Leo hii sikuamini macho yangu nilipouziwa mafuta ya dizeli kwa lita moja Tshs.2550 hapa Mwanza. Miezi michache iliyopita mafuta ya dizeli ilikuwa ama Tshs.2150 hivi. Hiyo tofautti ni kubwa sana. Nauliza kuna tattizo gani bei kupanda kwa kiasi hicho?. Mafuta ndo kila kitu na hii inapelekea gharama ya maisha kuwa ghali. Ni wakati muafaka Serikali kusimamia bei ya mafuta vinginevyo wanyonge watapata taabu sana.