Fahamu kuhusu Kampuni za Mfukoni-Briefcase Corporations

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,434
5,404
Habari za wakati huu;

Je unajua kuwa biashara zote kubwa zilianza kama wazo? Je, unajua kwama biashara nyingi kubwa zilianza kama briefcase companies? Je, unajua kuwa biashara nyingi kubwa zilianza chini?Leo nataka nizungumze kuhusu Briefcase Companies na umuhimu wa kuwa na Kabiashara kako ka Briefcase

Briefcase Company ni kampuni ambazo zina exist ama on paper only (Registered) au zina operate nyuma ya Kampuni nyingine kama Cover. Ni aina ya kampuni ambayo inaweza kuwa inaundwa na watu wa chache, haina bidhaa maalum wala huduma, haina anuani maalum ya biashara lakini ina vibali vyote vya msingi vya kuweza kufanya biashara. Briefcase Company inaweza kuwa ni Limited Company au Sole Proprietorship. Kmapuni inaweza kuanza kama Briefcase Company na baadaye ikakua na kuwa biashara kamili yenye TIJA.

Nini faida ya Briefcase Company? Faida za Briefcase Company ni nyingi sana.

Kwanza inakuwezesha kutumia fursa za kibiashara pindi zinapojitokeza bila kupata ugumu. Mfano kama wewe ni mwajiriwa na ikatokea ofisini kuna kakazi ambako kanahitajika kufanywa kwa kutumia mtu wa nje unaweza kutumia briefcase Company yako kufanya hio kazi bila kuleta mgogoro wa maslahi.

Pili iwapo hauna ajira ya kudumu unaweza kuweka Briefcase Company yako katika CV yako na ukajipa Cheo na majukumu kama yale unayotaka kufanya kulingana na uzoefu na utaalamu wako
Tatu unaweza kutumia Briefcase Company kutafuta mikataba ya kibiashara, dili za kibiashara na ukashirikiana na kampuni kubwa zenye ukwasi katika kuzitekeleza.

Katika karne hii ya ishirini na moja ni Rahisi zaidi kuanzisha Briefcase Companies ambazo kwa sasa zimekuwa zikiitwa Virtual Business/Digital Business. Hizi ni aina ya Biashara ambazo zinaendesha na kusimamiwa kwa njia ya mtandao, zinauza na kununua bidhaa na huduma kwa njia ya mtandao. Aina hii ya biashara ina maana kwama huhitaji Ofisi kwa ajili ya kuweka stock ya mzigo wala watu kuka kufanya kazi kwani kila kazi inaweza kufanywa kwa njia ya teknolojia.

Mfano Rahisi ni Jamii Forums Mmiliki wa JF anaweza weka Servers za JF Nyumbani kwake au akakodi toka kwa kampuni zinazotoa huduma hizo popote duniani. Kisha hawa moderators wakawa wanafanya kazi wakiwa sehemu tofauti kwa njia ya mtandao kulima watu ban na kufuta post za watu ili jukwaa liendelee kuwa safi na kazi ikaenda.

Ukitazama utaona kwamba hii kampuni haitahitaji kuwa na phyisical office, ndio maana hutasikia mod wa JF anakwambia ukiwa na malalamiko njoo ofisini tuyashughulikie mnamaliza kila kitu mtandaoni. Hii ina maana kwamba teknolojia inatumika vizuri.

Kinachosumbua watu wengi ni ama kutokuwa na ujuzi wa kutumia teknolojia au kutokujua waanzie wapi katika kuanzisha hio Kampuni ya Briefcase. Kuna namna nyingi za kuanzisha Briefcase Company na leo nitazungumzia moja ambayo ni rahisi. Fuata hatua zifuatazo ili kuanzisha Kampuni ya Briefcase.

  1. Hatua ya kwanza ni kutambua ujuzi au utaalamu wako. Hakikisha Angalau unakuwa na utaalamu fulani mfano unaweza kuwa na Genge la Nyanya, Muuza Karanga au Muuza mkaa. Sasa hakikisha kwamba unajenga mfumo wako wa biashara kwa kuzingatia hilo kwani biashara yako ndogo lazima uwe na maono makubwa nayo. Mfano Biashara ya mkaa inaweza husiana na sector ya Domestic energy au Forest Management, Biashara ya Karanga na genge la nyanya inaweza husiana na Kilimo biashara.
  2. Pili chagua Jina la Biashara ambalo litakua pamoja na Biashara yako.
  3. Kulingana na aina ya biashara unaweza kuanzisha kurasa za mitandao ya kijamii na hata tovuti ili uweze kurahisisha mawasiliano
  4. Sajili jina la biashara, tafuta leseni na Ufungue bank account kwa kutumia Jina la Biashara.
Ukishakuwa na hivyo tayari unayo Biashara yako ya Mfukoni ambayo sasa unaweza kuhangaika kuitafutia mtaji, wateja na bidhaa au huduma.

Ukishakuwa na Kampuni yako hakikisha unakuwa na Business cards na unakuwa active kuipeleka biashara yako sokoni. Kwa mfano unaweza anza kwa kuwatafuta wateja wa karibu na marafiki kisha ukaongeza na wengine. Zingatia Mfano niliotoa ni mfano mdogo.

Hata hivyo teknolojia inakuruhusu kuanzisha ecommerce shops za kuuza bidhaa mbalimbali kwa uwekezaji mdogo tu kwenye website na application za simu.

Anza leo na kuna siku utakuja kunishukuru.Uskubali CV yako iwe tupu kwamba huna kazi wakati unaweza kusajili jina la biashara na ukawa Mwajiriwa katika Biashara yako hata kama huna mshahara.Ukiona huwezi andika cheo kikubwa basi sema tu uko Field kwenye kampuni yako mwenyewe hakuna atakayekuuliza maswali.

Kama Unahitaji kanzisha kampuni yako ya mfukoni (Briefcase Company) Wasiliana nasi kwa email masokotz@yahoo.com ili tuone namna tunaweza kusaidiana.Tutshirikiana na wewe kufanya yafuatayo:

  1. Kusajili Biashara yako BRELA, TRA, LESENI, na VIBALI Vingine
  2. Kufungua Akaunti Bank
  3. Kuandaa Company Profile ikiwa ni pamoja na LOGO, WEBSITE, EMAILS etc
  4. Kutuma cold emails kwa potential Clients ikiwa ni pamoja na kufanya Appointments
  5. Kuandaa Job description kwa nafasi mbalimbali na kufanya shorlisting pamoja na interview.
  6. Kuwa na wewe katika hatua za mwanzo za biashara yako mpaka itakapoimarika na kukusaidia kupata ushauri wa kitaalam kwa gharama nafuu

Karibuni tujadili namna bora ya kuanzisha na kusimamia Briefcase Companies na Faida na Changamoto zake.
 
Umesahau beneficiries wote wanatakiwa Brela? Sasa utafichaje usijulikane kuwa ni mhusika wa kampuni
Mkuu,

Unajua sual beneficiaries ni kitu kingine. Beneficiary ni mtu ambaye ndo mnufaika wa mwisho wa maslahi ya kampuni. Mimi hapa ninachozungumzia sio kujificha usionekane bali ni kuonekana bila kutazamwa. Kama umeelewa gonga like.
 
Mimi nafanya hii, imenisaidia sana.

Niko na kila kitu cha kampuni,

Niko registered BRELA, TRA niko msafi, niko nakata leseni za biashara kila mwaka,

Nimeajiri mtu mmoja wa kunisaidia mishe zangu, kazi zingine natumia vibarua au nauza kazi kwa mtu anafanya me namlipa wakati nasubiri kulipwa huku.

Sina ofisi, ila napelekaga mkataba wa pango TRA kwa ajili ya withholding ya pango.

Nipo hadi na risiti ya EFD na VAT, na VAT yao nalipa kila mwezi.

Mungu akisaidia mwakani naweza kuwa na physical location.

Kazi nyingi napata kutoka kwa marafiki, na watu niliofanya nao kazi wananiunganisha kwa wengine.
 
Asante kwa ushuhuda Huu.Naamni unaweza kuwapa uzoefu watu kuhusu urahisi na ugumu wa aina hii ya biashara
 
Asante kwa ushuhuda Huu.Naamni unaweza kuwapa uzoefu watu kuhusu urahisi na ugumu wa aina hii ya biashara
Tusiseme ugumu, bali changamoto

1. Mtu uliyempa kazi akizingua inakuwaga balaa, coz sometimes unapokea kazi ambayo huna uzoefu nayo, ila ndo ukipiga hesabu unaona kuna faida unaingia.

2. Kuandaa mahesabu ya mwisho wa mwaka, huwa ni changamoto kwasababu kutunza kumbukumbu ni ngumu na kazi kubwa unafanya mtu mmoja hivyo huwa ni balaa, hasa kipindi kama hiki. Mimi hesabu za 2021 hazija balansi hadi muda huu na imebaki mwezi mmoja tu.

3. Wahasibu na watu wa manunuzi wa makampuni ninayofanya nayo kazi kuzungusha malipo hadi uwapoze, sasa nishajua jinsi ya kupambana nao.

Faida.
1. Ukiweka juhudi unaona pesa ikija na unakuwa na maamuzi juu ya faida. Cha msingi kuwa na focus na kuwa determined.
 
Good,Hayo ulosema ni kweli.

Kwenye kutunza kumbukumbu zipo solutions ambazo wengi wanazitumia za kiteknolojia nafikri hata wewe unaweza kuzitumia.Kwenye kuandaa hesabu za mwisho wa mwaka cha muhimu na kuhakikisha kwamba unakuwa na makusanyo ya Risiti za kukutosha na unaziscan na kuzihifadhi kwa njia ya kidigitali nayo inasaidia kupunguza headache.

Hata hivyo kadiri biashara inavokuwa kuna ahatua itafika utakuwa na uwezo wa kufanya shughuliz ako kwa uhuru kwa kadiri biashara inavokua.

Lakini pia unaweza kujiongezea ujuzi kwa kufanya mafunzo mtandaoni
 
Mtoa Mada nakuuna mkono na Mimi Binafsi tulifungu Partnership mwaka juzi ikiwa kwenye makaratas tunamshukuru Mungu Sasa Tumeingia kwnye VRN last week na Ofisi ipo MAGOMENI
Tumeajiri vijana wa 5 permanently na 3 temp-Vibarua

Kampuni inadeal na Ufungaji CCTV camera,Electrical Fence ,GPS Tracking, n.k (insta @cimax_tech_solutions au www.climaxtechsolutions.co.tz)

Nilivyoingia kwenye VAT for the first time nikajipiga kifua nikaajiita "Managing Director " nikamalizia kwa kicheko Kikubwa Sana

Jamani kila kitu is possible nakaribisha wawekezaji Sasa tuinvest kwenye GPS tracker na tracking nna proposal Idea kubwa Sana na nzuri changamoto no CAPITAL TU
 
Hongereni sana.

Kupata VRN huongeza CV

Me kabla nipate VRN kuna taasisi zilikuwa zinagoma kufanya kazi na sisi. Baada ya kupata imekuwa rahisi
 
Hongera sana mtoa mada, binafsi nasaidia au nipo kama consultant kwa wale wanaohitaji KUSAJILI BIASHARA/KAMPUNI, kUANDAA HESABU ZA KAMPUNI, KUANDAA MEMORANDUM, KUFANYA MAKADIRIO YA KODI N.K. kiujumla nimekusoma sana mada yako imekaa vizuri sana. keep it up
 
Similar Discussions

15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom