EWURA yapandisha bei ya mafuta nchini

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,515
Leo hii sikuamini macho yangu nilipouziwa mafuta ya dizeli kwa lita moja Tshs.2550 hapa Mwanza. Miezi michache iliyopita mafuta ya dizeli ilikuwa ama Tshs.2150 hivi. Hiyo tofautti ni kubwa sana. Nauliza kuna tattizo gani bei kupanda kwa kiasi hicho?. Mafuta ndo kila kitu na hii inapelekea gharama ya maisha kuwa ghali. Ni wakati muafaka Serikali kusimamia bei ya mafuta vinginevyo wanyonge watapata taabu sana.
 
Nadhani pia ishu ya IRAN kuwekewa sanctions na Marekani inachangia.

Maana kwanzia walipotangaza kuwa watarudisha sanctions, bei ya mafuta ilipanda kwenye soko la dunia.

Kumbuka IRAN ni miongoni mwa nchi zinazochimba na kuuza mafuta duniani.
 
wavuvi nao wamepigwa marufuku kuvua kwa kutumia taa za solar wanaambiwa watumie karabai ambapo litre mmoja si China 2400 na kwa mtumbwi mmoja zinatakikana si China ya litre 12 alafu tunadanganyana nchi ya viwanda
 
kwa nnavyojua mimi, hili suala lipo nje ya uwezo wa nchi yetu hata nchi nyingine yoyote isipokuwa marekani LEO rais Trump mwenyewe kwa kinywa chake amekiri kuwa hata yeye ana hofu kuwa vikwazo vya Iran viaweza kuleta matatizo kwenye soko la mafuta, lakini akasema ndo maana amewarusu baadhi ya washirika wake waendelee kununua mafuta ya Iran ili hali isiwe mbaya.
 
Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati, Maji na Mafuta (EWURA) imetangaza ongezeko la bei ya nishati ya mafuta ya dizeli, petroli na mafuta ya taa kwa mafuta yanayoshushwa kwenye bandari za mikoa ya Tanga na Dar es Salaam huku ikitaja kupanda kwa bei kwenye soko la dunia kuwa chanzo cha ongezeko hilo.
 
Na bei ikishuka kwenye soko la dunia huwa wanasema ni serikali ya wanyonge imeshusha bei ili kila mtanzania apate ñafuu ya maisha.

Nchi yenye laana hii.
 
Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati, Maji na Mafuta (EWURA) imetangaza ongezeko la bei ya nishati ya mafuta ya dizeli, petroli na mafuta ya taa kwa mafuta yanayoshushwa kwenye bandari za mikoa ya Tanga na Dar es Salaam huku ikitaja kupanda kwa bei kwenye soko la dunia kuwa chanzo cha ongezeko hilo.
na iatapanda mpaka 5,000/litre
 
Nchi hii Ccm mfanye kila liwezekanalo mumkabidhi George Boniphas Simbachawene Msomi asiye na makuu na mtu, mwenye upeo na hofu ya Mungu asiye mnafiki mpenda watu na mwona mbali kabisa. Tatizo la Ccm wanaangalia wapiga kelele wanawapa nchi badala ya kuangalia presidential materials ndio maana leo tupo tusipopajua.
 
Kitakachotuokoa uchumi wetu na athari za bei ya mafuta ni pale Uganda na Kenya watakapoanza kusafirisha na kuuza mafuta yao.

Vv
 
Nchi hii Ccm mfanye kila liwezekanalo mumkabidhi George Boniphas Simbachawene Msomi asiye na makuu na mtu, mwenye upeo na hofu ya Mungu asiye mnafiki mpenda watu na mwona mbali kabisa. Tatizo la Ccm wanaangalia wapiga kelele wanawapa nchi badala ya kuangalia presidential materials ndio maana leo tupo tusipopajua.

Kwa sifa hizi ww utakuwa Simbachawene.
 
vitu viwili vikubwa ndio vinachangia kuhusu bei ya nishati hii,kwanza bei ya mafuta kimataifa na pili sarafu yetu ina behave kivipi against US dollar;kama vyote hivi vinafanyika yaani bei ya soko la kimataifa la mafuta linapanda,na sarafu yetu dhidi ya US dollar inashuka ,tuelewe bei ya mafuta nayo itakuwa inapaa,ufumbuzi hapa na pamoja na kuimarisha public transports,nishati mbadala kuendesha mashine zetu,etc etc
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom