EWURA yafafanua kutoshuka bei ya mafuta nchini

Hivi Ukiangalia CNN na kuona picha ya mteja akijaza mafuta kwenye gari lake na bei imeandikwa kuwa imeshuka.....huyo mtaalamu wa Ewura anatuambiaje kuwa ni crude oil?

EWURA NI JIPU NA NI LAZIMA LITUMBULIWE
Mkuu naona ungetafuta kwanza maana ya neno crude oil ndio utie comment yako hapa
 
Kapyungu mkuu, kuna watu wanabisha kwamba bei ya soko la dunia si ya crude oil? Duh? Sasa mtu kama huyu unamsaidiaje? nimepost picha hapo juu labda ataielewa zaidi.
 
Kwanza watanzania inabidi wajue maana ya crude oil. Baada ya hapo EWURA imesema 46-49% ya bie ya mafuta hutokana na kuyatoa kutoka crude kwenda kwenye refined. Sasa hapa mchawi ni REFINING. Tukiweza kupambana na huyo mie najua bei lazima itashuka tu. Ikumbukwe kuwa makampuni mengi yanachimba mafuta lakuni hayachakatui. Huyo anayefanya kazi ya kuchakatua nae anataka faida. Na huo mzigo wote utakuja kwa mtumiaji wa mwisho ambaye ni mtanzania
 
Mkuu naona ungetafuta kwanza maana ya neno crude oil ndio utie comment yako hapa
Na ikumbukwe kuwa hali hii imepelekea makampuni mengi kusimamisha shughuri za uchimbaji. Kwan operating cost inazidi profit. Sasa isingekuwa bei ya mafuta ghafi kushuka!! Bila shaka na haya makampuni yangeendelea na uchimbaji wa mafuta. Lakin wanaogopa wakihofia kupata hasara zaidi
 
Hizi habari za kampuni nyingi kujiondoa kwenye uchimbaji nadhani ndiyo zinawakumba wenzetu Wakenya. Kampuni za mafuta sasa zinaangalia kwingine na moto wa uchimbaji mafuta uko chini. Pengina jambo la msingi pia ni kuangalia kwa namna gani bei za mafuta za majirani zetu zimeshuka. Miaka mitatu iliyopita nilifanya survey tena kwa kutumia mtandao hapa...nikaona kati ya nchi tisa majirani, nyingi ziliuza mafuta bei ya juu kuliko sisi, chache sana bei zilifanana including Kenya, na ni Angola tu ilikuwa na bei ya chini sana tena ni kwa kuwa nilikwenda nje ya majirani zetu. Inasaidia pia kujielimisha zaidi kwa kuangalia trend ya majirani, Afrika na pengine na mabara mengine pricingi ikoje.
 
Watz sijui lini lini tutaenjoy national cake,...daahhhhh
all days viongoz wanatafuta nyanja za kumbana mtz na kumnyonya kwa kile kidoogo alichonacho,....
mafuta yanashuka word market,..sisi kwetu hayashuki,...nchi zingine zote jirani yameshuka ila tz 7bu mingi,..
yakipanda fasta hawasubiri miez miwili mbele,...
hapa napata picha kuina force kutoka kwa viongoz wapigaji wanapiga,...
ila sisi watz wajinga kwanini tusigomeee mafuta yaoo hata siku1 wapate lesson hawa jamaa
waache ujinga wao,..
alaf wanachukulia easy,..
 
Dizeli Dar es Salaam Sh 1,747, Nairobi Sh za Tanzania 1,899. Uganda ni sh za Tanzania 1913, Rwanda ni sh 2, 506. Zambia sh 1,693 (na hawa wana refinery na wanaagiza white product pia).
 
Yasema kushuka kwa bei ya mafuta katika soko la dunia kutaendelea kushusha bei hapa nchini LAKINI sio kwa wakati huohuo KWA SABABU hiyo bei watu wanayolalama ni ya mafuta ghafi na zaidi stock inayouzwa wakati husika siyo ile inayotajwa kwenye news break CNN, BBC kwamba imeshuka.www.ewura.go.tz
================

View attachment 318523

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU BEI ZA MAFUTA KATIKA SOKO LA DUNIA NA LA HAPA NCHINI​

1. UTANGULIZI

Mamlaka ya Huduma za Nishati na Maji (EWURA) inapenda kutoa taarifa halisi kuhusiana na mwenendo wa bei za mafuta katika soko la dunia na la hapa nchini. Kati ya majukumu ambayo EWURA imepewa ni kuweka bei KIKOMO za mafuta aina ya petroli katika soko la hapa nchini, utaratibu ulioanza rasmi Januari 6, mwaka 2009 baada ya kutokea hali ya kukosekana uhalisia wa bei za mafuta katika soko la ndani ikilinganishwa na mwenendo wa bei katika soko la dunia. Matokeo yake ni kuwa watumiaji mafuta walikuwa wakinunua mafuta kwa bei isiyo halisi (2,200/= kwa lita) katika miezi ya mwisho mwaka 2008, na pia uchumi wa nchi uliathirika na mwenendo huu wa bei. EWURA ilishusha bei hizo hadi kufikia 1,140/= baada ya kuanza kupanga bei mwezi Januari 2009.

Pamoja na kwamba bei za mafuta katika soko la dunia ndicho kigezo kikubwa cha upangaji wa bei katika soko la ndani, kuna gharama zinazoambatana na uagizaji mafuta hayo hapa nchini, kama vile gharama za usafirishaji, faida za waagizaji mafuta, kodi za Serikali, gharama za bandari na tozo za mamlaka mbalimbali nk. Kwa bei za Januari 2016, kwa mfano, mchango wa bei hizi za ndani unaochangiwa na bei za mafuta masafi katika soko la dunia ni: Petroli 46.60%, Dizeli 47.82% na Mafuta ya Taa 49.83%. Lazima ifahamike kuwa bei zinazooneshwa kwenye mitandao mbalimbali ni bei za Mafuta GHAFI (Crude Oil) ambayo yakisafishwa hutoa petroli, dizeli, mafuta ya taa na ndege, gesi ya kupikia (LPG), oil, lami n.k. EWURA inaweka bei hizi kwa kuangalia bei halisia ya mafuta yaliyosafishwa na si mafuta ghafi.

2. UHUSIANO WA BEI ZA MAFUTA GHAFI KATIKA SOKO LA DUNIA NA BEI ZA HAPA NCHINI

Mafuta ghafi (crude oil) yanaponunuliwa katika soko la Dunia inabidi yapelekwe kwenye viwanda vya kusafishia mafuta (refineries) ili kupata mafuta safi. Hatua hii huchukua takriban miezi miwili mafuta hayo kutufikia sisi kama walaji hapa Tanzania.

Bei za mafuta katika soko la ndani hukokotolewa kwa kutumia gharama halisi za uagizaji mafuta nchini ambazo hutokana na meli za mafuta yaliyopokelewa katika mwezi husika, ambayo huwa yamenunuliwa mwezi wa nyuma yake. Hivyo uhusiano wa bei za soko la dunia kwa mafuta masafi na za soko la ndani huwa ni kwa kupishana kwa miezi miwili kama inavyoainishwa na Jedwali Na. 1.0. Aidha, uhusiano wa bei za mafuta ghafi katika soko la dunia na bei za hapa nchini huwa ni kwa wastani wa miezi mitatu au zaidi.

Jedwali Na.1 Uhusiano wa bei za mafuta masafi katika soko la dunia na soko la ndani
View attachment 318524

Bei za mafuta hapa nchini hupangwa na Mamlaka ya EWURA kwa kutumia kanuni (formula) maalum ambayo inatayarishwa kwa kuzingatia uhalisia wa vigezo husika. Aidha, utayarishaji wa kanuni hii huhusisha wadau wote na kisha kuchapishwa katika gazeti la Serikali baada ya kupitishwa na Bodi ya EWURA.

3. MWENENDO WA BEI ZA MAFUTA KWA SASA
Katika kipindi cha mwaka 2014 hadi Januari 2016 bei za mafuta katika soko la Dunia zimeendelea kushuka. Kushuka kwa bei za mafuta katika soko la dunia kutaendelea kushusha bei hapa nchini japo si wakati ule ule. Aidha ni muhimu kuzingatia kuwa bei za mafuta masafi katika soko la dunia huchangia takriban asilimia 46 mpaka 49 ya bei katika soko la ndani (kwa bei za Januari 2016), hivyo kushuka huko hakuwezi kuwa na uwiano wa asilimia mia na kushuka kwa bei

katika soko la ndani. EWURA itaendelea kutimiza wajibu wake kisheria katika sekta ndogo ya mafuta hapa nchini ikiwemo upangaji wa bei kikomo za mafuta, na pia kusimamia bei hizo katika maeneo yote nchini.

Ni vizuri ikakumbukwa pia kwamba hata hivi karibuni, bei za mafuta katika soko la Tanzania zimekuwa zikishuka kufuata mwenendo wa bei za mafuta katika soko la dunia kama ifuatavyo:
a) Bei ya petroli ilishuka toka kiwango cha juu zaidi, mwezi Septemba 2014, Shillingi 2,267 kufikia shillingi 1,898 kwa lita mwezi Januari 2016, hii ikiwa ni kupunguka kwa Shillingi 369 kwa lita.

b) Bei ya dizeli ilishuka toka kiwango cha juu zaidi, mwezi Aprili 2014, shillingi 2,149 kufikia shillingi 1,747 kwa lita mwezi Januari 2016, hii ikiwa ni kupunguka kwa shillingi 402 kwa lita.

c) Bei ya mafuta ya taa ilishuka toka kiwango cha juu Zaidi, mwezi Februari 2014 shillingi 2,069 kufikia shillingi 1,699 kwa lita mwezi Januari 2016. Hii ni sawa na punguzo la shillingi 370 kwa lita.

Punguzo hilo la bei limepatikana licha ya ongezeko la kodi ya Serikali la Shilingi 100 kwa lita ya mafuta na kushuka kwa thamani ya Shilingi ilishuka dhidi ya Dola ya Marekani ambapo katika mwaka 2015, thamani ya Shilingi dhidi ya Dola ilishuka kwa asilimia 30 toka Shilingi 1,729 kwa Dola ya mwezi Januari 2015 kufikia Shilingi 2,254 kwa dola mwezi Agosti 2015 na baada ya hapo thamani ya Shilingi imepanda kufikia Shilingi 2,158 mwezi Disemba 2015.

4. UZINGATIAJI WA KANUNI KATIKA KUKOKOTOA BEI ZA MAFUTA
Kanuni ya kukokotoa bei za mafuta ni ya wazi, siyo siri, na huandaliwa kwa mchakato ambao ni shirikishi na huhusisha wadau mbali mbali ikiwa ni pamoja na vyombo vya Serikali, wafanyabiashara wa mafuta na pia wawakilishi wa watumiaji wa mafuta. Kanuni inaelekeza kuwa kabla EWURA haijafanya mabadiliko yoyote ni lazima utaratibu huu uzingatiwe, isipokuwa kwa maamuzi ambayo yanapitishwa na Serikali, hususan kodi na tozo mbali mbali. Kunapotokea mabadiliko ya kodi au tozo za Serikali, EWURA hufanya mabadiliko husika mara moja, baada ya kupata waraka husika kutoka Serikalini.

5. HITIMISHO
Kushuka kwa bei za mafuta katika soko la dunia kutaendelea kushusha bei hapa nchini japo si wakati ule ule, kwamba yakishuka leo, kesho yanashuka hapa nchini.

Aidha kumekuwa na upotoshaji kwamba EWURA haishushi bei za mafuta kwa kuwa kushuka kwake kutaadhiri mapato yake. Ukweli ni kwamba tozo ya EWURA inatokana na lita za mafuta na si bei, kwa maana kwamba iwapo EWURA ingetaka mapato mengi, basi ingeongeza wingi wa lita za mafuta yanayoingia hapa nchini, na si kutegemea kupanda kwa bei. Hivyo basi kushuka au kupanda kwa bei hakuna uhusiano wowote na ongezeko la tozo kwa EWURA.

Imetolewa na Felix Ngamlagosi
Mkurugenzi Mkuu - EWURA
Hii nchi bhana!!! mnataka tubinafsishe mpaka akili Za mtanzania??? Hili lishirika huwa silielewi kabisa..
 
Mbona bei ikipanda mko faster kupandisha?? kwenye kushusha mnakuja na vimajedwari vya kitoto.
Dunia nzima inajua mafuta yameshuka bei mwenye kupinga hilo atakuwa msugule
 
Watz sijui lini lini tutaenjoy national cake,...daahhhhh
all days viongoz wanatafuta nyanja za kumbana mtz na kumnyonya kwa kile kidoogo alichonacho,....
mafuta yanashuka word market,..sisi kwetu hayashuki,...nchi zingine zote jirani yameshuka ila tz 7bu mingi,..
yakipanda fasta hawasubiri miez miwili mbele,...
hapa napata picha kuina force kutoka kwa viongoz wapigaji wanapiga,...
ila sisi watz wajinga kwanini tusigomeee mafuta yaoo hata siku1 wapate lesson hawa jamaa
waache ujinga wao,..
alaf wanachukulia easy,..
Yani nchii unawezakufika mahali ukawaza kesho utembee uchi mpaka ikulu
 
Mimi sion faida ya kuwa mtz,..
yan unakandamizwa na unaibiwa huku unaona na wezi ni viongoz wako,..
BORA KUBEBA BOX wakuu canada/swiden
 
Umenena mkuu, Mh. Magufuli tunaomba turudishie Maseru hapo ndio anapajulia, wapiga kazi bongo wana puuzwa sana sijui kwanini.
Anaitwa Haruna Masebu. Enzi zake EWURA walijali maslahi ya wananchi.Sasa kuna vibaka.na vibaraka wao wanakuja kuwatetea humu na vijijedwali uchwara..ooh data ..data.
 
Haiwezekani mali ghafi(crude) ishuke bei toka dola 145 mpaka dola 28 halafu bidhaa zake zibaki bei ile ile. huu ni wizi wa mchana.
 
Tusilalamike tu wabongo...hebu google tu bei ya wese Marekani sasa hivi ujue sh ngapi...tusidanganywe kirahisi na blah blah
 
Mbalamwezi

Kuna mambo ya hovyo ambayo watawala wakiafrika wanafanana sana katika utawala wao. Hilo ulielewe

1. Uchu na ulafi wa kulazimisha kutawala

2. ulafi, rushwa na wizi wa mali za umma

3. kufanya biashara wakiwa ikulu ama kupitia wanyabiashara

Hilo ndiyo eneo la kwanza ufaham kwamba wewe bwana mbalamwezi na wafanyabiashara wenzako mnalopitia kutuibia raia. (udhaifu wa wanasiasa hasa kufilisi mataifa yao kupitia biashara haram.......fuels, maliasilin nk. yaan

Hili linanya yafutayo na usibishe kishabiki.
a. Bei za mafuta zonapopanda hakunana lawama wala mjadala simnapata faida.

-Hutangazwa maramoja tena kwa asilimia stahiki zimepanda

-Sababu za kipuuzi kama transport, crude au kodi huwa haziongelewi isipokuwa ile asalimia ya ongezeko. (wanasiasa hawasemi lolote maana nao wajasiliamali)

b. Bei zamafuta zikishuka .....
-kwanza hazitangazwa unless watu wapige kelele sana tena baada ya muda mrefu

- visingizio vya kod, dola, crude oil, transport cost nk

- ikitangazwa nikwaasilimia kidogo ambayo kimahesabu haindani na ukweli ( Hapa kwenye hesabu ndo ushenzi woote unafichwa na hakuna ukweli zaid ya utapeli)

Hiyo nisehem ya kwanza ninakuja sehem yapi kukuuliza maswali yamsingi kuhusu hoja kwamba data zangu nyingi ni assumption nitataka majibu yastaha, weledi na kina.
 
Shida yote hii ni kwasababu mataifa mengi ya afrika ni tegemezi. Tukitaka kutoka hapa tujitegemee kwanza ndio tutaona manufaa
 
Mbalamwezi
Tuanze na production cost .....ambazo nimesema ni fixed whether crude imepanda au imeshuka

1. overhead cost huwa haishuki maana nimalipo ya wafanyakazi nk

2. cost of equipment maintenace
Hizi zinabaki palepale hata ukizalisha pipa moja
-running & power consumtion of all systems
-wear rate
-spareparts
nk

Sanasana hapa ufukuze wafanyakazi bali huwezi shusha mishahara yao au huwezi zima baadhi ya mitambo kubana matumizi process itakuwa incomplete.

Hivyo hii hoja ieleweke hivyo......tunaendelea
 
Formula siyo siri iwekwe wazi tuone au ndo kusema siyo siri halafu mnatuacha hewani tunyamaze?
 
Back
Top Bottom