Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,467
- 40,973
Sisi Waafrika, na zaidi Watanzania, huenda ubinadamu wetu haujakamilika. Mataifa ya watu wenye akili za hali ya juu, wanajua kuwa uhai na usalama wa mtu ndiyo kipaumbele cha kwanza cha Serikali na jamii.
Sisi, unaweza kushuhudia pesa ya sherehe za mwenge zikawepo, pesa ya sherehe za CCM ikawepo, pesa ya posho ya viongozi wanaozurura bila sababu za msingi ikawepo, pesa ya kulipana posho wabunge wasiojadili lolote la maana ikawepo, pesa ya msururu wa misafara ya magari ya viongozi wakuu ikawepo, pesa ya kununulia magari ya kifahari kwa viongozi wa serikali ikawepo, lakini pesa ya kufanyia utafiti wa kujua chanzo cha tatizo la saratani kuwa kubwa sana sehemu mojawapo ya nchi yetu, ikawa haipo.
Tena hao wanaoteseka na kufa kwa saratani, ndiyo chamzo kikuu cha hiyo pesa yote wanayotumia hao wapanga matumizi ya pesa ya Serikali.
Tatizo la saratani kuwa kubwa sana Kanda ya Ziwa, inafahamika tangu muda mrefu. Serikali inaliongelea kama habari ya mpira wa simba na yanga, badala ya kuliona ni jambo linalotakiwa kuwekwa kwenye agenda za kipaumbele cha kwanza kwa sababu ni suala linalohusu uhai wa binadamu.
Yaani aheri watu waendelee kufa lakini porojo na tafrija za kutafuna pesa kupitia mambo mbalimbali yasiyo ya lazima, zisikosekane.
Yaani inashangaza kusikia kuwa Marekani wanafanya utafiti juu ya chanzo cha tatizo hili, lakini Serikali yetu ipo tu, na inaona ni kawaida!!
Wananchi tunataka kujua, tangu tatizo hili lifahamike, Serikali imefabya nini? Na matokeo take yamekuwa yapi. Wananchi tuamke, tukiendelea kulala usingizi kwa kufikiria wapo wanaopigania uhai wetu, tunajidanfanya.
Kama Serikali, tangu tatizo hili lifamike, haijafanya chochote, wananchi tuwatake waliotakiwa kuchukua hatua halafu hawakuchukua, wajiuzuru mara moja. Tunataka Serikali na watendaji wanaowajibika kikamilifu kwa maisha ya wananchi, na hasa uhai na usalama wao.