FortJeasus
JF-Expert Member
- Jan 19, 2012
- 603
- 397
Miongoni mwa wanasiasa wapuuzi niliopata kuwajua,Fahmi Nassoro Dovutwa,mwenyekiti wa chama cha UPDP(sitaki kujua hata kirefu chake) ni mojawao.
Mwaka 2010 alijitoa katika kinyanganyiro cha Uchaguzi Mkuu alipokuwa anawania nafasi ya Urais kwa sababu za kipuuzi ambazo nisingependa kuzirejea hapa.Si vibaya kukumbusha kuwa,wakati akiendesha kampeni zake wakati huo,moja ya vipaumbele vyake ilikuwa kuanzisha kiwanda cha silaha kwa madhumuni ya kuinua mauzo ya nje pamoja na matumizi ya ndani ili kuimarisha usalama wa rai na mali zao pamoja na ulinzi wa taifa kwa ujumla!
Kwa sasa huyu mwananchi mwenzetu dhaifu mno kifikra na kimatendo yupo Dodoma ''akitunga'' Katiba!Badala ya kutoa mchango wake wa mawazo kuhusu Rasimu ya Pili ya Katiba,kipaumbele kwake ni maudhui ya mkutano wa TCD na Rais siku ya jumatatu iliyopita.Hapa chini nimeweka maelezo yake,kutoka gazeti la Mwananchi,ili kila mmoja wetu aone namna watu wanaojiita wanasiasa wanavyofikiri na kutenda.
Chanzo:Mwananchi

Dodoma. Sumu iliyomwagwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Seif Shariff Hamad imeanza kuwatafuna baadhi ya viongozi Taasisi ya Demokrasia nchini (TCD), akiwamo mwenyekiti wake, John Cheyo.
Akiwa mkoani Mwanza, Maalim Seif aliwatuhumu viongozi watatu wa TCD kuwa ni wasaliti kwa kile alichodai kukataa kusaini makubaliano kati ya Rais Jakaya Kikwete na viongozi hao walipokutana Dodoma Septemba 8.
Maalimu Seif alisema Cheyo, Mwenyekiti wa Taifa wa TLP, Augustino Mrema na Mwenyekiti wa UPDP, Fahmi Dovutwa hawakutia saini makubaliano hayo.
Waliotajwa kutia saini ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbroad Slaa.
Hata hivyo, akizungumza bungeni mjini Dodoma jana, Dovutwa alisema kauli hiyo ya Maalim Seif imemletea matatizo makubwa kwa vile tayari ameanza kupokea vitisho vya maisha yake.
Dovutwa alisema katika kikao chao na Rais Septemba 8 walikubaliana mambo mawili ya msingi, moja kuifanyia marekebisho Katiba ya sasa na pili Bunge liendelee hadi litakapofikia ukomo wake Oktoba 4.
"Suala hili limeshaleta chuki kwenye jamii na wengine maisha yetu yameshakuwa katika matatizo kwa kauli ya kiongozi mmoja mkuu wa Serikali kutoka CUF," alisema.
Alisema kitendo cha wao kukubaliana halafu viongozi wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na kumwacha yeye, Mrema, Cheyo na Mangula kuzungumza na wanahabari kilikuwa ni kitendo cha hatari.
"Document (nyaraka) inayosemwa sisi tulikataa kuisaini, tulikataa kuisaini kwa sababu ilikuwa na mitego. Ile ‘document' tumeambiwa tusaini dakika za mwisho kwenda mlangoni kwa Rais hatukuwa na muda wa kuisoma,"alisema.
Kwa mujibu wa Dovutwa, katika nyaraka hiyo kulikuwa na kipengele cha hatari ambacho kilikuwa kinataka Bunge lisitishwe na baada ya kusitishwa, itungwe sheria kumdhibiti Rais ajaye mara baada ya kuingia madarakani aitishe mjadala wa Bunge la Katiba.
"Kama hivyo ndivyo, yaani Rais anaingia madarakani mnamtwisha na mgogoro.
Nchi itakalika? Kwa hiyo tunakwenda pale mwanzo kwamba hawataki nchi itawalike,"alisisitiza.
Chanzo:Mwananchi