Fahamu kuhusu Kampuni za Mfukoni-Briefcase Corporations

Mtoa Mada nakuuna mkono na Mimi Binafsi tulifungu Partnership mwaka juzi ikiwa kwenye makaratas tunamshukuru Mungu Sasa Tumeingia kwnye VRN last week na Ofisi ipo MAGOMENI
Tumeajiri vijana wa 5 permanently na 3 temp-Vibarua

Kampuni inadeal na Ufungaji CCTV camera,Electrical Fence ,GPS Tracking, n.k (insta @cimax_tech_solutions au www.climaxtechsolutions.co.tz)

Nilivyoingia kwenye VAT for the first time nikajipiga kifua nikaajiita "Managing Director " nikamalizia kwa kicheko Kikubwa Sana

Jamani kila kitu is possible nakaribisha wawekezaji Sasa tuinvest kwenye GPS tracker na tracking nna proposal Idea kubwa Sana na nzuri changamoto no CAPITAL TU
Tafuta namna ulobby in mikopo ya halmashauri pale kinondoni.
 
Habari za wakati huu;

Je unajua kuwa biashara zote kubwa zilianza kama wazo?Je unajua kwama biashara nyingi kubwa zilianza kama briefcase companies?Je unajua kuwa biashara nyingi kubwa zilianza chini?Leo nataka nizungumze kuhusu Briefcase Companies na umuhimu wa kuwa na Kabiashara kako ka Briefcase

Briefcase Company ni kampuni ambazo zina exist ama on paper only(Registered) au zina operate nyuma ya Kampuni nyingine kama Cover.Ni aina ya kampuni ambayo inaweza kuwa inaundwa na watu wa chache,haina bidhaa maalum wala huduma,haina anuani maalum ya biashara lakini ina vibali vyote vya msingi vya kuweza kufanya biashara.Briefcase Company inaweza kuwa ni Limited Company au Sole Proprietorship.Kmapuni inaweza kuanza kama Briefcase Company na baadaye ikakua na kuwa biashara kamili yenye TIJA.

Nini faida ya Briefcase Company?Faida za Briefcase Company ni nyingi sana.

Kwanza inakuwezesha kutumia fursa za kibiashara pindi zinapojitokeza bila kupata ugumu.Mfano kama wewe ni mwajiriwa na ikatokea ofisini kuna kakazi ambako kanahitajika kufanywa kwa kutumia mtu wa nje unaweza kutumia briefcase Company yako kufanya hio kazi bila kuleta mgogoro wa maslahi.

Pili iwapo hauna ajira ya kudumu unaweza kuweka Briefcase Company yako katika CV yako na ukajipa Cheo na majukumu kama yale unayotaka kufanya kulingana na uzoefu na utaalamu wako
Tatu unaweza kutumia Briefcase Company kutafuta mikataba ya kibiashara,dili za kibiashara na ukashirikiana na kampuni kubwa zenye ukwasi katika kuzitekeleza.

Katika karne hii ya ishirini na moja ni Rahisi zaidi kuanzisha Briefcase Companies ambazo kwa sasa zimekuwa zikiitwa Virtual Business/Digital Business.Hizi ni aina ya Biashara ambazo zinaendesha na kusimamiwa kwa njia ya mtandao,zinauza na kununua bidhaa na huduma kwa njia ya mtandao.Aina hii ya biashara ina maana kwama huhitaji Ofisi kwa ajili ya kuweka stock ya mzigo wala watu kuka kufanya kazi kwani kila kazi inaweza kufanywa kwa njia ya teknolojia.

Mfano Rahisi ni Jamii Forums Mmiliki wa JF anaweza weka Servers za JF Nyumbani kwake au akakodi toka kwa kampuni zinazotoa huduma hizo popote duniani.Kisha hawa moderators wakawa wanafanya kazi wakiwa sehemu tofauti kwa njia ya mtandao kulima watu ban na kufuta post za watu ili jukwaa liendelee kuwa safi na kazi ikaenda.Ukitazama utaona kwamba hii kampuni haitahitaji kuwa na phyisical office ndo maana hutasikia mod wa JF anakwambia ukiwa na malalamiko njoo ofisini tuyashughulikie mnamaliza kila kitu mtandaoni.Hii ina maana kwamba teknolojia inatumika vizuri.

Kinachosumbua watu wengi ni ama kutokuwa na ujuzi wa kutumia teknolojia au kutokujua waanzie wapi katika kuanzisha hio Kampuni ya Briefcase.Kuna namna nyingi za kuanzisha Briefcase Company na leo nitazungumzia moja ambayo ni rahisi.Fuata hatua zifuatazo ili kuanzisha Kampuni ya Briefcase.

  1. Hatua ya kwanza ni kutambua ujuzi au utaalamu wako.Hakikisha Angalau unakuwa na utaalamu fulani mfano unaweza kuwa na Genge la Nyanya,Muuza Karanga au Muuza mkaa.Sasa hakikisha kwamba unajenga mfumo wako wa biashara kwa kuzingatia hilo kwani biashara yako ndogo lazima uwe na maono makubwa nayo.Mfano Biashara ya mkaa inaweza husiana na sector ya Domestic energy au Forest Management,Biashara ya Karanga na genge la nyanya inaweza husiana na Kilimo biashara.
  2. Pili chagua Jina la Biashara ambalo litakua pamoja na Biashara yako.
  3. Kulingana na aina ya biashara unaweza kuanzisha kurasa za mitandao ya kijamii na hata tovuti ili uweze kurahisisha mawasiliano
  4. Sajili jina la biashara,tafuta leseni na Ufungue bank account kwa kutumia Jina la Biashara.
Ukishakuwa na hivyo tayari unayo Biashara yako ya Mfukoni ambayo sasa unaweza kuhangaika kuitafutia mtaji,wateja na bidhaa au huduma.

Ukishakuwa na Kampuni yako hakikisha unakuwa na Business cards na unakuwa active kuipeleka biashara yako sokoni.Kwa mfano unaweza anza kwa kuwatafuta wateja wa karibu na marafiki kisha ukaongeza na wengine.Zingatia Mfano niliotoa ni mfano mdogo.

Hata hivyo teknolojia inakuruhusu kuanzisha ecommerce shops za kuuza bidhaa mbalimbali kwa uwekezaji mdogo tu kwenye website na application za simu.

Anza leo na kuna siku utakuja kunishukuru.Uskubali CV yako iwe tupu kwamba huna kazi wakati unaweza kusajili jina la biashara na ukawa Mwajiriwa katika Biashara yako hata kama huna mshahara.Ukiona huwezi andika cheo kikubwa basi sema tu uko Field kwenye kampuni yako mwenyewe hakuna atakayekuuliza maswali.

Kama Unahitaji kanzisha kampuni yako ya mfukoni (Briefcase Company) Wasiliana nasi kwa email masokotz@yahoo.com ili tuone namna tunaweza kusaidiana.

Karibuni tujadili namna bora ya kuanzisha na kusimamia Briefcase Companies na Faida na Changamoto zake.
Uzi una madini mazuri🤛online business ukiwa na full package ya skills ni kupiga pesa tu, kuna kipindi niliamua kukomaa na online business yangu as MR.MIKEKA , Nilikuwa nawasaidia watu kutengeneza pesa kupitia kubeti, katika kufanya accounting records zangu nilijikuta per month nimefunga kwa sales za tsh 300,000 , tena business nilikuwa naifanya kwa kutumia smartphone yangu tu nimetulia ghetto😀😀
 
Kama Unahitaji kanzisha kampuni yako ya mfukoni (Briefcase Company) Wasiliana nasi kwa email masokotz@yahoo.com ili tuone namna tunaweza kusaidiana.Tutshirikiana na wewe kufanya yafuatayo:

  1. Kusajili Biashara yako BRELA,TRA,LESENI,na VIBALI Vingine
  2. Kufungua Akaunti Bank
  3. Kuandaa Company Profile ikiwa ni pamoja na LOGO,WEBSITE,EMAILS etc
  4. Kutuma cold emails kwa potential Clients ikiwa ni pamoja na kufanya Appointments
  5. Kuandaa Job description kwa nafasi mbalimbali na kufanya shorlisting pamoja na interview.
  6. Kuwa na wewe katika hatua za mwanzo za biashara yako mpaka itakapoimarika na kukusaidia kupata ushauri wa kitaalam kwa gharama nafuu
 
Mfano nikitaka kufanya the same business as company nilioajiriwa, brela kule wakinichunguza si wataona jina langu kwamba mmiliki
 
Mfano nikitaka kufanya the same business as company nilioajiriwa, brela kule wakinichunguza si wataona jina langu kwamba mmiliki
Inategemea.Hata kama wakifahamu kumbwe unafanya biashara sawa na ajira yako sio kinyume cha sheria lakini inaweza leta mgogoro wa kimaslahi na mwajiri wako.Cha muhimu inategemea na aina ya biashara.Lakini Pia inategemea na mkataba wako wa ajira unasemaje.
 
Inategemea.Hata kama wakifahamu kumbwe unafanya biashara sawa na ajira yako sio kinyume cha sheria lakini inaweza leta mgogoro wa kimaslahi na mwajiri wako.Cha muhimu inategemea na aina ya biashara.Lakini Pia inategemea na mkataba wako wa ajira unasemaje.
Hapo ndio pana utata, sitaki wajue kama mimi ni owner kwa sababu zangu binafasi na kuhusu mgogoro wa kimaslahi material naunua ofisini ila sitaki tu wajue nina kampuni yangu
 
Hapo ndio pana utata, sitaki wajue kama mimi ni owner kwa sababu zangu binafasi na kuhusu mgogoro wa kimaslahi material naunua ofisini ila sitaki tu wajue nina kampuni yangu
Tuwasiliane kwa 0710323060 tuangalie namna ya kushughulika na case yako.Karibu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom