Fahamu mita za LUKU zinazofungwa majumbani

Fahamu mita za LUKU zinazofungwa majumbani

Nimenunua umeme wa sh 9000 nikapewa unit 68.8 badala ya unit 73.8, tatizo nn?
 
mkuu swali..
nmefungiwa umeme jumanne, mita imefungwa kwenye nguzo..
tatizo usiku inatokea umeme unakatika na kurud kwa jiran zangu unakuwepo ila kwangu inakuwa kama mchezo
hasa mida ya kuanzia saa mbil usiku mpaka saa nne mchana haitokei..
shida ni nin

yaani una tatizo Kama nililokuwa nalo.
Pole Sana.
 
Kwahili leo TANESCO mmefanya la maana kutoa elimu kama hii hapa Jamii Forums, Kwanini mmetofautisha tariffs kwa mteja mkubwa na mdogo per unit? Wakati unit moja ni hiyo hiyo mega watts 1000 au KWH 1
Nahosi KW 1000 ndiyo MW 1. Nadhani umechanganya.
 
Asante kwa taarifa ila nina swali moja maana nilishapitia kwenye office zenu sikupewa jibu katika hili kuna nyumba moja nataka niunganishe umeme sasa mimeongea nao wanaoishi hapo wao wamekataa sasa mimi nataka niunganishe vyumba vitatu sababu wanakaa watu wa muhimu sana wanavyo kaa kiza roho inaniuma nimepanga niwanunulie solar lakini naona nitaingia gharama sababu watapoongeza matumizi itabidi niongeze uwezo wa solar tena
 
Umemjibu very economical sijui kama ataelewa
Mkuu ninaomba unijibu haka kaswali

Nilifanikiwa kununua kibanda...sijahamia nikakipangisha...

nami nimepanga apartment tupo watatu tunatumia luku moja...pana jamaa mmoja aliamua kumtafuta fundi...anadai hana matumizi kama sisi wawili...vitu vyetu ni kama mapangaboi..fridges...majiko ya umeme...vacuum...za kunyonya vumbi...nk....kumbuka apartment zina sehem nyingi..choo..bafu..vyumba vitatu..jiko nk. sasa fundi akamuwekea kadude flan kakupimia kiasi cha umeme anachotumia...sisi wawili kulipa sio hoja kwa kuwa kula maisha tunapenda...

swali..huyu ni sahihi kweli kuwa kidude chake kitapima umeme wake tuuu.

tulisema "yeye asome kidude sisi tutanunua umeme tutumie" hiyo tumeamua iwe slogan yetu kwa sababu utumwa spendi. Yaani niliona wapangaji tunakuaga maboya sana. Ni bora kuweka mita yako kuliko haka kadubwasha....kama uhalisia wowote au ndio ushamba?
 
Mkuu ninaomba unijibu haka kaswali

Nilifanikiwa kununua kibanda...sijahamia nikakipangisha...

nami nimepanga apartment tupo watatu tunatumia luku moja...pana jamaa mmoja aliamua kumtafuta fundi...anadai hana matumizi kama sisi wawili...vitu vyetu ni kama mapangaboi..fridges...majiko ya umeme...vacuum...za kunyonya vumbi...nk....kumbuka apartment zina sehem nyingi..choo..bafu..vyumba vitatu..jiko nk. sasa fundi akamuwekea kadude flan kakupimia kiasi cha umeme anachotumia...sisi wawili kulipa sio hoja kwa kuwa kula maisha tunapenda...

swali..huyu ni sahihi kweli kuwa kidude chake kitapima umeme wake tuuu.

tulisema "yeye asome kidude sisi tutanunua umeme tutumie" hiyo tumeamua iwe slogan yetu kwa sababu utumwa spendi. Yaani niliona wapangaji tunakuaga maboya sana. Ni bora kuweka mita yako kuliko haka kadubwasha....kama uhalisia wowote au ndio ushamba?
Mkuu kufunga mita binafsi si ushamba. Ila ni kutafuta idadi kamili ya Units unazo tumia ili uweze kulipia. Kama ulivyo sema kuwa ww na jamaa yako mna appliances nyingi lakini yeye ana vifaa vichache. Cha ajabu unaweza kuta mnachanga pesa sawa kwa ajili ya matumiz ya umeme. Jamaa hapendi kunyonywa ndio maana ameamua kufunga kamita kake. So akitumia lets say units 25 kwa mwezi na kila unit inauzwa mf. 400 katika tariff mliyopo basi jamaa atalipia sh. Units 25 × sh. 40 = 10,000/=

So jamaa amefanya uamuzi sahihi kabisa amekwepa kulipa gharama ambazo yeye hatumii

Hata ww ukihisi unalipa gharama zaidi ya unavyo tumia basi waweza weka na ww kamita kako
 
Mkoa wa Tabora mita zimeadimika,mwezi unaisha hakuna,maombi ya kufungiwa umeme kimya!Ni janga la kitaifa au ni Tabora Tu?
 
Mie nina tatizo la Batani za Mita yangu kuna muda zinasumbua kama wiki iliyopita umeme uliisha nikanunua unit, kwenda kuweka batan kama 3 hazikubali ku respond je tatizo kama hilo linahitaji kubadilishwa Mita au?
 
Asante kwa maelezo mazuri TANESCO.

Umesema sababu mojawapo ya umeme kupotea ni earth lod kutokuwa shaba halisi.

Naomba kujua sababu zingine zinazoweza kuleta leakage ya umeme kwenye nyumba.

Lakini pia, taarifa za mtaani zinasema ni vizuri kuweka chumvi na mkaa pale kwenye earth lod. Je hii inasaidia umeme kutokupotea?
Ndio inasaidia kutokupotea kwa umeme
 
Wateja wetu wengi wamekuwa wakijiuliza iwapo wamefungiwa mita sahihi kutokana na matumizi yao ya umeme? Ama mita ambazo wamefungiwa ni za Viwandani na kulalamika wanatumia umeme mwingi zaidi tofauti na matumizi wanayotumia

Mita za LUKU zinazofungwa majumbani ni sahihi kwa matumizi ya nyumbani, ufungaji wa mita za majumbani hutegemea sana upimwaji wa matumizi /mahitaji ya umeme katika nyumba husika.

Mteja anafanyiwa tadhimini kabla ya kuunganishiwa umeme, wakati wa uunganishaji wa umeme inaangaliwa maombi kama Mteja ameomba kufungiwa njia moja (single phase) ama njia tatu (three phase) na haiwezekani Mteja aombe njia moja ya umeme afungiwe njia tatu.

Iwapo matumizi ya umeme ya Mteja yakiongezeka kufika unit 7500 hapo atalazimika kutumia mita za njia tatu (three phase) zenye uwezo wa Volts 400 kutoka mita ya njia moja yenye Volts 220 -250.

Wateja wengi hawafahamu hasa anapo tumia umeme ukafikia units 300 anadhani TANESCO ilikosea kumfungia umeme/mita. Sio kweli, kinachotakiwa ni Mteja kuwa na matumizi mazuri ya umeme ili kupunguza gharama.

Aidha, mita za LUKU za njia tatu kwa baadhi ya Wateja wenye mahitaji makubwa ya umeme wamefungiwa majumbani mwao hasa ambao tangu tathmini inafanyika ilionekana mahitaji ya umeme yatafika units 7500 maeneo mengine ni ya Kibiashara na ambako matumizi ya umeme wa njia moja hautofaa huwa wanafungiwa huo wa njia tatu.

Kwa wastani wa units 10 usiku na 6 mchana maana yake Mteja ana zaidi ya units 300 kwa mwezi yaani 16x30 utapata units mia nne (400) hayo si matumizi madogo, pia yapo mambo mengi ya kuyaangalia linapokuja suala la matumizi ya umeme, cha kwanza hiyo mita iko sahihi? TANESCO huwa inapima mita kulingana na maombi ya Mteja, ikiwa itagundulika kuwa mita ni mbovu Mita hiyo huondolewa eneo la Mteja, na Mteja atasahihishiwa account zake kulingana na kile kipindi mita haikusoma ipasavyo,

Jambo la pili ni Mteja anatakiwa kukagua mfumo wa umeme wa nyumba yake na kuhakikisha hakuna hitilafu (leakage) yoyote inayo pelekea umeme kuvuja na kumuongezea matumizi Mteja (Wiring system) na pia Mteja kuhakikisha earth load iwe shaba halisi.

Tatu ni vifaa anavyo tumia Mteja vina uwezo gani wa kutumia umeme? Nirahisi ku hesabu umeme tunaotumia na kutoa malalamiko kwa TANESCO, na Shirika litafanya ukaguzi ili kubaini matumizi hayo pengine ni sahihi, kila kifaa kina kiasi cha umeme kinachotumia kwa dakika ama masaa kadhaa. Inashauriwa Mteja kutumia vifaa vinavyotumia umeme mdogo (Energy Server), pia inashauriwa kuepuka vifaa vya mitumba sababu vingi vinatumia umeme mwingi.


Inachulua muda gani kati ya kulipia na kufungiwa mita?
 
Ahsante lkn naona maswali mengi hayajajibiwa Mimi binafsi niko mjini lkn. Matumizi yangu ni chini ya hizo unit75.lkn nimekua nikinunua Umeme kwa tsh 292/kutokana na tariff je nifanyeje ili nibadilishiwe hiyo tariff.....,????
 
Hivi Mita zote za tanesco zinatoka dsm. Nipo huku Arusha naambiwa kupata umeme hadi nisubiri mita isajiliwe na usajili unafanyika dsm kwahio nisubiri. Kwa mawazo yangu madogo naona hii haijakaa vizuri coz hata huku naamiini wanaweza kuzisajili. Jamani naombeni msaada
 
Aliekupa taarifa kama ni mtaani amekupa taarifa ambazo sio sahihi.

Ukitaka kutatua tatizo lako fika ofisi ya Tanesco hapo Arusha utasaidiwa
 
Jamani hizi luku mpya za tanesco nadhani kuna kitu wameziwekea aisee zinakulaa sanaa Umeme sio kawaidaa kabisaaa...!! Au ndo hapaa kazii tuu mnatafuta namna ya kukusanya Mapato mjenge Jengo jipya..!??? TANESCO kwa hili Hapanaa mnatuonea..
 
Back
Top Bottom