Facts: Chanzo cha Mgomo wa Madaktari

Facts: Chanzo cha Mgomo wa Madaktari

Kasheshe

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2007
Posts
4,694
Reaction score
793
Jamani acheni kutafuta mchawi; chanzo cha mgomo mrefu ukiacha ule wa mwanzo wa interns ni Posho za Wabunge! Kwa kuwa chanzo hicho kinajulikana; solution pia inajulikana.
  1. Wabunge waondoe mpango wa kulipana posho.
  2. Kwa kuwa walishaonyesha inawezekana kulipana watalazimika waongeze malipo ya madaktari from 10,000TZS to at least 30,000TZS
Mubarikiwe Waungwana.
 
For the first time you seem to understand
 
mimi ukinipa mshahra wa 2.5m sitaki kabisa posho...hivi jamani hadi maji marefu na lusinde wananipita mshahara!!!!this system is criminal
 
ningependa facts ziwekwe hapa jamvini.mambo ya kusubiri kamati naona ni uzushi tu
 
2subiri kamati ije na majibu ya kisiasa
 
Uongozi wote wa wizara ya afya ukiondolewa, bila shaka madaktari watarudi kazini bila masharti yoyote.
 
Mwalimu Julius Kambarage aliwahi kusema katika moja ya hotba zake. Wazanaki wanasema hivi, Wazanaki wanasema hivi "UBUBISUBISU OBUWERE EKIRO KIRIMBURA" ikiwa na maana Mfichaficha maradhi kilio kitamfichua.
 
Mwalimu Julius Kambarage aliwahi kusema katika moja ya hotba zake. Wazanaki wanasema hivi, Wazanaki wanasema hivi "UBUBISUBISU OBUWERE EKIRO KIRIMBURA" ikiwa na maana Mfichaficha maradhi kilio kitamfichua.
na wewe wasemaje
 
bado naamini chanzo kilikuwa huku huku kwenye posho za interns na baadae jinsi viongozi walivyoshughulikia suala hili.
MAELEZO KUHUSU SAKATA LA INTERNS HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI
Mgogoro huu ulihusisha Interns wa kozi za madaktari wa binadamu (119), wafamasia (61), wataalamu wa maabara (21) na madaktari wa meno (20) =221.
Kawaida posho huwa zinafika hospitalini tarehe 22 ya kila mwezi na kupatikana kwenye akaunti za interns kati ya tarehe 22-26. Kwa mwezi wa kumi na kumi na moja tulilipwa na hospitali, sababu fedha hizo zilikuwa hazijafika kutoka wizarani. Tatizo la ucheleweshaji wa posho ulikuwa umeishajitokeza hata awali kwa mfano posho ya mwezi wa kumi ambayo ilipitiliza na kulipwa tarehe 10, Novemba sababu ikiwa ni ile ile kwa wizara kutokufikisha fedha za malipo hospitalini hivyo hospitali ikaamua kulipa fedha hizo.
Sababu kubwa: kucheleweshwa kwa Posho za mwezi Desemba, 2011.
Ufuatiliaji uliofanyika:
1. Siku ya tarehe 27/12/2011 viongozi wa interns walikutana na mkurugenzi wa fedha wa hospitali ya taifa ya Muhimbili Mr. Cassian kuongelea suala hilo naye akajibu fedha hazijafika kutoka wizarani na vile vile hospitali haijapokea fedha kwa ajili ya matumizi mengine (other charges) kwa muda wa miezi mitatu.
2. Uongozi wa Interns uliamua kuonana na uongozi wa mafunzo na ajira hospitali ya taifa ya Muhimbili ambao walishauri kwenda kuonana na mkurugenzi mkuu wa hospitali.
3. Siku hiyo hiyo baada ya kukutana na mkurugenzi wa hospitali alisema hospitali haijapokea fedha kwa kipindi cha miezi mitatu na kuamua kuwasiliana na uongozi wa wizara, aliamua kuahirisha kikao na kuomba kukutana naye baada ya kupata majibu kutoka wizarani.
Muda wa saa tisa alasiri uongozi wa intern ulikutana na uongozi wa hospitali (mkurugenzi wa hospitali, mkurugenzi wa tiba, mkurugenzi wa upasuaji, mkurugenzi wa fedha) pamoja na wawakilishi kutoka wizara ya afya ambao walikuwa Mkurugenzi msaidizi wa tiba (Dr. Mung'ong'o ) na mkurugenzi msaidizi wa "curative services" Dr. Ayoub Maghimba. Wizara ilitamka kuwa haina fedha kwa ajili ya posho hizi sababu zilikuwa hazijapatikana kutoka hazina. Wizara iliahidi kufikia tarehe 30 mwezi wa kumi na moja posho hizo zitakuwa tayari kwenye akaunti ya hospital ya taifa ya Muhimbili.
Na mkurugenzi wa fedha wa muhimbili aliahidi kuwa tarehe 31, Desemba atahakikisha fedha hizo zimeingia kwenye akaunti za interns.
Vile vile uongozi wa wizara uliofika ulikubaliana na uongozi wa Intern kuendelea kufuatilia tatizo hilo kupitia mkurugenzi wa hospitali ya taifa ya Muhimbili siku ya tarehe 29 Desemba, ili kupata ripoti ya ufuatiliaji wa fedha hizo.
4. Tarehe 29 Desemba uongozi wa interns ulionana na uongozi wa hospitali ili kupata mrejesho kutoka wizarani, hata hivyo hakukuwa na taarifa yoyote iliyokuwa imefika na mkurugenzi wa hospitali ya taifa ya Muhimbili aliamua kuwasiliana kwa simu na wawakilishi wale wa wizara waliokuja bila mafanikio, hatimaye kuamua kuwasiliana na katibu mkuu wa wizara ya afya aliyejibu "wizara haijapokea fedha kutoka hazina na pia kwa kuwa interns ni wazalendo anaomba tuendelee kufanya kazi".
5. Uongozi wa Interns ulimuomba mkurugenzi wa hospitali ya taifa ya Muhimbili kukutana na interns wote ili kutoa taarifa hii (baada ya kupata ruhusa kutoka kwa katibu mkuu kuongea kwa niaba yake ambaye ndiye mwajiri wetu)
6. Tarehe 30 Desemba uongozi wa hospitali uliitikia wito na kukutana na interns wote majira ya saa nane. Baada ya kikao na majadiliano ya muda mrefu interns waliomba uongozi wa hospitali kuwapatia angalau sh 100,000Tshs kwa kila mmoja kwa ajili ya kujikimu kama sehemu ya posho wakingojea fedha zitakapofika kutoka wizarani, hata hivyo uongozi wa hospitali ulisema hauna fedha hizo (ambayo jumla ilikuwa ni kama Tshs 22,600,000/=)
Mapendekezo yaliyotolewa na uongozi wa Hospitali.
• Mkurugenzi wa hospitali ya taifa ya Muhimbili aliahidi ataendelea kushughulikia suala hili pamoja na uongozi wa interns kwa kwenda wizarani pamoja siku ya tarehe 02/01/2012.
7. Tarehe 02/01/2012 uongozi wa interns ulienda kuonana na mkurugenzi wa hospitali ya taifa ya Muhimbili ili kuomba kuambatana naye kuelekea Wizara ya Afya kama alivyoahidi, hata hivyo haukufanikiwa sababu mkurugenzi alisema anashughulikia majukumu mengine ya hospitali, hivyo uongozi wa intern uliondoka peke yake hadi Wizara ya Afya.
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
• Uongozi wa Intern ulifanikiwa kuonana na Mganga mkuu wa serikali. Vile vile walikuwepo viongozi wa interns kutoka hospitali ya Bombo, Mount Meru, Temeke na Amana.
• Mganga mkuu alitoa taarifa kuwa atawasiliana na uongozi wa hospitali ya taifa ya Muhimbili na Taasisi ya mifupa ya Muhimbili (MOI) ili kutumia mapato ya ndani ya hospitali hizo kulipia posho za interns na kwa upande wa hospitali za mikoani atawasiliana na wakuu wa mikoa husika watumie mapato yao ili kuweza kulipia posho hizo na fedha hizo zitarejeshwa kwa kuombewa mkopo wa dawa kutoka bohari ya dawa ya taifa (msd).
• Kikao kilipokuwa kinakaribia ukingoni katibu mkuu aliingia na kutoa kauli kuwa serikali haina fedha ila ameshapata fedha hizo na zingefika hospitali hizo ndani ya siku chache za usoni (Haya hayakuweza kuwekwa kwenye maandishi, ilibaki tu kama ahadi)
Kutokana na ahadi hizo ambazo hazikuwa timilifu na ugumu wa maisha kutokana na kukosa fedha za kujikimu interns waliamua kuandika barua kwa katibu mkuu wizara ya afya ya kuelezea kutokuweza kufika maeneo yao ya kazi kuanzia tarehe 03/01/2012 mpaka pale watakapopewa fedha hizo.
Tarehe 03/01/2012;
Baada ya uongozi wa wizara kupata taarifa ulikuja ujumbe kuwa katibu mkuu aliomba kukutana na interns wote muda wa saa sita na nusu mchana, hata hivyo alikuja mganga mkuu wa serikali saa saba na nusu mchana. Baada ya kusikiliza hoja alitoa vitisho mbalimbali na kusihi watu warudi kazini. Pia aliahidi fedha hizo zingeingia kati ya siku ya jumanne (03/01/2012) au jumatano (04/01/2012).

Tarehe 05/01/2012;
Fedha hizo zilikuja kuingia siku ya tarehe 05/01/2012 saa kumi na moja jioni. Na mara baada ya fedha kuingia interns walirudi kazini (majira ya saa kumi na moja jioni) na kuendelea na kazi kama kawaida.
Tarehe 06/01/2012;
Uongozi wa hospitali ulitoa barua kwa kila Intern kurudi wizara ya afya na ustawi wa Jamii. Barua hiyo ilieleza kuwa tumekiuka makubaliano ya mafunzo kwa vitendo (internship Agreement) baina yetu na Hospitali ya Taifa Muhimbili; kufungu na 1(b), (d), (e), (f) na (g). Vile vile ikimtaka katibu mkuu wa wizara ya afya na ustawi ya jamii kutupangia sehemu nyingine.
Mnamo taarehe 09/01/2012 wizara afya iliamua kutupangia vituo tofauti huku baadhi yetu walirudishwa hospitali ya taifa Muhimbili; madaktari 86, wafamasia 35 na wataalamu wa maabara 13 jumla ni 134.
Idadi ya intern waliopangiwa vituo vingine.
Hospitali ya manispaa ya Temeke- Madaktari 9, Wafamasia 2 na wataalamu wa maabara 1=12
Hospitali ya manispaa ya Amana-Madaktari 13, Wafamasia 3 na wataalamu wa maabara 3=19
Hospitali ya manispaa ya M/nyamala-Madaktari 10, Wafamasia 2 na wataalamu wa maabara 4=16
Hospitali ya jeshi Lugalo-Madaktari 7.
Hospitali ya Aga Khan-Madaktari 5 na wafamasia 2=7

Kitendo hiki cha kuhamisha interns kimekiuka ‘internship guidelines for medical and dental practitioners of medical council of tanganyika 2009' Katika kifungu cha nne aya ya nne "internship training should commence immediately and within 3-months of completion of undergraduate training and continue uninterrupted for twelve months."

MAMBO YALIYOPOTOSHWA NA WIZARA YA AFYA.

• Baada ya upangaji huu wizara ya afya ilisema kuwa haitoweza kurudisha interns wote katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa vile tayari walikwisha peleka interns 51 wakati ni madaktari 29 tu na hawa hawakuja kuchukua nafasi bali walikuwa wamepangiwa tangu mwezi November 2011 wafike muhimbili tarehe 02/01/2012, kama viambatanisho vinavyo onyesha.

Sababu iliyo tolewa na wizara ya Afya kuwa hospitali ya Muhimbili haiwezekuchukua interns zaidi ya 150 haina mantiki kwani Hospitali ya taifa ya Muhimbili kuna madaktari bingwa (specialist) wengi kuliko mahali pengine popote na ni suala la utendaji tu kuhakikisha kila daktari bingwa anasimamia interns wasiopungua watatu, hii inaifanya Muhimbili iwe na uwezo wa kuchukua interns wasiopungua mia tatu (300) kwa mda mmoja.

Katika upangwaji huu, Interns hawakupewa nafasi ya kusikilizwa hata wale walioonyesha nia ya kwenda kuendelea hospitali zingine kama vile Mbeya, hospitali ya Bugando au KCMC walikataliwa sababu "Serikali imeamua na haibadilishi" maneno ya Dr. Deogratius Mutasiwa (Mganga Mkuu wa Serikali) (ikumbukwe kuwa intern huwa anaomba ili kujiunga na hospitali na sio kupangiwa na wizara, upangaji huu umetunyima uhuru huo na kutuharibia mipangilio yetu ya mbele.

Pia hospitali zilizopewa interns wengi hazina madaktari bingwa wa kutosha kusimamia interns ili waweze kuwa na utaalamu unaotakiwa katika kuwahudumia wananchi.
Kwa mfano hospitali ya Amana kwa sasa ina madaktari bingwa 5 waliopo sasa hivi na interns waliokuwepo ni 38 ukiongeza walioongezewa ni 13 ambao jumla wangekuwa 51. Kwa maana hiyo uwiano kati ya daktari bingwa 1 kwa interns 10, huku baadhi ya idara kukiwa hakuna madaktari bingwa hawa mfano idara ya afya ya kina mama (obstetrics and gynaecology) kukiukwa kwa ‘internship guidelines for medical and dental practitioners of medical council of tanganyika 2009' Katika kifungu cha tano cha " supervision of internship" aya ya kwanza "during the internship period, the intern will be supervised by the specialist in-charge of the specialty together with other staffs in his department and by the hospital administrator".

Itambulike kuwa kwa upande wa interns wa maabara, sehemu walizopelekwa kuwa hakuna vifaa vinavyoweza kukidhi mahitaji ya interns hawa, pia wataalamu wa kuwasimamia wana elimu ya chini (diploma) kuliko interns (degree) wenyewe, vilevile hakuna specialties wanazo takiwa kupitia katika kipindi hiki cha internship kwa mfano ‘histology, biochemistry, haematology, parasitoloty and microbiology and immunology.

Aidha baadhi ya interns hata huko walikohamishiwa bado hawakuweza kufanya kazi kutokana na majibu waliyopewa na wakuu wa hospitali husika kuwa interns wamejaa na wengine kuambiwa hawana taarifa zao toka wizarani. Matatizo mengine ni pamoja na kutakiwa kufanya interview ili kuanza internship, mfano hospitali ya Agakhan.

• Vile vile taarifa alizotoa naibu waziri wa afya kwa vyombo vya habari tarehe 17/01/2012 kuwa sehemu nyingine hawakugoma/kushindwa kufanya kazi haikuwa sahihi kwani hospitali zilizohusika katika sakata hili ni pamoja na Bombo (siku 8), Temeke (siku 1), Dodoma (siku 5) na Mount Meru (siku 10). Na hawa hawakurudi kazini mara moja kama ilivyoelezwa. Na baada ya kulipwa posho zao, interns wa hospitali nyingine waliruhusiwa kuendelea na kazi bila mashariti yoyote.

• Kitendo kilichoitwa mgomo ambacho si sawa sababu interns hawakuweza kufika kazini sababu hawakuwa na fedha za kujikimu na taarifa ilitolewa na uongozi wetu kwenda kwa katibu mkuu na nakala kwa mkurugenzi tarehe 03/01/2012. Serikali pia ilikiri ucheleweshaji huo ila jambo la kushangaza tukapewa barua hiyo (kama viambatanisho vinavyo onyesha) kurudi wizarani ikisemekana tumevunja mkataba kwa "kugoma".
• Mkataba unaoongelewa kuvunjwa, una sehemu mbili; Sehemu ya intern na vipengele vyake na sehemu ya hospitali. Hospitali ndio ilikuwa ya kwanza kuvunja kwa kutokulipa kwa muda wote huo, na serikali ilikiri kucheleweshwa kwa malipo hayo.

KAULI YA WAZIRI WA AFYA.
Madaktari na watumishi wa Afya wamesikitishwa sana na kauli ya Waziri wa Afya Mhe. Dr. Hadji Mponda kwa kukana kuwa Interns sio madaktari ila ni wanafunzi wa Mwaka wa nne wa Udaktari, hii ni kuupotosha umma na udhalilishaji wa wataalamu na taaluma nzima ya utabibu. Kauli hii ilinukuliwa na baadhi ya vyombo vya Habari mfano kipindi Maalum cha ITV siku ya Jumatatu 09/01/2012. Na mpaka sasa hajafuta kauli hiyo.
Aidha kutowajibika kwake kumeendelea kuonekana hata kupotosha bunge tukufu la jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kutamka kuwa interns baada ya kulipwa hawakurudi kazini. Mafaili ya wagonjwa ya Tarehe 05/01/2012 ni ushahidi tosha
 
Uongozi wote wa wizara ya afya ukiondolewa, bila shaka madaktari watarudi kazini bila masharti yoyote.
hilo ni mojawapo,
ila linarank very low katika madai.
wataondoka, mgomo palepale.
 
Hahaha, wee DR. umepinda kisawasawa. Kumbe hadi Kizanaki kinapanda? Au ume-paste kutoka sehemu fulani?

Anyway, hiyo ilikuwa ni enzi ya Nyerere na sasa ni enzi ya Kikwete. Kuna member aliweka maneno mazuri sana jana na nimeona niyaweke kwenye sahihi yangu.

"Mwendo ni KINDUGAI NDUGAI tu, kila mtu atangulize tumbo, taifa baadaye" (Bumpkin Billionare wa JF).
Mwalimu Julius Kambarage aliwahi kusema katika moja ya hotba zake. Wazanaki wanasema hivi, Wazanaki wanasema hivi "UBUBISUBISU OBUWERE EKIRO KIRIMBURA" ikiwa na maana Mfichaficha maradhi kilio kitamfichua.
 
Definitely nakubaliana na wewe kwa asilimia 100, wabunge wanalala bungeni halafu wanalipana laki 2 kwa siku hala fu wanadharau watumishi wa kada nyingine kisa wao wameshikilia mpini.
 
nafatilia kikao cha muafaka cha siri kwa ukaribu zaidi naona ka wantaka kutushinda hivi.
 
Uongozi wote wa wizara ya afya ukiondolewa, bila shaka madaktari watarudi kazini bila masharti yoyote.

Huo ndiyo ukweli wenyewe,madai mengine yatakuwa mepesi kuzungumzika,naamini na kazini watarudi ila mimi nashangaa mioyo ya hawa viongozi wa wizara ya afya!!ni zaidi ya jiwe!!watu wanasema madaktari ni wauaji wakati hawa watu wameshindwa kujiuzuru,binafsi sina moyo wa aina hii,ningelikuwa mimi tayari ofisi nilishakabidhi,watu hawakutaki sasa unataka kumwongoza nani??
 
mimi ukinipa mshahra wa 2.5m sitaki kabisa posho...hivi jamani hadi maji marefu na lusinde wananipita mshahara!!!!this system is criminal

Heeeeeeee! kumbe lusinde naye ni debe tupu. Ila kweli jamani, huyu maji marefu mi naona hata mwenyewe haamini kama kweli shavu analokula ni kweli au anaota.
 
mimi ukinipa mshahra wa 2.5m sitaki kabisa posho...hivi jamani hadi maji marefu na lusinde wananipita mshahara!!!!this system is criminal
Yani umenifanya nicheke mwenyewe mpaka watu wananishangaa,kweli Tanzania kiboko Mganga wa kienyeji anampita Dr professional mshahara!hii kali
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom