Facebook wamefeli kuhusu tukio la Ufaransa

Facebook wamefeli kuhusu tukio la Ufaransa

Africa is for Africans.

ANawashangaa sana kila siku watu kama Maarim Seif eti anakimbilia nje kuomba wazungu wamsaidie, yaani waafrika kweli tuna matatizo ya akiri ..hivi unaweza ukahisi wazungu wanakupenda saaaana? nawashangaa sana watu wa hivi kwakweli
 
1447686002254.jpg
Kuna siku Mark aliweka bendera ya Rangi za Upinde wa mvua na watu wengine wakasapot kwa kuweka hizo pinde bila kujua zilikuwa zinamaanisha nini. Ilikuwa ni FACEBOOK CELEBRATION PRIDE.
 
Halafu kuna mapimbi kibao yanayotetea huu upuuzi ndo yameweka profile display huko fb, yanaonekana yameguswa kweli na tukio la ufaransa kuliko hata garissa
😡😡😡😡😡😡
 
Fb ufanya kazi kutokana nchi usika uwezekano walioweka ni wafaransa hapa ukiweka pc ya utupu aingii nchi ingine inaingia
 
Mtandao wa Facebook una users karibuni billion moja na million 400 na kati ya hao Users toka Africa ni wengi kiasi cha robo nzima.

Hivi jana yametokea mashambulizi ya kigaidi nchini Ufaransa na katika kuonyesha solidarity Facebook wameweka special icon ya mtu kuweka bendera ya Ufaransa (transparent) plus picha yako ili iwe profile picture.

Utaratibu huu ni mzuri ukizingatia unaonyesha solidarity katika janga lililowakumba ndugu zetu. Lakin April 2 2015 lilitokea shambulizi lilichukua maisha ya watu wengi zaid kuliko hata hili huko Garissa Kenya kana kwamba ni tukio la kawaida hakukuwa na bendera ya Kenya wala special privilledge kwa watu wa Kenya.

Hapa nadiriki kusema Facebook wanaonyesha kulemewa na itikadi za ukanda, ubaguzi, kutokua na usawa ilhali Wakenya ni moja ya mataifa makubwa yenye watumiaji wengi Facebook Africa baada ya South Africa na Nigeria of which ni wachangiaji wakubwa wa pato la Facebook.

Hii ndio picture halisi ya hali ilivyo kati ya mataifa ya Ulaya na Africa ingawa wanajitahidi sana kupaint ionekane wako concerned na kuna concern kubwa lakin Genocide za Rwanda na Burundi, vita za Wenyewe kwa wenyewe na vifo vya wapigania Uhuru kama Lumumba na Nkurhuma ni ushahidi tosha kuwa mikono na fikra zao hazina huruma wala concern dhidi ya waafrika.

Eeee kumbe hata Facebook Ina "Ukanda"😄😄😄😄
 
Sioni tatizo la Facebook.

Waafrika tuanze na kujithamini sisi wenyewe kwanza kwa kuheshimiana na kutendeana vyema.
 
Halafu kuna mapimbi kibao yanayotetea huu upuuzi ndo yameweka profile display huko fb, yanaonekana yameguswa kweli na tukio la ufaransa kuliko hata garissa
😡😡😡😡😡😡

garisa mbali wangelilia hawa wa kipindupindu maana idadi inaanza kukarbia wafaransa
 
Kweli kabisa mkuu, me ndio maana sijafanya kabisa kuweka france profile japo very sorry France, lakini pia Palestine, Syria pia wanauawa kila siku lakini hawajafanya kitu kama hicho hata siku moja
 
uache kulalamika vitu vya kindorobo. hili ndio shambulio la kwanza facebook kuweka huo utaratibu. inawezekana kabla walikuwa hawajagundua njia rahisi yakuwafanya watu wawe aware na habari kama hizo. ikitokea tena wakashindwa ndio uje ulalamike
 
Una dyslexia wewe! Wacha wazungu wajaliane, mmekatazwa kutumia mitandao yenu mpk mtegemee vya wazungu?
 
Wakati mwingine ndo maana nawafagilia wachina. Wana facebook yao, twitter yao, Whatsapp yao, Instagram yao...halafu wakaziblock hizi za kimarekani zote. Huo ndo uzalendo
 
Back
Top Bottom