Fahamu kuhusu msukule

Kesi nzito na kubwa kuliko zote kabisa Watumishi na Waumini wa Mungu wakiwa bado wako hapa duniani, ni ile ya kumsulubisha Yesu msalabani kwa mara ya pili; haina msamaha! Yeyote yule ambaye huwa anatamani kumuua Mtumishi au Muumini wa Mungu, dhambi yake ndiyo hii, kwa sababu the same person anatamani kumuua Yesu. Ni kesi mbaya kuliko kesi zote kwenye ulimwengu wa roho, mtu anaweza kupata akiwa bado anaishi hapa duniani!
 
Acha upopoma, wakati huku kwetu watoto wa wanaoshinda kanisani ndo wanabebwa kichawi KIRAHISI sana!!!


Kizibo
Hio yote kuto kuijua kweli na kutofahamu fumbo za shetani kushinda kanisani sio kufanya vita na nguvu za kichawi cha muhimu ni kushindana na kupambana na shetani na wapenda kazi wake
 
Uchawi ni sanaaa pana sana. Kuna namna nyingi ya utekelzaji matokeo yanayo takiwa.
Ni kama mahesabu pia yaani 6+3=9, 7+2=9, 1+8=9, 4+5=9...

So uchukuliwaji wa msukule, ukiwa pro. Unanjia nyingi ya kufanikisha hilo, na hiyo ya juu ni moja wapo.

Sent using Jamii Forums mobile app

kwa anaetambua umeandika sentensi yenye maana mno.
 
Huo msukule ukiwa huko usukuleni itafika siku atakufa kikweli kweli au hafi mara mbili?
zikifika siku alizopangiwa na mungu anakufa, lakin mara nyng ni wagumu sana kufa sababu wako chini ya watengeneza magonjwa so no chance watawathuru watu wao

pia mtu kukufanya msukule ni process sio kazi ndogo, mpaka ajue tarehe yako ya kuzaliwa, jina la ukoo nk ili aiombe mizimu/malaika akizuiwa analazimika kushindana nayo ikiwa legelege unaenda na maji kweli
 
Fafanua vizur mkuu
zikifika siku alizopangiwa na mungu anakufa, lakin mara nyng ni wagumu sana kufa sababu wako chini ya watengeneza magonjwa so no chance watawathuru watu wao

pia mtu kukufanya msukule ni process sio kazi ndogo, mpaka ajue tarehe yako ya kuzaliwa, jina la ukoo nk ili aiombe mizimu/malaika akizuiwa analazimika kushindana nayo ikiwa legelege unaenda na maji kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha upopoma, wakati huku kwetu watoto wa wanaoshinda kanisani ndo wanabebwa kichawi KIRAHISI sana!!!


Kizibo
Hawana ulinzi.wenye ulinzi hutaweza kuwachukua Wala kuwaloga.Kushinda kanisani siyo kigezo kuwa una yesu au mungu ndani yako.
 
Ujue ukweli huu wewe uliye ndani ya Yesu, ili usiendelee kuhangaika na vitu ambavyo wala hutakiwi hata kuviwaza katika maisha yako kwa sababu havitakiwi kuwepo kabisa kwenye ratiba ya mambo yako ya kila siku: Jua kwa uhakika kabisa kuwa Bwana au Yesu:
1. Anajua yote;
2. Anaweza yote;
3. Yuko kila mahali;
4. Alimnyang'anya Shetani Funguo na Mamlaka ya Mauti na Kuzimu;
5. Uhai wako umefichwa ndani yake; hayupo anayeweza kuuchukua uhai wako, kwa sababu ili auchukue, inabidi auchukue uhai wa Yesu kwanza, kitu ambacho ni kama mtu kujaribu kuogelea kwenye uji wa chuma cha moto kilichoyeyuka, akidhani kuwa ni maji ya Baharini au Ziwa
6. Shetani-yeye hayuko kila mahali

Ukiwa ndani ya Yesu, jua pia mambo haya mawili makubwa ya nyongeza: Nitayasema kwa Kiingerza kwa sababu ni "quotes" kutoka kwenye kitabu nilichowahi kukisoma

1.EVERY MOVE OF THE ENEMY MUST COME BY PERMISSION, UNDER THE PROTECTIVE HEDGE OF JESUS CHRIST. Kwa hiyo ukiona kitu ambacho hakieleweki kimekuja kwako, na hauna tatizo lolole kiroho, jua kuwa Yesu yuko nyuma yake, na anataka kuongea na wewe kitu ili akupandishe kutoka ngazi moja ya chini, kwenda nyingine ya juu, INAYOFUATA (tatizo moja kwa Yesu ni kuwa huwa hakuna kurushwa ngazi!)

2.WE FIGHT NOT FOR VICTORY, BUT FROM VICTORY
Ukiwa ndani ya Yesu, hupigani ili ushinde. Vita ilishapiganwa siku nyingi Kalvari na mshindi anajulikana. Ukiona kuwa una vita, jua kabisa kuwa unapigana ukiwa ndani ya ushindi, unapigana vita ambayo mshindi anajulikana, na katika uhalisia anayepigana ni yule ambaye alishawahi kushinda vita, analazmikika kupigana tena sababu ya upumbavu wa wasiomheshimu, na anatamani safari hii ajitambulishe kwa viwango vipya kabisa ambavyo havijawahi kuonekana tangu kuumbwa kwa ulimwengu, kuwa YEYE NI NANI!
Habari
Unaweza nipa jina la hiko kitabu nikisome?
 
Ni kweli Shetani ana nguvu kiasi fulani,ila nguvu zake zinaishia mwilini tu,hana uwezo, wala mamlaka ya kuua roho.Halafu msukule anamtumikia mchawi,kazi ya jini ni kufanikisha tu matakwa ya mchawi kwa ujira.

Mwisho,Jini lililofanikisha matakwa ya mchawi,lenyewe lilishahukumiwa kwa kumuasi Mungu Mbinguni,linachosubiri ni kutekelezwa tu kwa hukumu yake.Kwa upande mwingine, Mchawi ndiye atakaye-hukumiwa kwa kitendo chake cha uchawi,labda atubie uovu wake na kumkiri Bwana Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake.Vinginevyo ataishia jehanam ya moto.Hata hivyo Mungu katika
Mathayo 10:28 anasema,

"Msiwaogope wale wauao mwili, lakini hawawezi kuiua roho. Afadhali zaidi kumwogopa yule awezaye kuuangamiza mwili pamoja na roho katika moto wa Jehanamu." Kwa hiyo wa kumuogopa ni Mungu tu,sio Mchawi wala Jini.
Nafikiri kuna mahali kuhusu imani hayajakaa sawa.inawezekanaje mtu awachukue wengine kama misukule, Halafu atubu tu kwa Mungu asamehewe je wale aliowachukua misukule haki zao ipo wapi? Kila mtu jinsi anavyotendea watu wengine nae hivyo hivyo atatendewa kwa kipimo kile kile Hakuna cha kutenda ushetani halafu utegekee huruma ya kitubio no.utavuna ulichopanda.
 
Kuna nchi fulani hivi ni ya misukule. Wananchi wake wengi hushangilie kila anachokisema SIZONJE wao. Hawana uwezo wa kuhoji wala kukataa wanachoambiwe.
Wamefanywa wanyonge na mchawi wao na wanajisikia fahari kuitwa wanyonge.

Natamani kuipata dawa ya kumzindua msukule
hahahaaaaaaaaaaaaaaaaaa! Nimecheka sana mkuu. Ila kuna ukweli mkubwa sana 🤣 🤣
 
Kuna possibility ya msukule kurudi kwenye hali yake ya kawaida? Pia je huyo msukule ikifika siku yake ya kufa baada ya mmiliki wa mskule kufa kabisa inakuaje?
 
Msukule ni mtu ambaye anahesabiwa amekufa, lakini ukweli ni kuwa mtu huyo huwa amechukuliwa na Mchawi ili amtumie katika kazi zake maalum au amtumie katika mambo yake mengine anayoyataka.

Mchawi humfanya mtu huyo awe maiti au kama kitu kinachojiendesha chenyewe kikiwa kimekufa lakini hakijaoza wala hakiozi.

Mchawi kabla ya kumchukua mtu Msukule hufanya Mkataba Maalum na Jini anayeitwa “BAKAS” ili amsaidie katika kazi hiyo, na kuna Sadaka maalum ambayo hutoa kumlipa Jini huyo kama malipo ya kazi yake. Huyu Bakas ni Jini anayetawala siku ya Jumamosi.

Baada ya kukubaliana na Jini Bakas Mchawi huchagua mtu ambaye anataka kumchukua na akishampata huenda nyumbani kwa mtu huyo kinyume nyume mpaka anafika mlango wa mbele.

Anapofika mlangoni hunyonya roho ya mtu anayemtaka kwa kupitia tundu ya ufunguo na kama tundu hiyo haipo hutoboa tundu ndogo ambayo huiziba akimaliza kazi yake.

Baada ya kuipata roho anayoitaka huitia ndani ya chupa na kuziba chupa hiyo na kuondoka. Kazi hiyo hufanyika usiku wa manane kati ya saa nane na saa tisa usiku.

Siku inayofuata yule aliyechukuliwa roho yake huanza kuugua na hufa ghafla.

Baada ya Mazishi yule Mchawi huenda kaburini akiongozana na yule Jini Bakas ambaye hujigeuza kama babu kizee mwenye ndevu nyingi nyeupe ili kuuchukua ule mwili wa Marehemu.

Wanapofika makaburini yule Jini hukaa upande wa kichwani kwa maiti na mchawi hukaa upande wa miguuni na kila mmoja wao akifanya uchawi wake lakini kazi kubwa ya kumtoa maiti ndani ya kaburi kufanya na Jini.

Jini huomba kwa bidii na kunuiza Uchawi na husema maneno ya kichawi huku akimwaga juu ya kaburi majani ya Mkakaya (Acacia)

Mchawi yeye kwa upande wake husema maneno haya yafuatayo akirudia rudia “Mortoo tombo Mivi” maana yake ni kwamba “aliye ndani ya kaburi ni wangu”

Kwa nguvu za Uchawi mwili hutoka kaburini bila ya kaburi kuchimbwa na kusimama mbele yao na yule mchawi hukabidhiwa maiti huyo.

Baada ya kukabidhiwa kitu cha kwanza ambacho hufanya ni kwenda nyumbani na kumuonesha huyo ndugu zake kuona kama atawakumbuka.

Maiti huyo asipozinduka na kuwagundua ndugu zake au kutambua nyumbani kwao basi Mchawi hujua kwamba kazi imekuwa nzuri na hupelekwa nyumbani kwa mchawi.

Wakifika nyumbani Mchawi humrudishia yule Maiti roho ambayo aliiweka ndani ya chupa na kumnywesha dawa kali ambayo itamfanya asahau kabisa maisha yake yote ya nyuma yaliyopita na baada ya hapo maiti huyo atazinduka na kuwa Msukule.

Msukule ni binaadamu anayeishi lakini hana uhuru na anatumiwa kama mtumwa huku ndugu zake au jamaa zake wakijua kwamba amekufa.

Uchawi huu wa kuchukua Msukule ulianza miaka 500 na 1500 A.D. huko nchini Congo na Haiti na kuenea sehemu nyingi za Dunia.

James
James at February 15, 2020.

Sent using Jamii Forums mobile app
r
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom