ambayo maadili ya dini yake haya mfudishi mtu KUISHI KWA AMANI NA JIRANI YAKE! Aliambiwa kipaumbele cha Watanzania ni silaha-hata wakurya sidhani!
 
Back
Top Bottom