Exclusive: Canada Pulls back!

Tayari tuna wabunge wana JF i.e Dr. Slaa, Zitto.

Siongelei wabunge wa sasa, wala ambao wamekuwa members wa JF baada ya kuwa wabunge, naongelea mwanachama wa JF wa sasa hivi ambaye si mbunge aende kuwa mbunge.
 
Siongelei wabunge wa sasa, wala ambao wamekuwa members wa JF baada ya kuwa wabunge, naongelea mwanachama wa JF wa sasa hivi ambaye si mbunge aende kuwa mbunge.

na bado unazungumzia mmoja tu kama ndio lengo?
 
Siongelei wabunge wa sasa, wala ambao wamekuwa members wa JF baada ya kuwa wabunge, naongelea mwanachama wa JF wa sasa hivi ambaye si mbunge aende kuwa mbunge.

Pundit pls....mbona unajitoa?...Mtanzania ni haki yako hio mkuu
 
Hii sasa ni one down two to go, Je wabunge wetu watapitisha mapendekezo ya kamati teule ya madini? kwa sababu ishu ya hawa jamaa walikuwa wanalobby isipitishwe!

Huo ndio wasiwasi wangu...sipendi kuwa pessimistic...lakini tujiulize labda hawa jamaa wamesha seal deal?....Tuombe Mungu isiwe hivyo
 
Date::7/17/2008
Balozi wa Canada adaiwa kushawishi wabunge kuikataa ripoti ya madini
Na Julius Samuel, Dodoma
Mwananchi

BALOZI wa Canada nchini, Janet Siddall, yupo mjini hapa kuwashawishi wabunge ili wakatae mapendekezo ya ya ripoti ya Kamati ya Madini kwa kile anachodai kwamba yakipita yatawakimbiza wawekezaji wa sekta hiyo.

Habari zilizopatikana mjini hapa jana na kuthibitishwa na baadhi ya wabunge, Balozi huyo alianza kukutana na wabunge mbalimbali wenye ushawishi mkubwa na wale wanaotoka maeneo ya yenye madini ili kuwaeleza madhara ya kupitishwa kwa ripoti hiyo.

Kwa mujibu wa wabunge hao, Balozi huyo anasema kama ripoti hiyo ikipitishwa itakuwa na madhara makubwa kwa wawekezaji na hivyo watashindwa kuendesha shughuli zao hali itakayowalazimu kufunga shughuli zao nchini.

Balozi huyo aliwaomba wabunge hao waishauri serikali ikutane na makampuni ya madini, ili wajadiliane kuhusu kodi watakazolipa kwenye halmashauri.

Miongoni mwa kodi mpya zinazopendekezwa kwenye ripoti ya kamati hiyo ambayo habari zinasema kwamba imekwisha kupata baraka za Baraza la Mawaziri, ni ongezeko la kodi inayolipwa na makampuni hayo kwa halmashauri kutoka Sh200 milioni kwa mwaka hadi asilimia 20 ya mapato ya madini.

Jana mchana Balozi huyo alikutana na wabunge wa Chadema, mbunge wa UDP na baadaye wabunge wa CCM, na ajenda yake ikiwa ni kuwashawishi ama kuibadili ripoti hiyo au kuikataa kabisa kwa kisingizo kuwa itaathiri sekta ya madini kiasi cha kuwalazimisha wawekezaji kuondoka nchini.

Mmoja wa wabunge aliyeshiriki mazungumzo na Balozi huyo ni Zitto Kabwe wa jimbo la Kigoma Kaskaziani (Chadema), ambaye alithibitishia Mwananchi kwamba alikuwa anawashawishi kupinga mapendekezo ya kamati ya madini ambayo iliundwa na Rais mwaka jana na ripoti yake kukabidhiwa kwake Juni mwaka huu.

Kabwe alisema kwamba wabunge wa Chadema walimweleza wazi kwamba hawako tayari kukwamisha ripoti hiyo inayotarajiwa kujadiliwa na Bunge kabla ya kumalizika kwa mkutano wa 12 unaondelea sasa Dodoma, kwa sababu mapendekezo yake yamezingatia zaidi maslahi ya taifa.

Kadhalika, Kabwe alisema kwamba wamemweleza Balozi huyo kwamba Tanzania ni nchi huru na ina haki ya kuamua mambo yake kama inavyoona inafaa bila kuingiliwa na mtu yeyote kutoka nje.

Kabwe alisema kwamba walimweleza Balozi huyo kwamba mikataba ya sasa ya makampuni makubwa ya uchimbaji madini ilifikiwa kwa kutumia sheria ya madini ya mwaka 1998 ambayo ilitungwa kwa ushauri na ushawishi mkubwa wa Benki ya Dunia hali ambayo haikuzingatia kwa kina maslahi ya taifa.

Alisema sheria hiyo ina upungufu mkubwa katika kutetea maslahi ya taifa ndiyo maana pamoja na Tanzania kuwa nchi ya tatu kwa uzalishaji wa dhahabu Afrika, baada ya Afrika Kusini na Ghana, bado madini hayo hayajaweza kusaidia kutokomeza umasikini wa watu wake na wanaofaidi rasilimali hiyo ni makampuni makubwa ya nje.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Wilson Masilingi, alithibitisha kukutana na Balozi huyo na kujadiliana mambo mbalimbali, likiwamo suala la Darfur na Zimbabwe.

Kadhalika Masilingi alisema kwamba Balozi huyo alimweleza kuhusu ziara yake ya kutembelea migodi ya dhahabu iliyoko Kanda ya Ziwa.

Hata hivyo, Masilingi alisema Balozi huyo hakutoa ushawishi wowote kuhusu ripoti ya Kamati ya Madini.
 
Kevin Rutashobya - Dodoma (KLHN)

Some of the MPs who had had a chance to meet with the Canadian delegation in Dodoma during breakfast and dinner meals arranged and paid by the Canadians were enraged and others puzzled why such an effort from the Canadians (especially the presence of the Ambassador) except if the changes were to benefit the country and bring new standards, laws and regulations in the mining sector.

A Canadian source who spoke to KLHN on conditions of anonymity because she was not authorized to speak on the matter told KLHN that the Ambassador and her delegation are returning to Dar-es-Salaam ASAP where she is expected to issue a statement on the matter probably sometimes on Friday.

KLH News International inatuambia kwamba Wabunge wamekunywa chai na kupata mlo wa jioni wa ma lobbyist wa Kikanada huku wamekasirika!

Haya. Kwanza hapo mtu kama mimi naanza kugutukia Wabunge na anaeripoti. Nasogeza macho kwenye screen ya Laptop kusoma kwa makini.

Ukifika mwisho huoni mahala panaonyesha kwamba kuondoka Dodoma kwa Wakanada sio kurudi kwa kawaida nyumbani anakoishi. Tunaahidiwa statement ya Ubalozi. Lakini hatujui ni statement ya aina gani inakuja. Na anae ahidi statement ni "Chanzo cha Kikanada," kisicho na mamlaka ya kuongelea. Lakini kimetoa siri. Siri kuhusu kushindwa kwao U-Lobby!

Labda tungesubiri statement kabla hatujafikiria kuanza chereko chereko.

Wengi wetu tuliopata bahati ya kuishi kwenye U-lobbying uliobobea,tunajua kwamba huvunji kifuniko cha champagne kushangilia kushindwa kwa lobbyist kabla sheria kupitishwa ambayo haina zile provisions walizokuwa wanataka ma lobbyist.

Balozi wa Kanada hakai Dodoma. Labda asingeweza kubaki Dodoma anatoa milo na chai mpaka mwisho wa Bunge. Inawezekana alikuwa ana ajenda na bajeti ya kutoa vikombe na sahani kadhaa kwa walengwa kadhaa katika muda wa siku kadhaa, kabla ya kurudi kwake Dar-es-salaam. Kama ambavyo amefanya.

Inawezekana hii stori imewahi mno.

Here is my bet: Kwenye hiyo statement itakayokuja, ma lobbyist wa Kanada watasema wanaisihi Serikali ifanye vile wanavyotaka Wakanada, na wataweka spin yao zaidi. Kwa maneno mengine, lobbying itaendelea. Na mechi bado hata haijaanza Bungeni, achilia mbali kuisha.

Kwa hiyo, siyo tu kwamba sija break out the champagne yet, but I will hold off on buying a bottle at all.

KLH News imeleta habari bila qualifications. Bila compelling support. Tunaweza kuja kukuta hii reporting imewahi mno.

Nikiambiwa nichague kati ya mkataba mbaya wa madini na press mbaya nitachagua mkataba mbaya. Kwa sababu press nzuri siku za mbele ita expose, itazuia, mkataba mbaya. Ndio maana sioni shida kusema aliyeleta habari inayowezekana imepinda kuhusu mikataba iliyopinda nae inawezekana amepinda.

Nasubiri. Siiiti majina hii reporting. Bado.
 
Stupid idiots wanafikiri Watanzania ni wale wale wa enzi ya ukoloni. Hakuna FISADI yoyote atakayeachiwa kuwadhulumu WTZ nguvu zao kamwe, huu ni mwanzo na mwisho. Tumenyanyaswa kiasi cha kutosha na kupuuzwa kiasi cha kutosha na iko siku VIBAKA wote wataishia Keko.

Alutta Continua! Hatuna mpango wa kubeba silaha na kuingia msituni ili kudai nchi yetu iendeshwe kwa kufuata sheria na pia rasimali zetu ziwanufaishe Watanzania wote, lakini kamwe hatutakaa pembeni na kuwaangalia vikaragosi, manyang'au na mafisadi wakiendelea kufuja utajiri wetu kwa kuwafaidisha kundi lao la watu wachache na wageni ambao hawaoni aibu wala kusikia vibaya kusaini mikataba ambayo haina maslahi kwa nchi yetu. Mungu ibariki Tanzania na Watanzania wote wapenda haki na maendeleo ya Tanzania.
 
mzee unaniangusha.. mmoja kati ya 5000? it'll be a failure of incredible proportion... why not aim a little higher.. kwa sababu hadi hivi sasa tayari wapo members wa JF Bungeni.. sasa kumrudisha mmoja.. CCM watanesa nesa..

Ila wacanada wakiendelea hivi.. wasije kushangaa wanaongeza idadi ya watu wanaotaka kwenda Bungeni 2010

Now you're talking Mwankijiji. I'm willing to contribute hela ya Kampeni. This is a good start kama kweli tutaka kuichukua ile nchi toka mikononi mwa gang la wachache. The Kikwetes, the sittas, the...( that other guy..., I forget his name).
 
KLH News International inatuambia kwamba Wabunge wamekunywa chai na kupata mlo wa jiioni wa ma lobbyist wa Kikanada huku wamekasirika!

Haya. Kwanza hapo mtu kama mimi naanza kugutukia Wabunge na anaeripoti. Nasogeza macho kwenye screen ya Laptop kusoma kwa makini.

Ukifika mwisho huoni mahala panaonyesha kwamba kuondoka Dodoma kwa Wakanada sio kurudi kwa kawaida nyumbani anakoishi. Tunaahidiwa statement ya Ubalozi. Lakini hatujui ni statement ya aina gani inakuja. Na anae ahidi statement ni "Chanzo cha Kikanada," kisicho na mamlaka ya kuongelea. Lakini kimetoa siri. Siri kuhusu kushindwa kwao U-Lobby!

Labda tungesubiri statement kabla hatujafikiria kuanza chereko chereko.

Wengi wetu tuliopata bahati ya kuishi kwenye U-lobbying uliobobea,tunajua kwamba huvunji kifuniko cha champagne kushangilia kushindwa kwa lobbyist kabla sheria kupitishwa ambayo haina zile provisions walizokuwa wanataka ma lobbyist.

Balozi wa Kanada hakai Dodoma. Labda asingeweza kubaki Dodoma anatoa milo na chai mpaka mwisho wa Bunge. Inawezekana alikuwa ana ajenda na bajeti ya kutoa vikombe na sahani kadhaa kwa walengwa kadhaa katika muda wa siku kadhaa, kabla ya kurudi kwake Dar-es-salaam. Kama ambavyo amefanya.

Inawezekana hii stori imewahi mno.

Here is my bet: Kwenye hiyo statement itakayokuja, ma lobbyist wa Kanada watasema wanaisihi Serikali ifanye vile wanavyotaka Wakanada, na wataweka spin yao zaidi. Kwa maneno mengine, lobbying itaendelea. Na mechi bado hata haijaanza Bungeni, achilia mbali kuisha.

Kwa hiyo, siyo tu kwamba sija break out the champagne yet, but I will hold off on buying a bottle at all.

KLH News imeleta habari bila qualifications. Bila compelling support. Tunaweza kuja kukuta hii reporting imewahi mno.

Nikiambiwa nichague kati ya mkataba mbaya wa madini na press mbaya nitachagua mkataba mbaya. Kwa sababu press nzuri siku za mbele ita expose, itazuia, mkataba mbaya. Ndio maana sioni shida kusema aliyeleta habari inayowezekana ni imepinda kuhusu mikataba iliyopinda nae inawezekana amepinda.

Nasubiri. Siiiti majina hii reporting. Bado.

Of course.. sir.. I totally understand you.
 
.......Labda tungesubiri statement kabla hatujafikiria kuanza chereko chereko.

Wengi wetu tuliopata bahati ya kuishi kwenye U-lobbying uliobobea,tunajua kwamba huvunji kifuniko cha champagne kushangilia kushindwa kwa lobbyist kabla sheria kupitishwa ambayo haina zile provisions walizokuwa wanataka ma lobbyist. .............

........Balozi wa Kanada hakai Dodoma. .

Mkuu nakubaliana na wewe........Na hapa kuna swali...je hawa lobbyist walipoenda Dodoma ina maana wameishaiona hoyo ripoti ya Bomani?.

Halafu isije tukawa tunazugwa kama asemavyo mkjj....Sinclair alishaiona hii ripoti na sisi wenye nchi hatukuiona,tukapiga kelele vibaya sana.

Sasa isiwe hapa kuna game ya kutuliza wananchi kuonyesha kuwa sasa kuna mabadilko ktk sekta ya madini ambayo imewafanya hawa maKUPE ambawo wanaitwa wawekezaji kwenda Dodoma ku lobby kwa manufaa yao.

Sasa sisi tunafurahia kumbe hakuna mabadiliko yoyote bali yote hii ni kiini macho.
 
You know what.. nadhani itabidi tuyaweke haya mapendekezo hadharani... tumekaa kimya muda mrefu si kwa sababu hatujayaona yote, tunaheshimu process muhimu kama hii, lakini kama wazungu wanatudharau, basi hatuna buda kuwaonesha watu kile kinachopendekezwa ambacho kimeandikwa kwa kiasi kwenye vyombo vya habari.
 
Mkuu Mwanakikiji,

Uko right kabisa.

Umuhimu wa kuiweka hapa utakuwa kwa wananchi wengine kuelewa kwa mapana hasa pale watapoweza kusoma "between the lines".
 
Let me go to work.. kama wazungu wameweza kuyapata hadi kuamua kwenda kulobby, naamini na sisi tunaweza kuyapata yote.
 
JF Hongera sana; another success story. Kutokana na mafanikio haya tena, sasa nashauri kuwa jina rasmi la JamiiForums liwe
"JamiiForums (Sauti ya Wananchi)- Where we dare to talk openly "

Yaani tuongeze maneno "sauti ya wananchi" kwenye jina letu; mnaonaje.

Angalieni tu msije kuitwa mnatumia siasa za MUGABEISM!

Hapana, Kaka Mkandara. Sisi hatuwanyanyi mali zao kama alivyofanya Mugabe, tunaachotaka ni wao kulipa kodi tu. Ncho zote za Magharibi zimeendelea kutokana na kodi, kwa nini hawataki kutulipa sisi kodi? Mugabe alitibuwa kwa kuwanyanganya mali zao bila fair compensation, na sisi hatutafanya makosa hayo.
 
The only thing people need is support.. mwenzenu ndio maana leo na miye nimekuwa kimya muda mrefu... this is what I figured out.. if you need change, go and bring them! Sitakaa tena chini kulalamika on things on the ground... mwenye kutaka kukataa akae.. haitoshi tena kulalamika kwenye mtandao..!
I hear You Mkuu,and U'll have ma'vote4that, and i suppose from many JF members as well,but make sure You play YOUR best CARD the LAST!!
**just a word of advise.
 
hawa wazungu ni wajuzi sana wa mambo ya ku-lobby wayatakayo!

hapa inaonyesha kama wameshindwa, ila wasi wasi wangu waweza kuwa kajimtego fulani hivi.

twaweza ona kuwa yaliyopendekezwa na kamati ya bomani yanatosha na tukayapitisha haraka haraka kwa kuwa tunaona yapo sahihi kwa vile tu mcanada kashtuka.

tungeomba wabunge wapitie kwa makini kipengele kimoja kimoja cha mapendekezo, na iwapo mapendekezo hayo yanamuachia loop hole yoyote muwekezaji, yabadilishwe ili faida iende kwa mwananchi
 
Sidhani kama wameshindwa... wanachofanya ni kujipanga upya. I'm really interested to hear utakachosema Ubalozi. Lakini vyovyote vile.. kuna hela nyingi sana iko njiani and I'm telling you Barrick at the end will get whatever they want. Hata hivyo, kama hilo litatokea tusife moyo kwa sababu kupambana na giant kama barrick it gonna be bloody messy!

They have the money, they have the resources.. they have CCM MPs believe me.. hata kina Zitto wapige kelele namna gani kama CCM haitaki... ndivyo haitakuwa.

So friends.. ndio maana tumesema wame "pull back" they have not totally withdrawn or defeated.. it is a strategic maneuver...
 
hawa watu wanapesa kama mchanga.....na wakati wa ku-lobby kuna vitu wanavyovisema hadharani na vyengine ni rushwa ya hali ya juu ambayo vijisenti kadhaa vitaingia mifukoni mwa wabunge moja kwa moja.

wabunge wa ccm, future ya taifa iko mikononi mwenu.....for once tusahauni ulafi binafsi na tukumbuke taifa.
 
Sidhani kama wameshindwa... wanachofanya ni kujipanga upya. I'm really interested to hear utakachosema Ubalozi. Lakini vyovyote vile.. kuna hela nyingi sana iko njiani and I'm telling you Barrick at the end will get whatever they want. Hata hivyo, kama hilo litatokea tusife moyo kwa sababu kupambana na giant kama barrick it gonna be bloody messy!

They have the money, they have the resources.. they have CCM MPs believe me.. hata kina Zitto wapige kelele namna gani kama CCM haitaki... ndivyo haitakuwa.

So friends.. ndio maana tumesema wame "pull back" they have not totally withdrawn or defeated.. it is a strategic maneuver...

I welcome this clarification.

It provides a more cautious and sober interpretation of today's event involving the return of Canadian lobbying envoys back to Dar-es-Salaam where their mission is based.

I am confident that it will add perspective to the original story which may have engendered an unrealistic 'mission accomplished' euphoria a tad too early.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom