Fahamu mita za LUKU zinazofungwa majumbani

Fahamu mita za LUKU zinazofungwa majumbani

Asante kwa maelezo mazuri TANESCO.

Umesema sababu mojawapo ya umeme kupotea ni earth lod kutokuwa shaba halisi.

Naomba kujua sababu zingine zinazoweza kuleta leakage ya umeme kwenye nyumba.

Lakini pia, taarifa za mtaani zinasema ni vizuri kuweka chumvi na mkaa pale kwenye earth lod. Je hii inasaidia umeme kutokupotea?
...Ni Earth rod
 
Ushauri kama huu unampa mtu wa huduma kwa wateja, yeye mwenyewe anaface matatizo unayo experience ww
Kama upo serious its better ukaenda makao makuu uonane na mkurugenzi mkuu
...Huyo mtu wa huduma kwa wateja kajileta haha jukwaani mwenyewe bila consent ya bosi wake? Je una uhakika gani kwamba hapeleki feedback kwa mkuu wake kuhusu key issues ambazo ameulizwa na members hapa? Ikiwa mawaziri na possibly rais wanapitia humu ndo itashindikana kwa hao wakuu wa Tanesco? Juzi nimeona Azam Tv kwenye maoni from mitandaoni wameweka JF.
 
Wateja wetu wengi wamekuwa wakijiuliza iwapo wamefungiwa mita sahihi kutokana na matumizi yao ya umeme? Ama mita ambazo wamefungiwa ni za Viwandani na kulalamika wanatumia umeme mwingi zaidi tofauti na matumizi wanayotumia

Mita za LUKU zinazofungwa majumbani ni sahihi kwa matumizi ya nyumbani, ufungaji wa mita za majumbani hutegemea sana upimwaji wa matumizi /mahitaji ya umeme katika nyumba husika.

Mteja anafanyiwa tadhimini kabla ya kuunganishiwa umeme, wakati wa uunganishaji wa umeme inaangaliwa maombi kama Mteja ameomba kufungiwa njia moja (single phase) ama njia tatu (three phase) na haiwezekani Mteja aombe njia moja ya umeme afungiwe njia tatu.

Iwapo matumizi ya umeme ya Mteja yakiongezeka kufika unit 7500 hapo atalazimika kutumia mita za njia tatu (three phase) zenye uwezo wa Volts 400 kutoka mita ya njia moja yenye Volts 220 -250.

Wateja wengi hawafahamu hasa anapo tumia umeme ukafikia units 300 anadhani TANESCO ilikosea kumfungia umeme/mita. Sio kweli, kinachotakiwa ni Mteja kuwa na matumizi mazuri ya umeme ili kupunguza gharama.

Aidha, mita za LUKU za njia tatu kwa baadhi ya Wateja wenye mahitaji makubwa ya umeme wamefungiwa majumbani mwao hasa ambao tangu tathmini inafanyika ilionekana mahitaji ya umeme yatafika units 7500 maeneo mengine ni ya Kibiashara na ambako matumizi ya umeme wa njia moja hautofaa huwa wanafungiwa huo wa njia tatu.

Kwa wastani wa units 10 usiku na 6 mchana maana yake Mteja ana zaidi ya units 300 kwa mwezi yaani 16x30 utapata units mia nne (400) hayo si matumizi madogo, pia yapo mambo mengi ya kuyaangalia linapokuja suala la matumizi ya umeme, cha kwanza hiyo mita iko sahihi? TANESCO huwa inapima mita kulingana na maombi ya Mteja, ikiwa itagundulika kuwa mita ni mbovu Mita hiyo huondolewa eneo la Mteja, na Mteja atasahihishiwa account zake kulingana na kile kipindi mita haikusoma ipasavyo,

Jambo la pili ni Mteja anatakiwa kukagua mfumo wa umeme wa nyumba yake na kuhakikisha hakuna hitilafu (leakage) yoyote inayo pelekea umeme kuvuja na kumuongezea matumizi Mteja (Wiring system) na pia Mteja kuhakikisha earth load iwe shaba halisi.

Tatu ni vifaa anavyo tumia Mteja vina uwezo gani wa kutumia umeme? Nirahisi ku hesabu umeme tunaotumia na kutoa malalamiko kwa TANESCO, na Shirika litafanya ukaguzi ili kubaini matumizi hayo pengine ni sahihi, kila kifaa kina kiasi cha umeme kinachotumia kwa dakika ama masaa kadhaa. Inashauriwa Mteja kutumia vifaa vinavyotumia umeme mdogo (Energy Server), pia inashauriwa kuepuka vifaa vya mitumba sababu vingi vinatumia umeme mwingi.
Halafu kuna wajinga wanataka kuifungia jf wakati mashirika makubwa makubwa ya serikali yapo humu humu,elimu kama hii huwezi kuikuta fb wala instagram wala twita, it's only at jmaii forum,long live JF...thank u Tanesco...
 
... Inashauriwa Mteja kutumia vifaa vinavyotumia umeme mdogo (Energy Server), pia inashauriwa kuepuka vifaa vya mitumba sababu vingi vinatumia umeme mwingi.

Hizo energy server ndiyo zikoje mkuu?
..ukienda maduka ya vifaa vya ujenzi na umeme, ukawaambia wakupe bulb zinazotumia umeme kidogo unapata.
 
Hivi kwa nyumba ya kupangisha ambapo una wapangaji wengi ili kuondokana na tatizo la kupunjana wapangaji kwenye kulipa bili ya umeme Tanesco nasikia mna kifaa ambacho kila mpangaji anaweza kukifunga chumbani kwake ili kujua kiasi cha umeme alichotumia?
 
...wapi huko zinapatikana bure? Hizo during wiring unanunua kwenye harwares.
Ni hardwares sio harwares. Ila nashukuru kwa masahihisho ya earth rod.

Muhimu ilikuwa ni mantiki ya neno. Smart phones zina kadhia zake.
 
Waweza kumshukuru bila ku quote Uzi wote, mnatusumbua kweli sisi wengine.
Nakuelewa. Ila Wakati mwingine, swali ulilo omba, linakuwa limejibiwa vizuri mno na inakubidi kuapreciate kwa kuqoute majibu yote.

Lakini upo sawa kabisa.
 
Hivi kwa nyumba ya kupangisha ambapo una wapangaji wengi ili kuondokana na tatizo la kupunjana wapangaji kwenye kulipa bili ya umeme Tanesco nasikia mna kifaa ambacho kila mpangaji anaweza kukifunga chumbani kwake ili kujua kiasi cha umeme alichotumia?
Yes izo mita zipo. Ila sio jukumu la tanesco kuzifunga. Zinapatikana maduka ya vifaa vya umeme. Bei yaweza fikia sh. Elfu 80 kwa mita moja.
 
Hongera sana Tanesco,sasa mnatufikia na kutuelewesha,nadhani wewe unayeandaa haya mambo itakuwa kijana mwenye nguvu,tuombe Mungu wasiku-frustrate
 
mkuu swali..
nmefungiwa umeme jumanne, mita imefungwa kwenye nguzo..
tatizo usiku inatokea umeme unakatika na kurud kwa jiran zangu unakuwepo ila kwangu inakuwa kama mchezo
hasa mida ya kuanzia saa mbil usiku mpaka saa nne mchana haitokei..
shida ni nin
Tatizo kama langu
 
Inaelekea huna idea zozote za maswala ya uchumi mzee
Najua sana maswala ya uchumi kwa kuwa nimeyasoma ,shida yenu ni kuwa unakuja na tu na jibu la kupinga au kukubali kitu bila kutoa ideas ulizonazo,kuandika tu kuwa sina idea zozote za maswala ya uchumi ni kuonyesha uwezo wako wa kufikiri ulivyo,nadhani ungetoa mawazo yako ningekuelewa,kuliko kusema tu sina idea na maswala ya uchumi,ok kwa hiyo kama sina nisitoe maoni?na wewe mwenye idea maoni yako ni yapi?
 
kwanza nianze kwa kuwapongeza Tanesco kwa Huduma nzuri. mwaka Jana huku kwetu mlifanya mabadiriko ya Mita kwa sisi watu wa mita za kawaida tukawekewa mita za Luku. sasa Tatizo ni kwamba karibu wateja wote tumewekwa katika kundi la viwanda yaan Tariff 1 na wengi wetu hapa tuna matumizi ya kawaida yale ya Tariff 4 au Tariff 0. Hii inaweza kua imekaa aje Tanesco??
 
Ubaya wake ni upi Hazchem plate ?

Waliounganishiwa umeme hivi karibuni zimewekwa hizi mita za kwenye nguzo (nadhani hizo ndio mita mpya unazozungumzia hapa).
Mita za zamani unaweza kusoma salio la unit kwa urahisi ,lakini za sasa lazima uweke betri au ucharge ndio ujue salio,za zamani zinatoa mlio kuashiria kwamba salio linakaribia kuisha ,hizi inabidi kuangalia mara kwa mara kama umeme upo au la,pia hizi mpya kuweka salio inabidi kimashine kiwe na charge ya umeme au betri ndio uweke salio wakati za zamani ni kuweka tu salio.kifupi za zamani ni nzuri kuliko hizi za ''kutundika kwenye nguzo''
 
Kumbe sie tupo nchi nyingine. Huku Namanga tunalipa unit moja sh 357.14 sawa na 5000 kwa unit 14. Hapo mtu ni mtumiaji wa kawaida. Ila kuna watu nasikia wanaweka hela kidogo ila inakaa hadi wanasahau. Naona hao ndio mmeunga na watanzania wenzenu. Lingine Tanesco huku ni tabu tupu ukitaka ufungiwe umeme hadi ufunge na kuomba labda uwe na hela ya kuonga. Ila unajua tena sie watu wa pande hii hatuna shida bora tuonge tupate huduma ila saa zingine ni full magumashi. Wacha sasa liluku lenu liharibike au liwe na tatizo huku kwetu oohoo mtu utalia maana hawaji ngo. Tanesco leo nawashangaa huku Forum kumbe mnakuaga waungwana hivi hahaha ha. Yote heri ila fanyeni hata mkutano mmoja huku pamoja na wananchi wa huku huenda wakeeleza wanayowasibu
 
Yes izo mita zipo. Ila sio jukumu la tanesco kuzifunga. Zinapatikana maduka ya vifaa vya umeme. Bei yaweza fikia sh. Elfu 80 kwa mita moja.

Mkuu kwa hyo baada ya mita ya nyumba zima kufungwa, then kila chumba kinaweza fungiwa hiyo mita yake. Na katika kuweka anaweka unit zake pekee au inambidi aje kuweka kwenye mita ya pamoja? Elimu zaidi katika hili inahitajika.
 
Mkuu kwa hyo baada ya mita ya nyumba zima kufungwa, then kila chumba kinaweza fungiwa hiyo mita yake. Na katika kuweka anaweka unit zake pekee au inambidi aje kuweka kwenye mita ya pamoja? Elimu zaidi katika hili inahitajika.
Umeme unanunuliwa kwenye mita kuu ya tanesco. Mita ndogo zinawezesha kujua nani katumia units kiasi gani ambazo zinagharimu kiasi gani. So hii itasaidia mtu kuchanga kiasi cha pesa ambacho muhuusika ametumia umeme

Hope nimeeleweka
 
Back
Top Bottom