Fahamu: Nchi Zinazoitwa kwa Majina Tofauti na Yanayofahamika kwenye Ramani ya Dunia

Sam Gidori

Senior Member
Sep 7, 2020
165
414
Zipo sababu nyingi za nchi kufahamika kwa jina lililopo, baadhi ya sababu hizo ikiwa ni pamoja na lugha ya asili ya wazungumzaji, wageni au wafanyabiashara waliofika katika eneo hilo, jina la mtu maarufu au eneo maarufu katika nchi hiyo nk. Hakuna sababu moja iliyosababisha kila nchi kupata jina lake.

Baadhi ya nchi zilipata majina yao kwa bahati mbaya, mfano Canada, ambayo ilipaswa kuitwa 'Kanata' ikimaanisha Kijiji baada ya mpelelezi Jacques Cartier kukutana na wenyeji wa eneo hilo katika karne ya 16. Matumizi ya majina katika baadhi ya nchi yamebadilika kulingana na wakati, mfano Kisiwa cha Taiwan kilijulikana nchini Uingereza kama 'Formosa' jina lililotokana na wasafiri wa Kihispania likimaanisha 'Kisiwa Kizuri' na jina hili liliendelea kutumika hadi mwanzoni mwa karne ya 20.

Lakini si nchi zote zinazofahamika kwa jina lililopo katika orodha ya nchi zinazofahamika na Umoja wa Mataifa zinaitwa hivyo na wenyeji (wakazi) wa nchi hizo.

Hii ni orodha ya majina ya nchi zinavyoitwa na wenyeji tofauti na inavyofahamika katika ramani ya dunia.

NchiLughaJina Lingine (Local Name)
Albania KialbaniaShqipëria
AlgeriaKiarabu, BerberDzayer
ArmeniaKiarmeniaHayatsán
BhutanDzongkhaDruk Yul འབྲུག་ཡུལ
CambodiaKhmerKampuchea កម្ពុជា
ChinaKimandarini, KichinaZhōngguó 中国
CroatiaKikroatiaHrvastka
EgyptKiarabuمص Misr
FinlandKifini, KiswidiSuomi
GeorgiaKigeorgiaSak'art'velo საქართველო
UjerumaniKijerumaniDeutschland
UgirikiKigirikiHellas Ελλάς
IndiaKihindi, Bengali, Tamil, Telugu, n.kBhārat ભારત
JapanKijapaniNippon 日本
Korea KaskaziniKikoreaChosŏn 조선
Korea KusiniKikoreaHanguk 한국 Namhan 남한
MaldivesDhivehiDhivehi Raaje
MauritaniaKiarabu, BererAgawec
MontenegroKimontenegroCrna Gora Црна Гора
MoroccoKiarabu, BerberAl-maɣréb المغرب, Amerruk
New ZealandKiingereza, KimaōriAotearoa


Countrie Local Names.png
 
Mozambique - Msumbiji
South Africa - Mzansi
Tanzania - Bongo
 
Tofauti hizo zipo nyingi sana. Mifano michache; sisi twawaita Uingereza wao wajiita England; Marekani vs America; Ufaransa vs France; Ureno vs Portugal; n.k.
 
Back
Top Bottom