Exclusive: Ikulu hawataki MNF ijenge "twin towers" karibu yao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Exclusive: Ikulu hawataki MNF ijenge "twin towers" karibu yao

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jun 1, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jun 1, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Habari nilizonazo ni kwamba MNF (Mwalimu Nyerere Foundation) walitaka kujenga jengo la ghorofa 14 na 20 twin towers kama kitegauchumi kitakachoiwezesha taasisi kujiendesha yenyewe bila kutegemea michango ambayo kwa sasa haipatikani toka kwa mtu yoyote yule. Jengo hilo ilikuwa lianze kujengwa tangu mwaka jana lakini cha kusikitisha ni kwamba Wachina CRJE ambao ndio wajenzi walipotaka wapate building permit wajenge Halmashauri ya Jiji Ilala wakawaambia kwamba hawawezi kutoa building permit kwa sababu eneo hilo halipaswi kujengwa majengo yanayozidi gorofa 6 au tano sikumbuki vizuri.

  Wakasema kwamba maagizo hayo yametoka kwenye kikao kilichofanyika Ikulu. Lakini ukiangalia katika eneo ambalo linadaiwa kwamba ni Security zone ya Ikulu yapo majengo mengine ambayo ni marefu na moja linaendelea kujengwa as we speak lina gorofa zaidi ya 20 pale karibu na Ocean Road.

  Taasisi wamejaribu kupata waiver kwa kuwa ni mradi uliobuniwa na Baba wa Taifa mwenyewe wakati akiwa Mwenyekiti Mwanzalishi wa Taasisi. Ikulu imeziba masikio. wanadai Taasisi wapewe eneo jingine. Kama ni kupewa eneo jingine lazima liwe kwenye central area ili kuweza kupata wateja wauhakika kama ilivyodhamiriwa ili kuweza kurejesha fedha za Wachina na wabia wengine kama ADB, World Bank etc waliojitolea kuchangia ujenzi huo.

  Ni wazi kwamba Ikulu wanakataa makusudi maana hakuna sababu yoyote ya kushindwa kuruhusu jengo linalobeba jina la Baba wa Taifa kujengwa katika eneo hilo kwa kuwa yapo majengo mengine marefu zaidi.

  Vyanzo vya ndani vinasema watu wa Ikulu wanaogopa sana kuipa ujiko taasisi hiyo hasa kutokana na mwamko unaoendelea taratibu wa mawazo na fikra za Mwalimu kuhusu Taifa na hasa baadhi ya watu mashuhuri ambao sasa hawaoni tatizo kujipanga na fikra hizo. Lakini nyuma ya yote ni hofu kuwa yawezekana wakuu wa sasa wa MNF wanahusiana na CCJ na kama taasisi ikiweza kujijenga namna hiyo inaweza kuwa huru kweli na tishio hasa ikiwa karibu hivyo na Ikulu.

  Hivyo, sitoshangaa endapo taasisi wakajikuta wanahamishiwa pembezoni mwa jiji...
   
 2. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #2
  Jun 1, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  this is serious!
  tatizo HASA HASA NI NINI?

  -i mean hao CCJ wamekuwa mwiba kiasi hicho?
  -au tuseme hao CCM hawana confidence kiasi hicho?
  -au wameona ile mbinu ya ''magumashi kwenye masanduku ya kura'' haita work this tym around?
   
 3. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #3
  Jun 1, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Lakini MKJJ,

  Fikra za Mwl Nyerere si zilikuwa kuendeleza Dodoma? Au mwishowe alibadili mawazo?

  Kujenga ghorofa kama hilo katikati ya Dar ni kuchangia tatizo liliopo.

  Mimi napendekeza wapeleke 'maendeleo' Dodoma, wakawekeze huko!!
   
 4. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #4
  Jun 1, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  jaribu kurejea hoja ya ''AZMA'' ya huo mjengo....
  SIO KUENDELEZA DODOMA BANA...
  huo mjengo is one thing,and DODOMA is another cup of tea
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Jun 1, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Good thread lakini kama kawa hukufika mbali ukaweka sisije!!!

  Mwanakijiji ukweli ni kwamba kuna hilo tatizo la security zote na ni bahati mbaya baadhi ya majengo yalipenya hiyo porous vetting syste yetu na kuweza kuendelea, mfano ni hilo pembeni ya nyumba za "watumishi" karibu na hospitali

  there are two ways to deal with this matter positively, bila kulialia kama ambavyo tumeona viongozi wa CCJ wakifanya [nasema hivi kwasababu CCJ inakua maarufu zaidi kwa kulalama kuliko kupata mbinu mbadala za kuachieve wanachotaka

  • kwanza wajenge hizo ghorofa sita kama wanavyoweza kupewa hiyo hati
  • pili wauze hilo eneo wajenge nyingine elsewhere kwenye kuruhsiwa, maeneo yama ya mkapa tower, exim tower au hata ali hassan mwinyi road

  kwani nani alisema lazima wawe karibu na ikulu?? mji wenyewe uko congested, barabara hakuna [hata mtu akiachia hewa chafu - inachukua masaa hewa ku-clear], sasa kwanini basi nao wasingeenda hata kigamboni, karibu na chuo cha mwalimu nyerere kutafuta eneo na kuweka hicho kitega uchumi??
   
 6. Katikomile

  Katikomile JF-Expert Member

  #6
  Jun 1, 2010
  Joined: Jul 12, 2007
  Messages: 473
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Mamaaaaaaaaaaaaaaa1 sad news mwanakijiji!
   
 7. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #7
  Jun 1, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Injinia ana point muhimu sana, hasa kama unakumbuka "zidumu fikra sahihi za mwenyeheri"!!!
   
 8. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #8
  Jun 1, 2010
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,639
  Likes Received: 2,872
  Trophy Points: 280
  Jambo likiongelewa sana huwa ninakuwa na wasiwasi kwamba ni la ukweli. Si mara ya kwanza kwa JB kuhusishwa na CCJ. Time will tell!
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Jun 1, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Je majengo yote yaliyoko Dar ya vitega uchumi yahamishiwe Dodoma au ni hili la MNF tu? Au mnapendekeza kuwa watu wasiwekeze tena Dar kwani tayari kumeshajazana au ni MNF ndio wataongeza kisichowezekana kuwepo? Hivi, ingekuwa taasisi ya kigeni ungeweza kusema security issue.. taasisi ya Mwalimu inatishia usalama wa Ikulu? really! Kwani walioenda kumtumia mkapa kuvunja sheria na waliopandikiza watu wao kwenye Ikulu ya JK leo hii walivunja wapi ili waingie? Usalama wa Ikulu hautishiwi na majengo!
   
 10. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #10
  Jun 1, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  hawa sisijei hawa WAMEKUWA THREAT kwenye chama cha de-novo
  hahahahahaha!
   
 11. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #11
  Jun 1, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  hivo hivo!
   
 12. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #12
  Jun 1, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  'Azma' haijatengenezwa kwa sementi useme haibadiliki.

  Kama haiwezekani ( na kweli haiwezekani, si tu kwa ajili ya usalama wa Ikulu, pia kwa sababu nilizokwisha taja kabla) wabadilishe hiyo azma!
   
 13. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #13
  Jun 1, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  you are very right MMM, tatizo sasa wao wameona hivyo na dawa si kupiga mbinja bali kuangalia mbadala... msipoangalia mtaishia kuwa kama mtikila ila mtamzidi kidogo kwenye kulialia!!!

  WHERE IS GT WHEN YOU NEED HIM?

  nothing personal against CCJ but too much complaining is linked to certain psychotic disorders... KUMBUKA NYERERE ALIWAHI KUELEZEA JINSI WALIVYO-DEFY SOME EXPECTATIONS ZA WABAYA WAO KWA KUFANYA WASICHOTEGEMEA... TODAY IF MNF WAKIAMUA KUJENGA KWINGINE BASI HAWATANYIMWA HIYO PERMIT

  TRY IT
   
 14. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #14
  Jun 1, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Kwani fikra za kuendelea kutumia hii IKULU ya sasa bado zinalindwa kihivyo?. Mbona kama TWIN TOWERS ni eneo la karibu zaidi ukiacha hilo la Ocean Road?. Kwa nini Wasihamishe IKULU kupisha Uwwekezaji wa maendeleo ya Nchi?. Usalama uko wapi ikuwa hapa ofisi za shuhuli binafsi kama za WAMA zilishawahi kuruhusiwa kufanyia mambo humo humo IKULU?.
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Jun 1, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  De Novo.. CCJ haihusiani na ujenzi wa MNF wala MNF haihusiani na CCJ. NI watu wengine ndio wenye hofu hizo. Ninachozungumzia hapa ni MNF ambayo ni taasisi ambayo Nyerere mwenyewe aliianzisha na toka wakati huo alikuwa ameshapata na hilo eneo.. sasa kwa nini leo wahamishwe? Kisa CCJ?

  Hakuna mtu anayelia lia kuhusu CCJ ila kama kudai haki na usawa ni kulia lia basi tutalia sana kwani hakuna aibu kulia ukidai haki yako. Unataka tukae tu kimya na kukubali kwa sababu "serikali imesema". Yaani serikali ije kutusukumiza halafu tukubali kusukumwa kwa sababu tukilalamika tutakuwa tunalia lia. Haya ndiyo mawazo yamewafanya watanzania kuwa wanasukumwa sukumwa na serikali yao.

  kwenye CCJ mstari umeshachorwa hatuuvuki..
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #16
  Jun 1, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280

  Majengo yaliyopo na mengine yanayojengwa yasitishwe au ni hii MNF ndiyo inatakiwa kubadilisha azma yake?
   
 17. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #17
  Jun 1, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  As long as Kikwete ni rais Ikulu na as long as Salim Ahmed Salim na Joseph Butiku wako MNF kibali hakitatolewa.
   
 18. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #18
  Jun 1, 2010
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,639
  Likes Received: 2,872
  Trophy Points: 280
  Juzi juzi kuna kichaa aliingia Ikulu. Hivi alipitapitaje pale getini?
   
 19. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #19
  Jun 1, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Kwa Point ya usalama hapa IKULU wanasababu ambazo kwa mtu yeyote rational atakubali kuwa ni risk sana kwa Ikulu kuzunguukwa na majengo ya kibiashara yanayoizi urefu IKULU yenyewe, yaani mtu anaweza kuwa juu ya ghorofa ya 10 akaona what is taking placing on the ground of The State House.

  But Ili IKULU ioneshe kuwa hoja yao ina nguvu walitakiwa ama kubomoa au kusimamisha ujenzi wa majengo yote yanayozidi ghorofa 6 katika perimeter ambayo wao wanaiona ni security zone. Vinginevyo watakuwa wanaruhusu Politics kuchukua mkondo wake na kwa kuwa hili halijafanyika basi inanilazimu kuamini hoja ya Mkjj ina ukweli
   
 20. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #20
  Jun 1, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Yaani hujanielewa MKKJ, mimi sipo dhidi ya MNF!! Ninachosema ni kuwa, kama wanazibiwa (au wanaona kuwa wanazibiwa) basi wakawekeze kwingine, Tanzania si moja?

  Kama kuna majengo mengine yanayojengwa na hayafuati utaratibu huo wa 'ghorofa 6 mwisho', basi ndiyo, na yenyewe yasitishwe!!
   
Loading...