Fahamu mita za LUKU zinazofungwa majumbani

TANESCO

Official Account
Jul 12, 2014
4,595
2,115
Wateja wetu wengi wamekuwa wakijiuliza iwapo wamefungiwa mita sahihi kutokana na matumizi yao ya umeme? Ama mita ambazo wamefungiwa ni za Viwandani na kulalamika wanatumia umeme mwingi zaidi tofauti na matumizi wanayotumia

Mita za LUKU zinazofungwa majumbani ni sahihi kwa matumizi ya nyumbani, ufungaji wa mita za majumbani hutegemea sana upimwaji wa matumizi /mahitaji ya umeme katika nyumba husika.

Mteja anafanyiwa tadhimini kabla ya kuunganishiwa umeme, wakati wa uunganishaji wa umeme inaangaliwa maombi kama Mteja ameomba kufungiwa njia moja (single phase) ama njia tatu (three phase) na haiwezekani Mteja aombe njia moja ya umeme afungiwe njia tatu.

Iwapo matumizi ya umeme ya Mteja yakiongezeka kufika unit 7500 hapo atalazimika kutumia mita za njia tatu (three phase) zenye uwezo wa Volts 400 kutoka mita ya njia moja yenye Volts 220 -250.

Wateja wengi hawafahamu hasa anapo tumia umeme ukafikia units 300 anadhani TANESCO ilikosea kumfungia umeme/mita. Sio kweli, kinachotakiwa ni Mteja kuwa na matumizi mazuri ya umeme ili kupunguza gharama.

Aidha, mita za LUKU za njia tatu kwa baadhi ya Wateja wenye mahitaji makubwa ya umeme wamefungiwa majumbani mwao hasa ambao tangu tathmini inafanyika ilionekana mahitaji ya umeme yatafika units 7500 maeneo mengine ni ya Kibiashara na ambako matumizi ya umeme wa njia moja hautofaa huwa wanafungiwa huo wa njia tatu.

Kwa wastani wa units 10 usiku na 6 mchana maana yake Mteja ana zaidi ya units 300 kwa mwezi yaani 16x30 utapata units mia nne (400) hayo si matumizi madogo, pia yapo mambo mengi ya kuyaangalia linapokuja suala la matumizi ya umeme, cha kwanza hiyo mita iko sahihi? TANESCO huwa inapima mita kulingana na maombi ya Mteja, ikiwa itagundulika kuwa mita ni mbovu Mita hiyo huondolewa eneo la Mteja, na Mteja atasahihishiwa account zake kulingana na kile kipindi mita haikusoma ipasavyo,

Jambo la pili ni Mteja anatakiwa kukagua mfumo wa umeme wa nyumba yake na kuhakikisha hakuna hitilafu (leakage) yoyote inayo pelekea umeme kuvuja na kumuongezea matumizi Mteja (Wiring system) na pia Mteja kuhakikisha earth load iwe shaba halisi.

Tatu ni vifaa anavyo tumia Mteja vina uwezo gani wa kutumia umeme? Nirahisi ku hesabu umeme tunaotumia na kutoa malalamiko kwa TANESCO, na Shirika litafanya ukaguzi ili kubaini matumizi hayo pengine ni sahihi, kila kifaa kina kiasi cha umeme kinachotumia kwa dakika ama masaa kadhaa. Inashauriwa Mteja kutumia vifaa vinavyotumia umeme mdogo (Energy Server), pia inashauriwa kuepuka vifaa vya mitumba sababu vingi vinatumia umeme mwingi.
 
Ahsante mkuu.

Naomba kuuliza kwa wateja wapya mnatoa luku za aina gani ni zile mnazotundika LUKU kwenye nguzo na mteja anabakiwa na remote ya ku recharge?

Kama ni hivyo mbona wengine luku wanawekewa kwenye nguzo na wengine hawawekewi? je ni mteja anaomba au ni vigezo gani mnatumia kwa sasa. Ahsante
 
LUKU zinawekwa mahali ambapo TANESCO wanaona salama.

ukichukulia wateja wapo 20 ni vigumu kufunga mita 20 kwenye nguzo hivyo ndio maana nyingine zinawekwa majumbani juu ambapo Mteja hawezi kufika mahali salama
 
Swali, inakuwaje pale mteja yupo kwenye nyumba ya kupanga/ chumba cha biashara na akafuata taratibu zote za kutaka kufungiwa mita yake pekeyake na akafungiwa baadaye akahama lakini akataka ahamishe na hiyo mita lakini Tanesco wanamkatalia? hii nimeiona sana songea, mbaya zaidi mteja anahama kwenye chumba cha biashara na hicho chumba kikakosa mpangaji mita zinakaa tu bila kitumika.
 
Tanesco mimi nashida hapa napokaa! Kila baada ya siku mbili umeme lazima ukate kwetu huku majirani wakiwa na umeme muda wote ukiuliza shida nini? Unaambiwa line yetu ina tatizo! Is that fair kweli? Imekuwa too much sasa hapa Urafiki Maeneo ya Kiliman hospital hazipiti siku mbili umeme unakata line ya nyumba nne tu kisingizio line yetu na hata umeme ukikata mtaa mzima na ukirud kwetu haurud kwa wakati kwa kisingizio cha line yetu ina tatizo
 
mkuu swali..
nmefungiwa umeme jumanne, mita imefungwa kwenye nguzo..
tatizo usiku inatokea umeme unakatika na kurud kwa jiran zangu unakuwepo ila kwangu inakuwa kama mchezo
hasa mida ya kuanzia saa mbil usiku mpaka saa nne mchana haitokei..
shida ni nin
 
Wateja wetu wengi wamekuwa wakijiuliza iwapo wamefungiwa mita sahihi kutokana na matumizi yao ya umeme? Ama mita ambazo wamefungiwa ni za Viwandani na kulalamika wanatumia umeme mwingi zaidi tofauti na matumizi wanayotumia

Mita za LUKU zinazofungwa majumbani ni sahihi kwa matumizi ya nyumbani, ufungaji wa mita za majumbani hutegemea sana upimwaji wa matumizi /mahitaji ya umeme katika nyumba husika.

Mteja anafanyiwa tadhimini kabla ya kuunganishiwa umeme, wakati wa uunganishaji wa umeme inaangaliwa maombi kama Mteja ameomba kufungiwa njia moja (single phase) ama njia tatu (three phase) na haiwezekani Mteja aombe njia moja ya umeme afungiwe njia tatu.

Iwapo matumizi ya umeme ya Mteja yakiongezeka kufika unit 7500 hapo atalazimika kutumia mita za njia tatu (three phase) zenye uwezo wa Volts 400 kutoka mita ya njia moja yenye Volts 220 -250.

Wateja wengi hawafahamu hasa anapo tumia umeme ukafikia units 300 anadhani TANESCO ilikosea kumfungia umeme/mita. Sio kweli, kinachotakiwa ni Mteja kuwa na matumizi mazuri ya umeme ili kupunguza gharama.

Aidha, mita za LUKU za njia tatu kwa baadhi ya Wateja wenye mahitaji makubwa ya umeme wamefungiwa majumbani mwao hasa ambao tangu tathmini inafanyika ilionekana mahitaji ya umeme yatafika units 7500 maeneo mengine ni ya Kibiashara na ambako matumizi ya umeme wa njia moja hautofaa huwa wanafungiwa huo wa njia tatu.

Kwa wastani wa units 10 usiku na 6 mchana maana yake Mteja ana zaidi ya units 300 kwa mwezi yaani 16x30 utapata units mia nne (400) hayo si matumizi madogo, pia yapo mambo mengi ya kuyaangalia linapokuja suala la matumizi ya umeme, cha kwanza hiyo mita iko sahihi? TANESCO huwa inapima mita kulingana na maombi ya Mteja, ikiwa itagundulika kuwa mita ni mbovu Mita hiyo huondolewa eneo la Mteja, na Mteja atasahihishiwa account zake kulingana na kile kipindi mita haikusoma ipasavyo,

Jambo la pili ni Mteja anatakiwa kukagua mfumo wa umeme wa nyumba yake na kuhakikisha hakuna hitilafu (leakage) yoyote inayo pelekea umeme kuvuja na kumuongezea matumizi Mteja (Wiring system) na pia Mteja kuhakikisha earth load iwe shaba halisi.

Tatu ni vifaa anavyo tumia Mteja vina uwezo gani wa kutumia umeme? Nirahisi ku hesabu umeme tunaotumia na kutoa malalamiko kwa TANESCO, na Shirika litafanya ukaguzi ili kubaini matumizi hayo pengine ni sahihi, kila kifaa kina kiasi cha umeme kinachotumia kwa dakika ama masaa kadhaa. Inashauriwa Mteja kutumia vifaa vinavyotumia umeme mdogo (Energy Server), pia inashauriwa kuepuka vifaa vya mitumba sababu vingi vinatumia umeme mwingi.
Mimi natumia unit 60 kwa mwezi,lakini nimeenda ili wanihamishie tariff ndogo wanasema mpaka nikae miezi sita mara huduma hyo kwa sasa hakuna,naomba nipate jibu kamili kutoka kwako nifanyeje ili niwekwe kwenye tariff ndogo
 
Asante kwa maelezo mazuri TANESCO.

Umesema sababu mojawapo ya umeme kupotea ni earth lod kutokuwa shaba halisi.

Naomba kujua sababu zingine zinazoweza kuleta leakage ya umeme kwenye nyumba.

Lakini pia, taarifa za mtaani zinasema ni vizuri kuweka chumvi na mkaa pale kwenye earth lod. Je hii inasaidia umeme kutokupotea?
 
1. Je! ni kweli kuwa umeme unatofautiana bei ya unit kutokana na aina ya mita uliofungiwa?

2. Je ! kwa mita hizi mpya nimefunga umeme 3 phace low voltage kwa bahati mbaya umeme ukaisha wote, ninapoweka mwingine nitumie namba ngapi maana inasumbua.
 
ni taratibu gani nifuate ili kuunganishiwa umeme kwa mteja mpya? na gharama ya kuunga umeme kwa eneo linalohitaji nguzo 3 ni kiasi gani kwa kijijini
 
Wateja wetu wote katika Jukwaa hili mita zinazofungwa kwa wateja kwa sasa zote ni zile zinazofungwa kwenye nguzo Wassion na aina nyingine ni EDMI ndizo zinazo patikana katika ofisi zote za TANESCO .

Mita hizo zote zinatumia remote au kiwasilianishi kama wengine wanavoita na remote hizo zipo za aina mbili kuna zile zinazo hitaji kuchomekwa ukutani kwenye socket switch ndio uingize umeme na kuna zile ambazo si lazima chomeke ukutani kwenye swichi ndio uweke umeme,aina hii ya pili hutumia antena kuwasiliana na mita remote hizo zote zina ubora sawa.

KUHUSU Tarrif mgawanyo wa makundi ya matumizi ya umeme unafanyika kutokana na kiwango cha matumizi ya mteja mfano kuna mtu kauliza kuwa kwanini mtu mmoja anauziwa unit moja sh 100 na mwingine ni zaidi ya hapo , jawabu ni kuwa makundi ya matumizi yapo kama ifuatavyo

Kundi la kwanza ni wale wateja wanao tumia unit ambazo hazivuki units 75 kwa mwezi, wateja hawa mara nyingi ni wale wenye matumizi madogo kabisa wengi wao hawa a vifaa vingi vya umeme mostly wako vijijini .wateja hawa hulipia unit moja shs 100 kama atatimiza kigezo cha kuto vuka units 75 kwa mwezi . na ikiwa atavuka units 75 kila unit inayo zidi baada ya zile 75 za mwanzo atachajiwa tshs 350 , na ikiwa mteja huyo atavuka units 75 kwa miezi mitatu mfulululizo mteja huyo atahamishwa daraja na kwa mashatri hayo mteja huyo hataweA kurudi daraja hili dogo tena.

Kundi lapili ni lile la wateja wanao tumia units zaidi ambao huanzia units 0 283.4 hadi hawa ndio wale wanao itwa Tarrif 1 hawa bei ya units ni shs 292 nahapa atatumia mita ya single phase yenye volts 220 -250 au ataweza kutumia ile ya three phase ile yenye volts 400 ikiwa atakuwa anamatumizi yanayo fikia units 7500 katika kundi hili bei inafanana kwa units hizo zote .

na kundi la tatu ni lile la wateja wa matumizi ya kati ambao hutumia units zaidi ya hizo 7500 na bei ya units moja ni shs 195 kwa unit moja na kundi la nne ni kundi la wateja wakubwa ambao unit moja wanauziwa shs 157 hawa hutumia umeme mkubwa sana mfano wale wanao jengewa line kabisa ya 33 Kv etc wateja hawa pamona na kundi lile la wateja wa kati wote huchajiwa kitu kina itwa KVA charges ambayo ni constant like kwa wale wa T2 tarrif 2 ni tshs 15004 na T3 ni 13200 nii ni ile gharama ya kiwango cha juu cha mahitaji tunaita maximum demand charges
 
Back
Top Bottom