Expatriates hawana sifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Expatriates hawana sifa

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Bw. Ufahamu, May 17, 2010.

 1. B

  Bw. Ufahamu Member

  #1
  May 17, 2010
  Joined: Apr 23, 2010
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wageni wanaoletwa nchini kufanya kazi kama expatriates ni mbumbumbu wa kutupwa. Eti utamwona mhasibu katoka india hajui hata kazi ya uhasibu huku Cv yake inaonesha ana masters. Kunani huku!! Ninavyoona hata baadaye wauza vitumbua watatoka nje km expats!!!!!!! :mad2:
   
 2. c

  chibhitoke Member

  #2
  Jun 1, 2010
  Joined: Jun 1, 2010
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bwana Ufahamu,
  Ni aibu kubwa sana katika nchi hii/ kuna taasisi moja inaitwa BRAC inatoa mikopo yenyeewe kila Branch kuna wa bangladesh kama wanne hivi wakifanya kazi ambazo watotot wetu wangeweza kabisa kuzifanya. Lazima serikali ilinde ajira za watanzania/ ndio tunahitaji wataalamu lakini sio sampuli hii ya BRAC. Sasa jinsi wanavyofoji vibali vya kazi utashangaa ni dau tu tena kwa dola, .Inasemekana Pasi zinachukuliwa na kupelekwa Airport kama vile jamaa walisafiri wakati wako hapa hapa Mbezi Beach/ aibu aibu kubwa
   
 3. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #3
  Jun 1, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,365
  Likes Received: 6,996
  Trophy Points: 280
  Tanzania ni shida mno ku;linda soko la ajira, ni tamu mno idara ya uhamiaji haifanyi kazi kabisa
   
 4. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #4
  Jun 2, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Nikiwa rais nitabadilisha sheria za ajira kuhakikisha kuwa ni vigumu kumpa ajira raia wa nje (hata wa Kenya) kwa kazi ambazo zinaweza kufanywa na watanzania.
   
 5. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #5
  Jun 2, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,173
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo case ya wahasibu, ina maana hatuna wahasibu nchini mpaka tunaleta wahasibu kutoka India?
   
 6. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #6
  Jun 2, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  The same old story za shamba la bibi..

  Watu wanaingia kuvuna na kutoka bila taarifa, BIBI HANA HABARI.
   
 7. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #7
  Jun 2, 2010
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,034
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kila mahali siku hizi wamejaa wageni. Ukifika Precision Air, utakuta mpaka cabin crew/Secretary/Operations na wengine wengi tu, wanatoka Kenya, Mafundi ndio usiseme, Mishahara wanayolipwa ni zaidi ya mara 3 ya wazawa. Wakati watu wenye sifa zaidi ya hizo tunao hapa hapa. Itafika wakati, tutachukua hatua mikononi kama South Africa tulinde wenyewe soko la ajira zetu. INAUMIZA SANA.
   
 8. HeartBreak

  HeartBreak JF-Expert Member

  #8
  Jun 2, 2010
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 346
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  kule zanzibar naona tatizo hili ni kama kitu cha kawaida kwenye mahoteli yote ya zanzibar,wageni wengi hawana hata sifa,shule hawajaenda kama ukiangalia hoteli kubwa kama zamani zanzibar kempinski ilikuwa na wageni kila idara wote hawana sifa ya kufanya kazi nchini hii ni aibu,tena wakenya,wahindi na wazungu hapo ndio kwao.....zanzibar inanuka kwa rushwa hakuna lolote kwenye bodi ya utalii,mungu atawasaidia wazanzibar kuondokana na serikali mbovu isiyojali wazawa wake.
   
 9. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #9
  Jun 2, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Haianzi na ajira kama tunavyodhania... inaanzia mbali zaidi.
  1.Mnakaribisha "wawekezaji" kila nyanja na hao huamua waajiri watu gani. Uhamiaji nako kama masharti yametimizwa basi hakuna tatizo kutoa vibali husika.

  • Chukulia BRAC - hii ni taasis iliyotoka huko Bangladesh na inapigiwa mfano dunia nzima kwa kuweza kutoa mikopo midogomidogo - si ajabu wakaweza kujenga hoja nzuri kwanini walete wahasibu wao.
  • Ukija Precision Air - watanzania wenzetu waliopewa dhamana kusimamia maslahi ya waTz, wao ndio mstari wa mbele kupiga vita mashirika ya watanzania kama ATC, Swissport etc na kuipa Presicion air ( mdau mkubwa akiwa Kenya Airways) kuchukua biashara za uchukuzi wa anga.Cha kushangaza wakati yote yanatokea Watazania wanashangilia utadhani wako kwenye mashindano ya kombe la dunia!
  • Hapo bado hatujaangalia taasis nyingine na mashirika kama Care, Oxfam,World Vision etc ambayo yameajiri wageni hata pale pasipostahili kwenye kazi za kusaidia jamii na kuwanyima wasomi wetu ajira!
  • Biashara nazo zimejazwa na wageni - hadi kuna wamachinga wa kichina wametapakaa kila mahali!
  Ifike mahali watanzania kwa ujumla wetu tuweze kuchambua na kuona ni kipi kina maslahi kwa Taifa na kukisimamia badala ya kuoneana kijicho kwa vile Taasis fulani ina watanzania wenzetu wanaifaidi sana basi tuwapige vita.
  Kumbuka - UKIRUSHA UCHAFU KWENYE FENI UTAKURUDIA MWENYEWE!
   
 10. Eng. SALUFU CA

  Eng. SALUFU CA Senior Member

  #10
  Jun 2, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 146
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa hawa si ndio wawekezaji tunaowataka tufanyeje? Kwani hamuwaoni wach... wanavyouza maua bandia pale kariakoo kwani Mluguru wa MG hawezi hii? Mimi nashangaa watu wanakalia viti tu hawawezi kuvitumia hebu tuanze kuwango'oa wazee wote ambao tangu uhuru wa nchi hii ni viongozi na hawana jipya, hebu pisheni dame mpya ichape kazi jamani, utajiri tulionao hatustahili kuwa hivi tulivyo!!!!!!!!!!!!
   
 11. Da Womanizer

  Da Womanizer JF-Expert Member

  #11
  Jun 2, 2010
  Joined: May 24, 2010
  Messages: 1,562
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Tatizo pia Wabongo kazi yenu kubwa ni kusema tuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu NO ACTION na mtu akijaribu kufanya chochote anaonekana kama kichaa fulani vile. What I am trying to say is either stop complaining and act or just shut up and mind your own business.
   
 12. Sokwe Mjanja

  Sokwe Mjanja JF-Expert Member

  #12
  Jun 12, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kula tano ndugu yangu.......
   
 13. Drifter

  Drifter JF-Expert Member

  #13
  Jun 12, 2010
  Joined: Jan 4, 2010
  Messages: 1,968
  Likes Received: 668
  Trophy Points: 280
  Tatizo letu Watanzania na Serikali yetu ni kuwa upeo wetu wa maendeleo umeishia kwenye kiwango cha mitaa yetu - competition at community (local) level. Tuko tayari kusaidia wageni kuhujumu uchumi wetu almuradi tuambulie makombo yatakayotuwezesha kuzidiana mitaani kwa vinyumba, vigari, vifenicha, n.k. na matanuzi kwenye majumba ya starehe. We do not see the big picture at all. Nenda nchi za wenzetu hata zile masikini kama Ethiopia, huoni ujinga kama tulio nao. Mgeni habebwi kiasi hicho. Na tunavyoendelea kuiendekeza Serikali isiyo makini katika masuala ya uzalendo, ujinga huu utaendelea hadi tutakapokuta wenye nchi ni wengine kabisa; sio "sisi" tunaojifikiria ni Watanzania ilhali hata kupeana vitambulisho vya utaifa vya uhakika imeshindikana.
   
 14. B

  Bw. Ufahamu Member

  #14
  Jun 14, 2010
  Joined: Apr 23, 2010
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  NINACHOONA NI KUWA HAKUNA WATU WENYE UCHUNGU NA HII NCHI. Unapomwajiri mgeni na wenyeji wapo, wenye sifa zote, mimi sipati picha, inamaana wabongo hawaaminiki, yaani ni matapeli au. Waangalie wachina walivyojaa, hata watoto wa kichina + kitanzania wapo sasa hivi mitaa ya buguruni etc. TUANDMANE!!!!!!!
   
 15. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #15
  Jun 14, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Kwenda wapi??

  Hii kitu inaitwa Rushwa, Mlungula, Etc... Inasababisha hii shida

  Kampuni zinafunguliwa feki za wawekezaji wa maua na ndala pale Kariakoo, then anaajiri jamaa zake kama 20hivi, documents zao zinapelekwa na M-TZ pale Wizara ya Kazi (Labour Dept), pale jamaa anahongwa hela anapitisha document, then ikitoka hapo inaenda Immigration, nako wanahonga wanapewa work permit, imagine Country Director ambaye no Form 4 leaver (Kenya) na hana qualification nyingine... wanaishi hapa nchini hata miaka 10, na Labour pamoja na Immigration wana-renew tu permit zao... ni aibu, then na wao wanaleta ndugu zao....

  Dah, inaboa sana
   
 16. Muthaisu

  Muthaisu Member

  #16
  Jun 14, 2010
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 64
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  my brathas pleeeeeeeeeeeeeease hii shida haijaletwa na wakenya huko mbongo! ni serikali ya bongo ndio shida , kenya hii shida ilikuwa sometimes back but now the asians waatolewa na wakenya kila kuchao infact wengi wao wanaend canada sana coz of that....no place in kenya utapata wamedominate even though there are still some but by 2030 i think kenya will revert back to the owners..............when i was a first year i college a mhindi friend told me in kenya you pple own the flag ( a piece of coloured cloth!) but we own the economy! ( all the money) I felt stung to the core:mad: as of now most of the businesses are being run by natives. nowadays kenyans rarely wait to be employed through some programmes za government and the common mwanainchi watu ni biashara....travel anywhere on the earth and if you miss a nigerian you wont miss a Kenyan looking for opportunities! If I were to advice the government of TZ, then the would empower mwanainchi first and the rest will follow ...can you imagine how many licenses you require to a start a business in TZ as a local? how much you have to pay? how much time you have to waste running form officec to another for the same? Somebody spoke of english as an impediment to many Tanzanian brothers/sisters but look at s.korea they have their own language and economy to boot closer home botswana! By the way Kenyans went there in droves build the economy and some became nationals ...so u dont have to worry about us! Cheers guys!
   
 17. B

  Bw. Ufahamu Member

  #17
  Jun 14, 2010
  Joined: Apr 23, 2010
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Basi tutakapoungana nchi za africa mashariki, watanzania wengi wanaweza kupoteza hata hizo kazi walizo nazo. Wakenya watakubali kuwa cheap labour mwanzoni ili kumeza nafasi zote, hafu wengi tunaenda kuchunga ng'ombe(monduli) au kulima mbamia (tanga). Mungu atusaidie!
   
 18. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #18
  Jun 14, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,392
  Likes Received: 81,412
  Trophy Points: 280
  Niliwahi kukutana nao hawa wengi sana toka Sweden na Denmark (MaTX) kwao walikuwa ni unemployed wakiletwa kwetu kwa njia ya misaada na kulipwa mishahara na marupurupu makubwa pamoja na kutojua lolote katika fani iliyowaingiza Bongo. Wote niliokutana nao walikuwa hawataki kurudi makwao walipokuwa wanamaliza mikataba yao ya miaka miwili na waliruhusiwa kurenew mara moja, walikuwa wanaishi maisha ya raha sana. Wengine waliangusha hata machozi waliokuwa wanarudi kwao. Kuna haja ya kuwa na chombo cha kutathmini hawa MaTX wanaoingia Bongo kama kweli wana sifa zinazoonyeshwa katika CVs, hata kwa kuwapa mitihani kabla ya kuruhusu waajiriwe, vinginevyo watakuwa wanaajiriwa "wataalam" wasiokuwa na sifa zozote wakati Wabongo wanaendelea kusaga lami.
   
 19. E

  Edo JF-Expert Member

  #19
  Jun 14, 2010
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 728
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Mimi naunga mkono yote yalosemwa hapo juu, ila nakumbusha kuwa "SIO SIFA ZINAZOFANYA KAZI". Na hili ndilo tatizo letu, tunataka nafasi kwa sababu tuna "sifa", wakati kazi zenyewe kufanya kila siku ni "excuses tu". Hivi unadhani nani yuko tayari kumlipa mtu mwenye sifa asiyefanya kazi? Tubadilike, halafu utaona kama ataagizwa mtu nje !!!!
   
 20. M

  Mundu JF-Expert Member

  #20
  Jun 14, 2010
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Wenzako wanasema, ma expatriate wengi hawajui kazi walizoletwa kufanya!! Kwahiyo, hata wakijipinda vipi, output ni sifuri! hapo ndipo penye hoja na mjadala ndugu.
   
Loading...