Fahmi Dovutwa na ahadi ya kiwanda cha silaha!

Ndallo

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
7,622
2,000
Jamani uchaguzi umeisha lakini ni tukio ambalo limeacha mijadala mingi vinywani mwa watanzania wote! Kuna kuchakachua! Kuchakachuliwa na mengineo mengi tu bado hayajaisha tutaendelea kujadiliana mpaka tuone mwisho wake.

Kwa upande wangu mimi ni kua katika zile ahadi lukuki kwa kila mgombea walivyoahidi bado tunasubiri tuone matekelezo yake bila ya kusahau ile ahadi ya kule kwa wakwe zangu KIGOMA kua DUBAI nyie acheni tu! Lakini ahadi zote zilikua na changamoto zake na ni zakufurahisha na kuleta matumaini kama kweli zitatekelezeka!

Kilichonipa msukumo wa kuandika hii topic ni ile ahadi ya yule mgombea kupitia chama cha UPDP Ndugu Fahmi Dovutwa kuahidi kua akipata ridhaa ya kupata kukalia kile kiti cha Urasi atajenga kiwanda cha silaha!

Jamani Greaty Thinkers naombeni mchango wenu huyu jamaa alikua anamaniisha nini kwenye taifa hili la amani tuwe na kiwanda cha silaha?
 
Renegade

JF-Expert Member
Mar 18, 2009
6,271
2,000
Huyo bwana ni zamwamwa,mazamwamwa ni watu i wale ambao macho yao memeshindwa hata kuona umbai wa umbali wa pua zao wenyewe
Mbali ya kuwa hivyo lakini pia huyu jamaa alichakachuliwa!! kama hakuchakachuliwa alijichakachua.
 
Njowepo

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
9,536
2,000
dOVUTWAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA
Jina lake tuu huwa linaniacha hoi kwa wanaojua maana ya ilo jina tuambiane pls
Maana kuna jamaa mtaani kabatizwa ilo jina bse mission zake nyingi huishia kuangukia pua
 
Safari_ni_Safari

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
23,288
2,000
Funny enough alijitoa kwenye kinyang'anyiro lakini bado watu wakampa kura...na zingine CCM wakazimega kwao
 
Iza

JF-Expert Member
Jan 8, 2009
2,000
2,000
Nilipata taabu mwanzoni nikihisi labda "DOVUTWA" ndo jina la chama...
Ndani ya umaskini huu ukaweke kiwanda cha bunduki....hata ujumbe wa nyumba kumi haumfai..
 
Mabel

JF-Expert Member
Sep 1, 2010
1,217
2,000
Jamani uchaguzi umeisha lakini ni tukio ambalo limeacha mijadala mingi vinywani mwa watanzania wote! Kuna kuchakachua! Kuchakachuliwa na mengineo mengi tu bado hayajaisha tutaendelea kujadiliana mpaka tuone mwisho wake.

Kwa upande wangu mimi ni kua katika zile ahadi lukuki kwa kila mgombea walivyoahidi bado tunasubiri tuone matekelezo yake bila ya kusahau ile ahadi ya kule kwa wakwe zangu KIGOMA kua DUBAI nyie acheni tu! Lakini ahadi zote zilikua na changamoto zake na ni zakufurahisha na kuleta matumaini kama kweli zitatekelezeka!

Kilichonipa msukumo wa kuandika hii topic ni ile ahadi ya yule mgombea kupitia chama cha UPDP Ndugu Fahmi Dovutwa kuahidi kua akipata ridhaa ya kupata kukalia kile kiti cha Urasi atajenga kiwanda cha silaha!

Jamani Greaty Thinkers naombeni mchango wenu huyu jamaa alikua anamaniisha nini kwenye taifa hili la amani tuwe na kiwanda cha silaha?

Yawezekana jamaa alitaka Silaha kwa ajili ya biashara kwenye nchi zenye migogoro zinazo tuzunguka na tungepata fedha za kigeni. Jamani huu mtazamo wangu tu maana wengi wanafanya biashara ya silaha
 
Lambardi

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
12,497
2,000
Dovutwaa...alishavutwa na jk akapewa hela ya kampeni kujaribu kuonyesha kuwa........kila mtu ana haki kugombea urais na kujaribu kugawa kura za wapinzani....hana lolote ni pandikizi binafsi la jk tuu.....anajenga kiwanda silaha wakati wananchi wanakufa njaa....na wanaumwa...sasa anauza silaha akanunue sembe na panadol..nje?akili hiyoo?/
 
sheiza

JF-Expert Member
Sep 29, 2010
5,434
2,000
huyu jamaa ni ndondocha la ccm.. alishindwa hata kuandika jina lake kwenye fomu ya urais..matokeo yake akaomba kura zake apewe kikwete....eti italeta shida wakati wa kuapishwa jina lake kama angeshinda..anadhani watu wanapiga kura ovyo....
 
Kamongo

JF-Expert Member
Mar 20, 2009
1,102
2,000
hili jamaa ni poyoyo sana alinikera sana aliposema amejitoa,nasikia ni dalali wa magari pale Lumumba
 
Ehud

JF-Expert Member
Feb 12, 2008
2,686
0
huyu jamaa kajitoa lakini kwenye kutangazwa matokea kaenda

Halafu walipoitwa wagombea kwenda kuwashika mkono wajumbe wa NEC yeye hakwenda akabaki ame-pose kwenye kiti chake akiwa amevaa kofia yake ya Kibanga ampiga mkoloni!
 
Utotole

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
6,608
2,000
Huyu jamaa ni wa ajabu ajabu tu kuanzia mavazi yake, haiba yake, sera zake hadi maamuzi yake
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom