Fahamu Aina za Kodi Zinazotozwa Pindi unapoingiza Gari Nchini

zachaja

Senior Member
May 16, 2015
153
193
Kodi zifuatazo hutozwa kwenye magari yanayoingia nchini;

1. Ushuru wa forodha (Import Duty): asilimia 25% ya thamani ya kununulia gari (CIF Value)
2. Ushuru wa bidhaa (Excise Duty due to CC-EX): asilimia 0%, 5% & 10% kutegemea na ukubwa engine (chini ya 1000cc= 0%, cc 1000 mpaka 1,999=5% & cc zaidi ya 2000= 10%) ya thamani ya gari (CIF) PLUS Ushuru wa Forodha.
3. Uchakavu (Excise Duty due to Age-EXA): asilimia 15% & 30% kutegemea na na umri (zaidi ya miaka 3 na chini ya miaka 8= 15%, zaidi ya miaka 10 toka litengenezwe= 30%) ya thamani ya gari (CIF) PLUS Ushuru wa Forodha.
4. Ushuru wa maendeleo ya Reli (Railway Development Levy-RDL): 1.5% ya thamani ya gari (CIF).
5. Tozo ya Forodha (Customs Processing Fee-CPF):0.6% ya thamani ya gari bila Bima (FOB).
6. Ada ya Usajiri (Motor Vehicle Registration Fee-VEH): TZS-450,000, TZS-500,000 & TZS-550,000 hapa inategemea na ukubwa wa Engine.
7. VAT:18% ya Thamani ya gari (CIF) PLUS kodi zote zilizokokotolewa hapo juu.

NOTE:
a). Kwa magari mapya (gari lisilozidi miaka 3) hayatozwi kodi ya uchakavu
b). Magari yanayotumia umeme hayatozwi kodi ya ushuru wa bidhaa.

“Kwa huduma bora zifuatazo karibu Ruaha Freight Ltd;
1. Clearing & Forwarding kwa mizigo aina yote (Magari, container & Loose Cargo),
2. Kusaidia kuhamisha umiliki wa vyombo vya moto (Motor vehicle ownership transfer-Dar pekee).
 
Laiti kama tungekuwa tukimaliza CIF pekeyake tunakuja kulipia ushuru wa forodha Tu nadhani kila mtanzania angemiliki chuma
 
Kwa style hii sjui kama ntamiliki gari
IMG_20240114_094749.jpg
 
Back
Top Bottom