Fahamu kuhusu Kampuni za Mfukoni-Briefcase Corporations

Hapo ndio pana utata, sitaki wajue kama mimi ni owner kwa sababu zangu binafasi na kuhusu mgogoro wa kimaslahi material naunua ofisini ila sitaki tu wajue nina kampuni yangu
Mkuu mtoa maada ametoa siri ya mafanikio ya baadhi ya watu. Kwa case yako unaweza muandikisha ndugu au rafiki then wewe ukasimamia kila kitu cha msingi wote mnufaike.
 
Kwa wale wenye kampuni za mifukoni.Msisahau kufanya estimates za TRA,Annual returns za TRA na BRELA.Kwa estimates mwisho ni march 30
 
Habari za wakati huu;

Je unajua kuwa biashara zote kubwa zilianza kama wazo?Je unajua kwama biashara nyingi kubwa zilianza kama briefcase companies?Je unajua kuwa biashara nyingi kubwa zilianza chini?Leo nataka nizungumze kuhusu Briefcase Companies na umuhimu wa kuwa na Kabiashara kako ka Briefcase

Briefcase Company ni kampuni ambazo zina exist ama on paper only(Registered) au zina operate nyuma ya Kampuni nyingine kama Cover.Ni aina ya kampuni ambayo inaweza kuwa inaundwa na watu wa chache,haina bidhaa maalum wala huduma,haina anuani maalum ya biashara lakini ina vibali vyote vya msingi vya kuweza kufanya biashara.Briefcase Company inaweza kuwa ni Limited Company au Sole Proprietorship.Kmapuni inaweza kuanza kama Briefcase Company na baadaye ikakua na kuwa biashara kamili yenye TIJA.

Nini faida ya Briefcase Company?Faida za Briefcase Company ni nyingi sana.

Kwanza inakuwezesha kutumia fursa za kibiashara pindi zinapojitokeza bila kupata ugumu.Mfano kama wewe ni mwajiriwa na ikatokea ofisini kuna kakazi ambako kanahitajika kufanywa kwa kutumia mtu wa nje unaweza kutumia briefcase Company yako kufanya hio kazi bila kuleta mgogoro wa maslahi.

Pili iwapo hauna ajira ya kudumu unaweza kuweka Briefcase Company yako katika CV yako na ukajipa Cheo na majukumu kama yale unayotaka kufanya kulingana na uzoefu na utaalamu wako
Tatu unaweza kutumia Briefcase Company kutafuta mikataba ya kibiashara,dili za kibiashara na ukashirikiana na kampuni kubwa zenye ukwasi katika kuzitekeleza.

Katika karne hii ya ishirini na moja ni Rahisi zaidi kuanzisha Briefcase Companies ambazo kwa sasa zimekuwa zikiitwa Virtual Business/Digital Business.Hizi ni aina ya Biashara ambazo zinaendesha na kusimamiwa kwa njia ya mtandao,zinauza na kununua bidhaa na huduma kwa njia ya mtandao.Aina hii ya biashara ina maana kwama huhitaji Ofisi kwa ajili ya kuweka stock ya mzigo wala watu kuka kufanya kazi kwani kila kazi inaweza kufanywa kwa njia ya teknolojia.

Mfano Rahisi ni Jamii Forums Mmiliki wa JF anaweza weka Servers za JF Nyumbani kwake au akakodi toka kwa kampuni zinazotoa huduma hizo popote duniani.Kisha hawa moderators wakawa wanafanya kazi wakiwa sehemu tofauti kwa njia ya mtandao kulima watu ban na kufuta post za watu ili jukwaa liendelee kuwa safi na kazi ikaenda.Ukitazama utaona kwamba hii kampuni haitahitaji kuwa na phyisical office ndo maana hutasikia mod wa JF anakwambia ukiwa na malalamiko njoo ofisini tuyashughulikie mnamaliza kila kitu mtandaoni.Hii ina maana kwamba teknolojia inatumika vizuri.

Kinachosumbua watu wengi ni ama kutokuwa na ujuzi wa kutumia teknolojia au kutokujua waanzie wapi katika kuanzisha hio Kampuni ya Briefcase.Kuna namna nyingi za kuanzisha Briefcase Company na leo nitazungumzia moja ambayo ni rahisi.Fuata hatua zifuatazo ili kuanzisha Kampuni ya Briefcase.

  1. Hatua ya kwanza ni kutambua ujuzi au utaalamu wako.Hakikisha Angalau unakuwa na utaalamu fulani mfano unaweza kuwa na Genge la Nyanya,Muuza Karanga au Muuza mkaa.Sasa hakikisha kwamba unajenga mfumo wako wa biashara kwa kuzingatia hilo kwani biashara yako ndogo lazima uwe na maono makubwa nayo.Mfano Biashara ya mkaa inaweza husiana na sector ya Domestic energy au Forest Management,Biashara ya Karanga na genge la nyanya inaweza husiana na Kilimo biashara.
  2. Pili chagua Jina la Biashara ambalo litakua pamoja na Biashara yako.
  3. Kulingana na aina ya biashara unaweza kuanzisha kurasa za mitandao ya kijamii na hata tovuti ili uweze kurahisisha mawasiliano
  4. Sajili jina la biashara,tafuta leseni na Ufungue bank account kwa kutumia Jina la Biashara.
Ukishakuwa na hivyo tayari unayo Biashara yako ya Mfukoni ambayo sasa unaweza kuhangaika kuitafutia mtaji,wateja na bidhaa au huduma.

Ukishakuwa na Kampuni yako hakikisha unakuwa na Business cards na unakuwa active kuipeleka biashara yako sokoni.Kwa mfano unaweza anza kwa kuwatafuta wateja wa karibu na marafiki kisha ukaongeza na wengine.Zingatia Mfano niliotoa ni mfano mdogo.

Hata hivyo teknolojia inakuruhusu kuanzisha ecommerce shops za kuuza bidhaa mbalimbali kwa uwekezaji mdogo tu kwenye website na application za simu.

Anza leo na kuna siku utakuja kunishukuru.Uskubali CV yako iwe tupu kwamba huna kazi wakati unaweza kusajili jina la biashara na ukawa Mwajiriwa katika Biashara yako hata kama huna mshahara.Ukiona huwezi andika cheo kikubwa basi sema tu uko Field kwenye kampuni yako mwenyewe hakuna atakayekuuliza maswali.

Kama Unahitaji kanzisha kampuni yako ya mfukoni (Briefcase Company) Wasiliana nasi kwa email masokotz@yahoo.com ili tuone namna tunaweza kusaidiana.Tutshirikiana na wewe kufanya yafuatayo:

  1. Kusajili Biashara yako BRELA,TRA,LESENI,na VIBALI Vingine
  2. Kufungua Akaunti Bank
  3. Kuandaa Company Profile ikiwa ni pamoja na LOGO,WEBSITE,EMAILS etc
  4. Kutuma cold emails kwa potential Clients ikiwa ni pamoja na kufanya Appointments
  5. Kuandaa Job description kwa nafasi mbalimbali na kufanya shorlisting pamoja na interview.
  6. Kuwa na wewe katika hatua za mwanzo za biashara yako mpaka itakapoimarika na kukusaidia kupata ushauri wa kitaalam kwa gharama nafuu

Karibuni tujadili namna bora ya kuanzisha na kusimamia Briefcase Companies na Faida na Changamoto zake.
Sawa!
 
Wabari jfs,
Tunakumbushwa
 

Attachments

  • 20230517_184110_0001.png
    20230517_184110_0001.png
    206.1 KB · Views: 29
Huu uzi umenipa morali,hapa nipo njiani kuelekea TRÀ kufanyiwa estimates ya kodi,nifanye biashara.Nina business name tu.
Nshakadiriwa,nimewalipa,kilichobaki ni leseni tu,ambayo nimejaribu kuingia kwenye mfumo wa TAUS,mtandao unasumbua,hope wiki ijayo ntakamilisha
 
Nshakadiriwa,nimewalipa,kilichobaki ni leseni tu,ambayo nimejaribu kuingia kwenye mfumo wa TAUS,mtandao unasumbua,hope wiki ijayo ntakamilisha
Nafurahi kwamba umepiga hatua.Ni jambo zuri.Iwapo unahitaji huduma zetu nyingine usisite kuwasiliana nasi.Tunakutakia mafanikio katika biashara yako.
 
Nafurahi kwamba umepiga hatua.Ni jambo zuri.Iwapo unahitaji huduma zetu nyingine usisite kuwasiliana nasi.Tunakutakia mafanikio katika biashara yako.
Mkuu option ya kukupata ni hiyo ya email tu? Maana namba uliyoweka hapo juu haipatikani..
 
Usichelewe kuanzisha Kampuni yako.Tuwasiliane leo kwa email:masokotz@yahoo.com

Mkuu,kama umesoma andiko kwa umakini na unataka kuanzisha microfinance basi ni swala la hatua kwa hatua.
Nimejaribu kuwasiliana nawe kwa namba ulizonipa pm, bahati mbaya ni kwamba haijawahi kupatikana hata nilipojaribu mara kadhaa, mkuu nadhani si sawa kuassume kwamba kila muhitaji atakupata kwa njia ya email pekee, badilika mkuu.
 
Nimejaribu kuwasiliana nawe kwa namba ulizonipa pm, bahati mbaya ni kwamba haijawahi kupatikana hata nilipojaribu mara kadhaa, mkuu nadhani si sawa kuassume kwamba kila muhitaji atakupata kwa njia ya email pekee, badilika mkuu.
Mkuu samahni kama tunapishana hewani.Nimekupm.Unawezamnipatia namba yako nikupigie.

Appologies
 
Je Umeshaanzisha Kampuni Yako?Kama bado Tuwasiliane kwa email:masokotz@yahoo.com
Habari mkuu, je unashauri vipi kwenye scenario ifuatayo: kuna watu wanne (na mimi nikiwepo) ila sisi wawili tuna kampuni tayari ila wawili hawana, kuna haja ya kufungua kampuni nyingine au wawili wafungue kisha tuwe na LLP? Au ifunguliwe kampuni moja ila baadi ya shares zimilikiwe na kampuni iliyotangulia?
 
Habari mkuu, je unashauri vipi kwenye scenario ifuatayo: kuna watu wanne (na mimi nikiwepo) ila sisi wawili tuna kampuni tayari ila wawili hawana, kuna haja ya kufungua kampuni nyingine au wawili wafungue kisha tuwe na LLP? Au ifunguliwe kampuni moja ila baadi ya shares zimilikiwe na kampuni iliyotangulia?
Uamuzi unategemea na Malengo ya Hiyo Kampuni Mpya na Shughuli zinazaofanywa na hiyo kampuni ya Zamani.Kwa Tanzania hatuna mfumo wa LLP.Ulijadiliwa ila haukufikia Muafaka.Ili kukupa ushauri mzuri ningependa kufahamu zaidi kuhusu malengo ya kampuni ya sasa na Malengo ya kampuni Mpya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom