slimhamimu
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 325
- 111
Wateja wetu wote katika Jukwaa hili mita zinazofungwa kwa wateja kwa sasa zote ni zile zinazofungwa kwenye nguzo Wassion na aina nyingine ni EDMI ndizo zinazo patikana katika ofisi zote za TANESCO .
Mita hizo zote zinatumia remote au kiwasilianishi kama wengine wanavoita na remote hizo zipo za aina mbili kuna zile zinazo hitaji kuchomekwa ukutani kwenye socket switch ndio uingize umeme na kuna zile ambazo si lazima chomeke ukutani kwenye swichi ndio uweke umeme,aina hii ya pili hutumia antena kuwasiliana na mita remote hizo zote zina ubora sawa.
KUHUSU Tarrif mgawanyo wa makundi ya matumizi ya umeme unafanyika kutokana na kiwango cha matumizi ya mteja mfano kuna mtu kauliza kuwa kwanini mtu mmoja anauziwa unit moja sh 100 na mwingine ni zaidi ya hapo , jawabu ni kuwa makundi ya matumizi yapo kama ifuatavyo
Kundi la kwanza ni wale wateja wanao tumia unit ambazo hazivuki units 75 kwa mwezi, wateja hawa mara nyingi ni wale wenye matumizi madogo kabisa wengi wao hawa a vifaa vingi vya umeme mostly wako vijijini .wateja hawa hulipia unit moja shs 100 kama atatimiza kigezo cha kuto vuka units 75 kwa mwezi . na ikiwa atavuka units 75 kila unit inayo zidi baada ya zile 75 za mwanzo atachajiwa tshs 350 , na ikiwa mteja huyo atavuka units 75 kwa miezi mitatu mfulululizo mteja huyo atahamishwa daraja na kwa mashatri hayo mteja huyo hataweA kurudi daraja hili dogo tena.
Kundi lapili ni lile la wateja wanao tumia units zaidi ambao huanzia units 0 283.4 hadi hawa ndio wale wanao itwa Tarrif 1 hawa bei ya units ni shs 292 nahapa atatumia mita ya single phase yenye volts 220 -250 au ataweza kutumia ile ya three phase ile yenye volts 400 ikiwa atakuwa anamatumizi yanayo fikia units 7500 katika kundi hili bei inafanana kwa units hizo zote .
na kundi la tatu ni lile la wateja wa matumizi ya kati ambao hutumia units zaidi ya hizo 7500 na bei ya units moja ni shs 195 kwa unit moja na kundi la nne ni kundi la wateja wakubwa ambao unit moja wanauziwa shs 157 hawa hutumia umeme mkubwa sana mfano wale wanao jengewa line kabisa ya 33 Kv etc wateja hawa pamona na kundi lile la wateja wa kati wote huchajiwa kitu kina itwa KVA charges ambayo ni constant like kwa wale wa T2 tarrif 2 ni tshs 15004 na T3 ni 13200 nii ni ile gharama ya kiwango cha juu cha mahitaji tunaita maximum demand charges
Shukrani sana kwa kutupatia ufahamu huu.