Halmashauri Kuu Taifa ya Chama cha (UPDP) imemvua uenyekiti Fahmi Dovutwa kwa kufanya kosa la kukisemea chama hicho kinyume na Katiba

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,852
141,786
Chama cha UPDP kimemvua madaraka Mwenyekiti wake mzee Dovutwa baada ya kuvunja katiba ya chama hicho.

Dovutwa aliungana na Mbowe wa Chadema kujitoa kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa ilhali katiba ya UPDP haina kipengere kinachoruhusu chama chao kujitoa kwenye uchaguzi wowote.

Dovutwa atabakia kuwa mwanachama wa kawaida.

Chanzo: Star tv habari

Maendeleo hayana vyama!

=====


pic+dovutwa.jpg

Halmashauri Kuu Taifa ya Chama cha United People's Democratic Party (UPDP) imemvua uenyekiti Fahmi Dovutwa baada ya kubainika kufanya kosa la kukisemea chama hicho kinyume na katiba.

Uamuzi huo ulitangazwa jana Jumapili Desemba 2, 2019 Mjini Unguja, Zanzibar na Kaimu Mwenyekiti wa UPDP Taifa, Abdalla Mohammed Khamis akisema uamuzi huo umefikiwa baada ya kikao hicho kujadili kwa kina makosa alioyafanya Dovutwa.

Alisema kosa kuu lililopelekea kuvuliwa kwa wadhifa wake ni kukisema chama hicho kuwa hakitoshiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa uchaguzi uliofanyika Novemba 24, 2019 Tanzania Bara kitendo ambacho alikifanya bila kuagizwa wala kupata ridhaa ya uongozi wa chama hicho.

"Alichokifanya Fahmi ni kukiuka katiba ya chama chake kwani hakupaswa kabisa kukisemea, uhalali wa kushirikiana au kutoshiriki uchaguzi huo na tunafanya hivi ili iwe ni funzo kwa viongozi wengine waliomo ndani ya chama na wanaokuja," alisema Kaimu mwenyekiti huyo.

Alisema suala la chama hicho kutoingia katika uchaguzi wa serikali za mitaa imekiathiri kwani utekelezaji wa agizo alilotoa Dovutwa limesababisha chama kukosa wenyeviti wa serikali hizo ambao wataweza kuwakilisha chama.

Khamis alisema Dovutwa anaweza kukata rufaa endapo atahisi amevunjiwa haki yake kisheria na kikatiba na kwa sasa atabaki kuwa mwanachama wa kawaida.

Pia, alisema kikao hicho kilimteua Twalibu Ibrahim Kadege kuwa naibu Katibu mkuu, ambapo kabla ya uteuzi nafasi hiyo ilikuwa wazi.

Mwananchi limemtafuta Dovutwa amesema atafutwe baadaye kwani yuko safarini kutoka Zanzibar kwenda Dar es Salaam.

Itakumbukwa, UPDP ilikuwa miongoni mwa vyama sita vilivyosusia uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika Novemba 24, 2019.

Vyama vingine ni; Chadema, NCCR-Mageuzi, CUF, Chaumma na ACT-Wazalendo.


Chanzo: Mwananchi
 
Hizo habari sidhani kama utampata aliye interest kuzijadili. Ungeishia nazo kwenye korido za Lumumba ingetosha.
CCM na branch zenu mtajuana, labda utueleze baada ya Dovutwa mmempanga nani?
Ulivyojadili wewe imetosha.

Safari hii hainaga Ushemeji.....by F T Sumaye!
 
Hao UPDP wanapingana na kauli " Kujitoa nayo ni democrasia"......JPM
 
Back
Top Bottom