Fahamu mita za LUKU zinazofungwa majumbani

Hamnaa matumizi makubwa maana tulibadilishiwa luku tukapewa mpya...matumizi ni yale yalee ilaa sasa unit zinaenda sanaa..
 
Ulishazoea kuserereka na kuti, zile mita za zamani analogy zilikuwa sometimes hazizunguki kwajili ya kutu saivi umewekewa kitu digital unajiskia kufa? Na bado.
 
Duhhh,,inaonekana we kula kulala hujui maisha ni nini,,,,,
 
Wateja wetu wengi wamekuwa wakijiuliza iwapo wamefungiwa mita sahihi kutokana na matumizi yao ya umeme? Ama mita ambazo wamefungiwa ni za Viwandani na kulalamika wanatumia umeme mwingi zaidi tofauti na matumizi wanayotumia

Mita za LUKU zinazofungwa majumbani ni sahihi kwa matumizi ya nyumbani, ufungaji wa mita za majumbani hutegemea sana upimwaji wa matumizi /mahitaji ya umeme katika nyumba husika.

Mteja anafanyiwa tadhimini kabla ya kuunganishiwa umeme, wakati wa uunganishaji wa umeme inaangaliwa maombi kama Mteja ameomba kufungiwa njia moja (single phase) ama njia tatu (three phase) na haiwezekani Mteja aombe njia moja ya umeme afungiwe njia tatu.

Iwapo matumizi ya umeme ya Mteja yakiongezeka kufika unit 7500 hapo atalazimika kutumia mita za njia tatu (three phase) zenye uwezo wa Volts 400 kutoka mita ya njia moja yenye Volts 220 -250.

Wateja wengi hawafahamu hasa anapo tumia umeme ukafikia units 300 anadhani TANESCO ilikosea kumfungia umeme/mita. Sio kweli, kinachotakiwa ni Mteja kuwa na matumizi mazuri ya umeme ili kupunguza gharama.

Aidha, mita za LUKU za njia tatu kwa baadhi ya Wateja wenye mahitaji makubwa ya umeme wamefungiwa majumbani mwao hasa ambao tangu tathmini inafanyika ilionekana mahitaji ya umeme yatafika units 7500 maeneo mengine ni ya Kibiashara na ambako matumizi ya umeme wa njia moja hautofaa huwa wanafungiwa huo wa njia tatu.

Kwa wastani wa units 10 usiku na 6 mchana maana yake Mteja ana zaidi ya units 300 kwa mwezi yaani 16x30 utapata units mia nne (400) hayo si matumizi madogo, pia yapo mambo mengi ya kuyaangalia linapokuja suala la matumizi ya umeme, cha kwanza hiyo mita iko sahihi? TANESCO huwa inapima mita kulingana na maombi ya Mteja, ikiwa itagundulika kuwa mita ni mbovu Mita hiyo huondolewa eneo la Mteja, na Mteja atasahihishiwa account zake kulingana na kile kipindi mita haikusoma ipasavyo,

Jambo la pili ni Mteja anatakiwa kukagua mfumo wa umeme wa nyumba yake na kuhakikisha hakuna hitilafu (leakage) yoyote inayo pelekea umeme kuvuja na kumuongezea matumizi Mteja (Wiring system) na pia Mteja kuhakikisha earth load iwe shaba halisi.

Tatu ni vifaa anavyo tumia Mteja vina uwezo gani wa kutumia umeme? Nirahisi ku hesabu umeme tunaotumia na kutoa malalamiko kwa TANESCO, na Shirika litafanya ukaguzi ili kubaini matumizi hayo pengine ni sahihi, kila kifaa kina kiasi cha umeme kinachotumia kwa dakika ama masaa kadhaa. Inashauriwa Mteja kutumia vifaa vinavyotumia umeme mdogo (Energy Server), pia inashauriwa kuepuka vifaa vya mitumba sababu vingi vinatumia umeme mwingi.
Shukrani Tanesco,Ninaswali moja,Kuna uwezekano wa kupata print out ya mihamala inayofanywa kulipia umeme kwenye luku meter husika?. Mfano ukitaka kupata statement ya units zilizoingizwa katika luku fulani kila baada ya muda fulani.
 
Unaweza kupata mkuu
 
Wateja wetu wote katika Jukwaa hili mita zinazofungwa kwa wateja kwa sasa zote ni zile zinazofungwa kwenye nguzo Wassion na aina nyingine ni EDMI ndizo zinazo patikana katika ofisi zote za TANESCO .

Mita hizo zote zinatumia remote au kiwasilianishi kama wengine wanavoita na remote hizo zipo za aina mbili kuna zile zinazo hitaji kuchomekwa ukutani kwenye socket switch ndio uingize umeme na kuna zile ambazo si lazima chomeke ukutani kwenye swichi ndio uweke umeme,aina hii ya pili hutumia antena kuwasiliana na mita remote hizo zote zina ubora sawa.

KUHUSU Tarrif mgawanyo wa makundi ya matumizi ya umeme unafanyika kutokana na kiwango cha matumizi ya mteja mfano kuna mtu kauliza kuwa kwanini mtu mmoja anauziwa unit moja sh 100 na mwingine ni zaidi ya hapo , jawabu ni kuwa makundi ya matumizi yapo kama ifuatavyo

Kundi la kwanza ni wale wateja wanao tumia unit ambazo hazivuki units 75 kwa mwezi, wateja hawa mara nyingi ni wale wenye matumizi madogo kabisa wengi wao hawa a vifaa vingi vya umeme mostly wako vijijini .wateja hawa hulipia unit moja shs 100 kama atatimiza kigezo cha kuto vuka units 75 kwa mwezi . na ikiwa atavuka units 75 kila unit inayo zidi baada ya zile 75 za mwanzo atachajiwa tshs 350 , na ikiwa mteja huyo atavuka units 75 kwa miezi mitatu mfulululizo mteja huyo atahamishwa daraja na kwa mashatri hayo mteja huyo hataweA kurudi daraja hili dogo tena.

Kundi lapili ni lile la wateja wanao tumia units zaidi ambao huanzia units 0 283.4 hadi hawa ndio wale wanao itwa Tarrif 1 hawa bei ya units ni shs 292 nahapa atatumia mita ya single phase yenye volts 220 -250 au ataweza kutumia ile ya three phase ile yenye volts 400 ikiwa atakuwa anamatumizi yanayo fikia units 7500 katika kundi hili bei inafanana kwa units hizo zote .

na kundi la tatu ni lile la wateja wa matumizi ya kati ambao hutumia units zaidi ya hizo 7500 na bei ya units moja ni shs 195 kwa unit moja na kundi la nne ni kundi la wateja wakubwa ambao unit moja wanauziwa shs 157 hawa hutumia umeme mkubwa sana mfano wale wanao jengewa line kabisa ya 33 Kv etc wateja hawa pamona na kundi lile la wateja wa kati wote huchajiwa kitu kina itwa KVA charges ambayo ni constant like kwa wale wa T2 tarrif 2 ni tshs 15004 na T3 ni 13200 nii ni ile gharama ya kiwango cha juu cha mahitaji tunaita maximum demand charges
Mie mbona Huwa kwa mwezi hazizidi Unit 45 lakini mbona nanunua kwa Bei kubwa
 
kuna kifaa nasikia mnacho kwa mtu ambaye hajafanya wiring anaweza ingiziwa umeme?je ni kweli!
 
Maswali mebgi yameulizwa hayajajibiwa, kwa hiyo mmekuja kutuchora tuuu? Nikinunua luku naweza kuhama NAyo? Km haoana mini kinakwamisha?
 
Wateja wetu wote katika Jukwaa hili mita zinazofungwa kwa wateja kwa sasa zote ni zile zinazofungwa kwenye nguzo Wassion na aina nyingine ni EDMI ndizo zinazo patikana katika ofisi zote za TANESCO .

Mita hizo zote zinatumia remote au kiwasilianishi kama wengine wanavoita na remote hizo zipo za aina mbili kuna zile zinazo hitaji kuchomekwa ukutani kwenye socket switch ndio uingize umeme na kuna zile ambazo si lazima chomeke ukutani kwenye swichi ndio uweke umeme,aina hii ya pili hutumia antena kuwasiliana na mita remote hizo zote zina ubora sawa.

KUHUSU Tarrif mgawanyo wa makundi ya matumizi ya umeme unafanyika kutokana na kiwango cha matumizi ya mteja mfano kuna mtu kauliza kuwa kwanini mtu mmoja anauziwa unit moja sh 100 na mwingine ni zaidi ya hapo , jawabu ni kuwa makundi ya matumizi yapo kama ifuatavyo

Kundi la kwanza ni wale wateja wanao tumia unit ambazo hazivuki units 75 kwa mwezi, wateja hawa mara nyingi ni wale wenye matumizi madogo kabisa wengi wao hawa a vifaa vingi vya umeme mostly wako vijijini .wateja hawa hulipia unit moja shs 100 kama atatimiza kigezo cha kuto vuka units 75 kwa mwezi . na ikiwa atavuka units 75 kila unit inayo zidi baada ya zile 75 za mwanzo atachajiwa tshs 350 , na ikiwa mteja huyo atavuka units 75 kwa miezi mitatu mfulululizo mteja huyo atahamishwa daraja na kwa mashatri hayo mteja huyo hataweA kurudi daraja hili dogo tena.

Kundi lapili ni lile la wateja wanao tumia units zaidi ambao huanzia units 0 283.4 hadi hawa ndio wale wanao itwa Tarrif 1 hawa bei ya units ni shs 292 nahapa atatumia mita ya single phase yenye volts 220 -250 au ataweza kutumia ile ya three phase ile yenye volts 400 ikiwa atakuwa anamatumizi yanayo fikia units 7500 katika kundi hili bei inafanana kwa units hizo zote .

na kundi la tatu ni lile la wateja wa matumizi ya kati ambao hutumia units zaidi ya hizo 7500 na bei ya units moja ni shs 195 kwa unit moja na kundi la nne ni kundi la wateja wakubwa ambao unit moja wanauziwa shs 157 hawa hutumia umeme mkubwa sana mfano wale wanao jengewa line kabisa ya 33 Kv etc wateja hawa pamona na kundi lile la wateja wa kati wote huchajiwa kitu kina itwa KVA charges ambayo ni constant like kwa wale wa T2 tarrif 2 ni tshs 15004 na T3 ni 13200 nii ni ile gharama ya kiwango cha juu cha mahitaji tunaita maximum demand charges
Shukran
 
Jaman mm nmefungiwa luku mwaka Jana December nikawekews na umeme wa 30000 mpk sasa haujaisha kuna tatzo hapo?
 
Ghrama ya kuvuta umeme ni sh 27000 tu. Je gharama ya nguzo na transforma ni bei gani kuke kijijini?
 
Jaman mm nmefungiwa luku mwaka Jana December nikawekews na umeme wa 30000 mpk sasa haujaisha kuna tatzo hapo?
Kama ni umeme wa REA hapo hamna tatizo maana elfu 5 ubafumia mwezi mzima!
 
Nipo kongowe pale mpkani mwa pwani na dar ila pale ni pwani je na pale pana umeme wa area?
 
hivi kutenganishiwa mita kwenye nyumba moja mathalani ya wapangaji kila mtu akawa na mita yake kwanini imekuwa ni gaharama kubwa kama vile ndo unavuta umeme kwako?mnaonaje muwe na offer ili kupunguza kelele na misuguano isiye ya lazima baina ya wapangaji
 
Unaweza kupata mkuu
Tuna office zetu zipo mbez beach mkabala na mbezi high school..
Toka mwaka jana. Wezi wa 11 tumeripotia nguzo imekatika kabisa bado kuanguka tu imeshikiliwa na kitu kidogo sana
Tanesco mbezi wanakuja wanaangalia kisha wanasema watarudi lakini hawarudi
Hii nguzo ipo ndani ya eneo la nyumba na ni office yenye wafanyakazi wengi..
Je mnataka siku iangukie na kuua au kujeruhi wafanyakazi ndio mje kurekebisha..
5dbf5698690c2160e8eda279e01c7957.jpg

Kesho nitaleta picha za hiyo nguzo muone jinsi ilivyo je? Tanesco mbezi beach wameshindwa kuhudumia wananchi...
Tunaomba msaada wa haraka kabla madhara zaidi hayajatokea
Nawasilisha
 
Asante kwa kutupa fursa hii. Naomba kuuliza. Kwa watu wa Kongowe Kibaha. Kuwekewa umeme wa majumbani unaohitaji nguzo mbili ni shilingi ngapi ? Jee ? Baada ya surveyor ku survey inachukua muda gani mpaka mteja anapewa invoice ya kulipia ? Hapa nilipo nimefanyiwa survey over two weeks. Na je baada ya kulipia gharama za nguzo. Inachukua muda gani mpaka kuwekewa umeme ? Nadhani hakuna ofisi ya ovyo ya Tanesco kama hii ya Kibaha.
 
Tumeipokea kwa hatua zaidi mkuu
 
Chukua fomu tukupimie ndio tukuoe makaridio kwa kuwa kila umbali zaidi ya mita 30 una bei yake, survey inafanyika ndani ya siku 7, 10 au 14 za kazi kwa mujibu wa mkataba wa huduma kwa wateja
 
Back
Top Bottom