Facebook wamefeli kuhusu tukio la Ufaransa

Facebook wamefeli kuhusu tukio la Ufaransa

Hiyo feature ilikuwa haipo FB wakati huo, nadhani imranza juzi juzi na haki za magay ndo ikaja Rainbow flag.
 
First and foremost hiyo feature haikuwepo kipindi hicho. Pili, Ni option kuweka bendera ya France sio lazima l, FB haimbadilishii mtu yeyote profile pic yake.

Huwezi kumchagulia mtu msiba wa kulia au kutokulia, kuna wengine wanaguswa zaidi na ugaidi uliotokea France kuliko ule wa Kenya au nchi zingine hivyo wanaonyesha solidarity zao kwa namna moja au nyingine kwa matukio yanayowagusa zaidi.
 
Kuwa na Facebook yetu ya Kiafrica zaidi ndio tutaweza otherwise tutabakia kupiga kelele tu na hakutakuwa na majibu.
 
Waafrika wapi "Wanaounga mkono Wazungu au Waarabu"??

Mkuu wapo wengi tu,kwani Mara ngapi tunashuhudia Serikali yetu inamkandamiza Mzawa lkn inambeba Mzungu au Mwarabu??,Kipindi cha Uongozi wa Mhe.Mkapa Madaktari wa Muhimbili waligoma kwasababu Serikali ili muajiri Mkurugenzi mzungu na kumlipa mshahara mnono wakati elimu yake ni ya kawaida sana huku wao Madaktari wakiambulia mishahara midogo ya kutosha kununulia bagia;Nenda kwenye Migodi ya madini uone jinsi Wazawa wanavyonyanyaswa na Serikali yao kwa nia ya kumlinda mzungu,hiyo ni Mifano michache tu ya baadhi ya Waafrika wenzetu wanaowaunga Mkono hawa Watu weupe.
 
Jaman mnaobeza huo mtandao mkae mfaham Tu kuwa mitandao n vile unavotumia facebook n nzuri hasa ukiitumia ipasavo
 
Kwahiyo unatakaje, wao wamekaa darasani na kubuni facebook, kwenu Tanzania mmebuni nini cha maana
Wamebuni mbinu za kuiba kura na kujitangazia matokeo ya uongo. Nchi ya Walaghai kamwe haitaendeleo.
 
Hata mimi nimeshangazwa na outcry hii, wakati juzi kati Ndege yaUrusi ililipuliwa na watu zzaidi ya 200 ndani hatukuona maombolezo ya Facebook!
 
Hata mimi nimeshangazwa na outcry hii, wakati juzi kati Ndege yaUrusi ililipuliwa na watu zzaidi ya 200 ndani hatukuona maombolezo ya Facebook!

mkuu watakuwa ndo wameanza hii huduma,si unajua kilakitu kina mwanzo???now watakuwa hata wachimba migodi wa nyamongo wakikwama na kufia huko itakuepo hii maombolezo through facebook
 
Back
Top Bottom