SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 5,152
- 7,926
Sijui huu ni utaratibu wa wapi unaotumiwa na Simba kufanya vikao vya kila siku na wachezaji. Hauwezi kujua shida za mchezaji kwa utaratibu huu. Tukisema siasa imezidi pale Simba kuna watu hawatuelewi.
Kila mchezaji wa Simba ana manager wake anayejua kila issue ya mteja wake. Mimi nadhani klabu hasa kwa upande wa management na bodi ianzishe utaratibu mpya wa kuwasiliana na mamanager wa wachezaji kwenye masuala yote yanayohusiana na mchezaji. Kama kuna ahadi za posho ambazo zimechelewa kutekelezwa, mazungumzo yasifanyike kwa mdomo bali kwa maandishi kwenda kwa manager. Kama kuna issue zozote za malimbikizo ya mishahara, taarifa zote zipitie kwa maandishi kwa management ya mchezaji. Kama mchezaji ana malalamiko yoyote ukiacha yale ambayo ameyafikisha kwa benchi la ufundi nae inabidi ayapitishe kwa manager wake atakayefikisha kwa vyombo husika ndani au nje ya klabu. Kama kuna mapungufu au malalamiko ya jumla ya wachezaji mfano hali ya kambi, vifaa duni vya gym, nk. ni jukumu la captain wa timu kufikisha kwa viongozi. Hilo halihitaji vikao.
Wachezaji wa mpira hawana tofauti sana na wasanii wa muziki, hawajui kujieleza hasa kwenye masuala ya fedha, biashara au kisheria. Ukimzingua au akiona mbabaishaji atakufanyia tu vitimbwi kwa jinsi anavyojua yeye.
Wachezaji wakiwa uwanjani wanaonekana wana mawazo na hawana morali ya kucheza kwa sababu wana visirani vyao na hawana jinsi ya kuvifikisha kwa uongozi. Kwanza inaonyesha mazingira ya pale ukijifanya kulalamika tena mbele ya viongozi wote wanaona Aha tumempata mchawi wetu, huyu ndiyo anaongoza mgomo baridi.
Cha mwisho nadhani kuna mgawanyiko kati ya wachezaji wazawa na wageni na pia kuna wachezaji wanaopewa vipaumbele zaidi ya wengine hata katika malipo.