Exclusive: Canada Pulls back!

Hapa ndipo tunaelekea kwenye kiini kabisa cha kunyanganywa raslimali zetu na kutufanya tukawa masikini.

Hapa ndipo tunatakiwa tukatae misaada badala yake tuseme Raslimali tulizo nazo zinatosha kutufanya tukawa matajiri kuliko hivyo vimisaada mnavyotupatia baada ya kutuibia mali zetu.

Na hapo ndipo tunaweza kuona kwa nini watu waliweza kupata ripoti ya kamati ya madini kabla ya watanzania. Lazima kama wanataka kuwekeza wafuate sheria za nchi na siyo tufuate sheria zao.

Mawazo mazuri sana. Lakini, Serikali ya kufanya hivyo iko wapi?
 
Mkakati unaonekana kuendelea na wamebadili mbinu,naambiwa kuwa huko Dodoma bungeni leo wajumbe wa kamati ya bunge ya nishati na madini wamekutana na maofisa wa benki ya Dunia, sasa kilichozungumzwa huko bado kukipata ila wajumbe wa kamati hiyo ni pamoja na Dr,Mwakyembe,Lucas Selelii, Mnyaa, Stella Manyanya,Shelukindo ndo mwenyekiti wa kamati ,nitalifuatilia kama naweza kumpata mmojawapo .

Ila taarifa ni kuwa ni juu ya ripoti ya madini.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom