Mbalamwezi
JF-Expert Member
- Sep 30, 2007
- 800
- 171
Mbalamwezi salama Mkuu,Wazambia wananunua Mafuta kwetu kwa sababu hela yao muda mrefu against us dola inayumba sana kuna kipindi ilifika us dola mia kwacha milion na laki tano ndio maana wakibadilisha shilingi kwa kwacha wanaaona bora wanunue hapa kwetu kama sisi tunavyotaka kununua mafuta kutoka kenya..isanga home kwa sasa nipo Arusha Mkuu.ukiwa bara bara ya Namanga, tarakea au holili boda eti biashara ya magendo ni mafuta ya Taa? Yaani ni kazi kwa kuwa hapa kwetu yapo juu kwa sababu eti ya kuzuia uchakuchuaji ni akili hiyo mkuu kweli au wezi walitoa walitoa wazo ili waibe kisheria maana bunge si lilipitisha sheria ya kupandisha bei ya Mafuta ya Taa wakati katika masoko ya Nje haipo bei iyo..
MwanaIsanga,
sasa ndiyo ugundue kwamba hata shilingi yetu inazidi kuwa dhaifu against dollar kila kukicha kama wazambia wanavyopata shida na Kwacha yao. Na hii ina effect kubwa tunaponunua mafuta nje ya Nchi: Exchange rate.
Mafuta ya taa hayajawahi kuwa bei rahisi kule yanakotengenezwa. Na sisi hapa hayajawahi kuuzwa kwa bei rahisi. isipokuwa yalionekana bei rahisi machoni pa watumiaji kwa sababu serikali iliondoa kodi miaka ya nyuma. Otherwise ni mafuta yanayopatikana kwenye mchakato ule ule wa refining Petrol na Diesel, na gharama ni zile zile. Inasikitisha kuwa baada ya kuwa hayana kodi kwa miaka mingi, wengi wetu tunayaona kuwa ni ya masikini. Unajua hayo ndiyo yanaitwa JET A1 kwa jili ya ndege? Kwa hiyo hutegemei kwamba mafuta ya ndege yakawa bei rahisi, isipokuwa serikali iliamua kurejesha kodi yake, nadhani walitaka fedha zaidi kwenye bajeti ya serikali. japo ni kweli yalitumika saana kwenye uchakachuaji... wale wa arusha, Moshi na Kibaha Chalinze wanajua huu mchezo. Millions of kerosene ziliishia maeneo hayo...huko kwenu Tukuyu zilikuwa zinakuja lita chache tu mwashie taa.