VIWANDA TRANS!!!!!
ulisha wahi panda gari kutoka unapo pajua kwenda usipo pajua???
Iko hivi.......
katika maisha kuna kipindi tunapanda usafiri either daladala, bus, ama bodaboda huku atujui tunako kwenda, ila tutokapo tunapajua vizuri tu!!!!
hufika mahala ukasikia kondakta anataja vituo, kwakuwa wewe hupajui unapokwenda basi unamuuliza jirani yako pembeni kwenye siti "hivi ni hapa ndo napo kwenda ama kushuka??? ndipo panaitwa ........." nayeye anakupa majibu "sijui kama ni hapa" labda tumuulize konda,"
konda naye yuko mbaaaali........
maana mlundikano wa watu kwenye gari unamfanya asifikike kiraisi!!! hata anapotaja vituo,..... sauti yake haifiki kwa haraka kwa abiria wake!!!
anapiga story huko mbele, mara apigane na makonda wenzake!!! mara afokeane na wanafunzi wasio na nauli za kutosha, mara abadilishe muziki kwa karimoti kake aliko kashika mkononi,
mara agombane na mama mwenye mikungu yake ya ndizi iliyopakizwa kwenye gari lake kwamba amelipia kidogo aongeze hela maaana mzigo mkubwa, wakati anapanda walisha kubaliana bei vizuri tu,
so yuko bizy na mambo mengine meeengi kuliko kujua abairia wake wanapaswa kushuka wapi!!!
mnaendaaaaaaa mpaka mwisho....... wengi mnapitishwa vituo, maaana dereva anakanyaga mafuta na yeye ndio anaamini anajua njia na hakuna mwingine!!!
inafika mahala dereva na konda wanaaza kulaumiana mbona ulikua unambii kusimama,??? hii nikutokana na wingi wa abiria waliopitishwa vituo,!!!! konda anakasirika abiria wanakasirika, dereva anashuka kwenye gari anaendakukaa pembeni anawatazama tu!!!
hii inakugharim wewe abiria kutafuta usafiri wa kukurudisha kwenye kituo ulichopitilizwa!!!!
twendeni tu!!! tukipitilizwa tutarudi kwa miguuu!!! nihayo kwa leo wapendwa wangu!!!!