Khantwe
JF-Expert Member
- Dec 20, 2012
- 61,150
- 124,755
mi natafuta limbwata mwenye ujuzi anipm
Njoo piemu kwangu
mi natafuta limbwata mwenye ujuzi anipm
Sijui kama hilo neno "limbwata" linafaa ila kuna kitu kama hicho kinatumiwa na watu (sana ni wanawake)
Habari zenu Great thinkers....
Najua wapo watu ambao hawaamini kwamba katika mapenzi kuna kitu kinaitwa limbwata. Hata mimi nilikuwa siamini kabisa kuhusu hili suala lakini hivi karibuni nimeamini.
Nlikuwa naishi kwenye mkoa mmoja hivi miaka kama miwili au mitatu iliyopita..... Katika kijiji kile alikuwepo baba mmoja mwenye mke na watoto wanne. Huyu baba alikuwa mtu wa heshima na pesa zake za kumtosha kubadilisha mboga....kifupi ni kwamba hakuwa na dhiki.
Mke wake sasa.....alikuwa ni kicheche balaa....alikuwa anagawa utadhani sio mke wa mtu. Ilifika hatua akawa anatoka na kijana mmoja jirani tu na nyumbani kwake na huyo kijana alikuwa na mkewe kabisa. Bas ilikuwa yule kijana akimfuma yule mwanamke na mwanaume (hawara mwingine) anamshushia kipigo hadharani....siku nyingine kamdunda weee akamburuza hadi nyumbani kwake akafika getini kamsukumizia ndani....na mumewe yupo ndani!
Nilikuwa napata shida najiuliza hivi huyu baba ni mzima kweli? Maana katika kipindi chote sikuwahi kusikia ana mgogoro na huyo mkewe mzinzi.... Siwezi kusema hana akili timamu maana majukumu yake ya kiofisi alikuwa anayatekeleza vizuri kabisaa..
Eti wana MMU nisaidieni kama hili sio limbwata basi ni kitu gani? Siwezi kukubali kwamba eti ilikuwa ni ndoa ya kawaida hii....
Wewe mwenzangu huko mtaani kwako umewahi kukutana na matukio kama haya?
lipo tena wanaume wa siku hz wanafanyiwa sana kwa sababu hawaeleweki
jamani msibishe utakuta mme yupo kimyaaa zingine hadi zinawafanya wawe machizi
Khantwe mambo hayo yapo na watu wameyapa majina kutokana na kazi zao, kama libwata, wengine chuma ulete, n.k
Chuma ulete kwenye mapenzi???? Sema yamepewa majina kulingana na sekta yanazotumikia. Kwenye sekta ya mapenzi ni limbwata....hiyo chuma ulete ni sekta ya uchumi lol
huyuo jamaa ni professional kwenye mambo haya.
Limbwata ni imani tu. Hakuna kitu kama hiko.
mi natafuta limbwata mwenye ujuzi anipm
Ina maana huyo baba alikuwa poyoyo kiasi cha kushindwa kujitetea kweli?
Limbwata ni imani tu. Hakuna kitu kama hiko.