JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 625
- 938
Ni rahisi kuhisi kuzidiwa na kila kitu unachosikia kuhusu #COVID_19. Inaeleweka pia ikiwa watoto wako wanahisi wasiwasi. Watoto wanaweza kupata shida kuelewa kile wanachokiona mtandaoni au kwenye Runinga - au kusikia kutoka kwa watu wengine - kwa hivyo wanaweza kuwa katika hatari ya kuhisi wasiwasi, mafadhaiko na huzuni. Lakini kuwa na mazungumzo ya wazi na watoto kunaweza kuwasaidia kuelewa na kukabiliana na ugonjwa huu
Katika kuzungumza na watoto kuhusu mlipuko huu fuata nji ahizi zifuatazo;
1. Uliza maswali ya wazi na sikiliza
Fahamu kwanza anajua nini kuhusu #Corona na muache aongoze mazungumzo. Thamini hisia zake na muahakikishe kuwa ni kawaida kuhisi hofu juu ya vitu hivi. Kama ni mdogo na hajui kuhusu Corona, unaweza usimwambie ili usimpe hofu mpya ila mfundishe kuhusu usafi kwa ujumla
Hakikisha uko katika mazingira salama na umruhusu mtoto wako azungumze kwa uhuru. Mchoro, hadithi na shughuli zingine zinaweza kusaidia kufungua mjadala
Onyesha kuwa unasikiliza kwa kuwapa umakini wako kamili, na hakikisha wanaelewa kuwa wanaweza kuzungumza na wewe wakati wowote wanapotaka.
2. Kuwa mwaminifu, eleza ukweli kwa njia rafiki mtoto
Watoto wana haki ya kupata taarifa ya kweli juu ya kile kinachotokea ulimwenguni, lakini watu wazima pia wana jukumu la kuwalinda ili wasipate mawazo. Kama hujui jibu la swali lake usibahatishe, tumia nafasi hiyo kutafuta majibu pamoja hata mtandaoni
3. Waoneshe namna ya kujinda na #CoronaVirus
Wahamasishe kunawa mikono mara kwa mara. Haihitaji kuwa mazungumzo ya kutisha. Pia unaweza kuwafunsha kupiga chafya au kukohoa na kujizuia kwa kutumia sehemu ya ndani ya kiwiko. Waambie wakueleze watakapoanza kuhisi dalili za ugonjwa huo
4. Bila Kuwatisha waeleze kwa namna mapambano yanavyoendelea
Waeleze kwa namna wafanyikazi wa afya, wanasayansi na watu wengine ambao wanafanya kazi kuzuia kuenea kwa #COVID19 na kuweka jamii salama. Inaweza kuwa faraja kubwa kujua kwamba watu wenye huruma wanachukua hatua
5. Funga mjadala kwa kuonesha kujali na kutoa uhakika
Ikiwa unakabiliwa na mlipuko katika eneo lako, wakumbushe watoto wako kwamba hawawezi kupata ugonjwa huo kirahisi, kwamba watu wengi wenye ugonjwa huo hawaugui sana na kuwa jitihada zinaendelea kuzuia maambukizi
Wakumbushe watoto wako kuwa wanaweza kuwa na mazungumzo mengine magumu na wewe wakati wowote. Wakumbushe kwamba unajali, unasikiliza na unapatikana kila wanapohisi kuwa na wasiwasi