FACT: Tanzania ya Magufuli haina Industrial Strategy

FACT: Tanzania ya Magufuli haina Industrial Strategy

TROTSKY

Senior Member
Joined
Aug 30, 2016
Posts
134
Reaction score
159


Kama ipo ileteni hapa tuone iliandikwa na nani na how ambitious is it na je inaendana na hii karne tuliyopo au bado iko kwenye zama za stone age?

Nishatafuta sana hii kitu kwenye website za wizara na serikali sijaipata

This document is harder to find than ile ya muungano wa Tanganyika na Unguja
 
Wewe elewa tu kuwa Tanzania ya viwanda inakuja, na pia Tanzania ya Magufuli ni Tanzania ya viwanda.

Mambo ya strategy tuwaachie wazungu. Mifuko ya jamaa imezuia fao la kujitoa ili wajenge viwanda. Ni viwanda, viwanda, viwanda. Tunaweza kuweka viwanda kila kata kama shule za sekondari. Hapa Kazi Tu
 
Swali lako nila msingi. Lakini JF ya siku hizi siyo ile. Hivyo tegemea matusi tu.

Lakini niliwahi sikia mahala flani kwamba hawa jamaa wa buku saba wametafutiwa shamba maeneo ya Rufiji ili wakalime. Ngoja tusubiri labda ni kweli maana imagine they get paid Tsh 7k everyday, this is a misuse of public funds.
 
1 Nguvu za umeme unaendana na viwanda?
2 Wawekezaji au Serikali ndio itakayojenga viwanda?
Maoni yangu sioni kama kweli kuna dalili ya kujengwa viwanda lakini ilikuwa ni njia ya kupata kura wakati wa kampeni tu. Siasa inauza maneno mazuri kuliko hata mwanaume anavyo mtongoza mwanamke.
 
Hii yaani tena nasema hivi tanzania yangu ni ya maviwanda tu kila mahali


Lakini hata kufyatuana si vuwanda au
 
Mkakati wa viwanda uko katika nyaraka mbili: (1) Sera iliyopo sasa ya maendeleo ya viwanda (Strategic Industrial Development Policy - SIDP) iliyoanza kutumika 1996. Hii sera inasema viwanda vitajengwa na sekta binafsi na jukumu la serikali ni kuweka mazingira mazuri kwa maendeleo ya viwanda. Jambo la ajabu ni kwamba tangu sera hii ianze kutumika idadi ya viwanda imepungua kwa kiasi kikubwa. (2) Mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano, 2016/17-2020/21 (FYDP2), ambao umekuja na 'mkwara' wa kauli mbiu kwa Kimombo: "Nurturing Industrialization for Economic Transformation and Human Development". FYDP2 tayari imeanza 'kutekelezwa' lakini jambo la ajabu tena ni serikali kutokuwa na mkakati wa kuboresha na kuendeleza sekta ya kilimo ambayo ni mhimili muhimu wa maendeleo yoyote ya viwanda. Katika bajeti ya mwaka huu kwa mfano, fedha 'kiduchu' iliyotengwa kwa ajili ya maendeleo ya kilimo ni uthibitisho kuwa FYDP2 ni usanii mtupu.
 
Tatizo kubwa la hii serikali ya CCM ni kutokujikita kwenye vipaumbele vya maendeleo (kulingana na mipango iliyopo) hasa vile vya muda mrefu na muda wa kati (kama ilivyo FYDP2) na badala yake 'kuchomeka' miradi mikubwa ambayo haiko kwenye mipango kama 'elimu bure msingi na sekondari' na kuhamia Dodoma. Kwa namna hii hatutakwenda popote kimaendeleo!
 


Kama ipo ileteni hapa tuone iliandikwa na nani na how ambitious is it na je inaendana na hii karne tuliyopo au bado iko kwenye zama za stone age?

Nishatafuta sana hii kitu kwenye website za wizara na serikali sijaipata

This document is harder to find than ile ya muungano wa Tanganyika na Unguja
Kwani wewe hujaiona strategy no. 1 ya serikali ya awamu ya 5 ya JPM ya kuelekea kwenye TZ ya viwanda, namna wanavyojitahidi 'kulinyonga' fao la kujitoa kwenye mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa wafanyakazi ili pesa hizo zikajenge viwanda?!
 


Kama ipo ileteni hapa tuone iliandikwa na nani na how ambitious is it na je inaendana na hii karne tuliyopo au bado iko kwenye zama za stone age?

Nishatafuta sana hii kitu kwenye website za wizara na serikali sijaipata

This document is harder to find than ile ya muungano wa Tanganyika na Unguja
Sasa wewe Unataka strategy gani zaidi ya ile aliyotoa Mkulu ya kuwahimiza wa TZ wafyatue watoto wengi kwenye 'viwanda' vya kwenye kaya zao?!
 
Labda viwanda vya mikwara na kufoka
It is very true.

Hivyo vitakuwa viwanda vya kufikirika.......

Hivi TZ ambayo baada ya zaidi ya miaka 50 baada ya Uhuru, TZ yetu imeshindwa hata kuwa na kiwanda kimoja aidha cha toothpick, socks, handkerchief na underpants, ndiyo kweli katika kipindi cha miaka 5 ijayo ifanye 'muujiza' mkubwa wa kuwa na viwanda vikubwa vya nguo hadi kupiga marufuku uingizaji wote wa Nguo za mitumba na brand new clothes toka nje ya nchi?!

Hakika hii TZ yetu haiishagi vituko........
 
me sielewi aiseee nna hasira sana acha nkae kimya nsije nkaitwa mchochezi sina milioni 7
 
Mkuu, unaamka usiku wa manane badala ya kutafuta watoto wewe unamuwaza mwanaume mwenzako?
 
Back
Top Bottom