EWURA tuambieni ukweli ni upi kuhusu upungufu wa mafuta ya petrol wiki ijayo

REJESHO HURU

JF-Expert Member
Mar 6, 2014
4,460
9,394
Mod usifute huu uzi na upaste kama ulivyo andikwa kigogo media

Kiburi cha rushwa ,uhuni na ujeuri wa EWURA na waziri wa nishati wafikisha mgogoro wa upungufu wa mafuta ngazi za juu serikalini, chanzo chetu ndani ya EWURA kinatujulisha asubuhi na mapema leo hii.

Baada ya kuona nchi inaingia kwenye uhaba wa petroli na bidhaa hiyo kuanza kuadimika ,EWURA kupitia mkurugenzi wake mkuu Dokta Andilile wamewaandikia barua ya vitisho chama cha waagizaji mafuta Tanzania (TAOMAC) na kuwatishia kuwafutia vibali kama wataendelea kukaidi kukutana na waziri January Makamba ambaye anahaha kutaka kukutana na wafanyabishara hao kwa siku tatu sasa lakini wamegoma kukutana naye katika jitihada za kunusuru nchi kukosa mafuta ya petroli baada ya muagizaji aliyepewa tenda hiyo kwa rushwa kushindwa kufanya hivyo mpaka sasa.

Madai ya TAOMAC ni kuwa hawawezi kukutana na waziri ambaye wamekuwa wanamuomba kukutana naye zaidi ya miezi mitatu lakini hataki kukutana nao na amefika hatua hataki kupokea simu zao.

TAOMAC wamekwenda mbali zaidi na kusema hawawezi kukutana na mtu ambaye ana kampuni yake na watu wake ambao ndiyo anawapa kazi ya kuagiza mafuta kwa makubaliano wanayoyajua wao, sasa iweje leo kampuni hiyo imekwama kuleta mafuta ndipo waziri aone umuhimu wa kukutana nao?

TAOMAC wameendelea kulalamikia uamuzi wa EWURA kuwaandikia barua za vitisho na kuwaambia watafutiwa vibali vya kuagiza mafuta kama hawatataka kukutana na waziri January Makamba ifikapo leo jioni.

Malalamiko ya rushwa na matumizi mabaya ya ofisi juu ya waziri January Makamba kwenye hii wizara hayajaanza leo na yamekuwa ni mengi sana. Ikumbukwe wakandarasi wa REA walishafikisha malalamiko ya kunyimwa tenda kwa kuwa wamekataa kutoa rushwa kwa waziri na TANESCO kitu ambacho kilikuja kugungulika na CAG kwenye ukaguzi wake kuwa makampuni yakikoseshwa tenda bila vigezo wala sababu za msingi na hii inaashiria rushwa.

Suala la uagizaji wa mafuta ni nyeti sana na linabeba hatma ya uchumi wa taifa na watu wake. Kitendo cha EWURA kutishia kufuta vibali kwa TAOMAC ni wazi kuwa wafanyabiashara hawa wamechoshwa na rushwa na matatizo January Makamba kama waziri wa hii sekta kwa matendo yake ya rushwa za waziwazi na dharau kwao kama wadau muhimu wa sekta ya mafuta nchini.

TAOMAC wamesema walikutana na mmoja ya kiongozi mkuu wa serikali wiki iliyopita kuelezea matatizo na shida wanazopata na vitisho kutoka kwa waziri January Makamba na hawako tayari kukutana naye kwa lolote kwa kuwa alishaonyesha dharau na kutotoka kuonana nao siku za nyuma hivyo hawaoni haja ya kuonana naye sasa kwa kuwa nchi iko kwenye shida ya kukosa mafuta ya petroli.

Tunajua na tunafahamu mamlaka husika zinajua haya yote na tunajua uongozi wa nchi unajua juu ya upungufu na kukosekana kwa mafuta ya petroli kulikosababishwa na waziri January Makamba na mkurugenzi wa EWURA kuipa kampuni isiyo na uwezo kuagiza mafuta lakini yenye uwezo wa kuwahonga $2m ili ilete mafuta. Rushwa za namna hii ni hatari sana kwa ustawi wa jamii na zinapokuwa zinakaliwa kimya ni hatari zaidi kwa kuwa watanzania wanakosa majibu jinsi mnavyowaona na kuwafikiria mwisho wa siku wataona mtu huyu anafanya haya kwa kuwa mnamtuma au mnagawana mapato ya rushwa hizi kubwa kiasi hiki.

Mambo haya inawezekana yanawafurahisha huko CCM na ndiyo maana ma " god father" wa January Makamba wanamlinda na kumtetea kwa kuwa ni sehemu ya wanufaika wa hizi rushwa. Lakini mtazamo huu si mwema sana kwa CCM na serikali kwa kuwa kuna siku watanzania watawaweka kwenye chungu kimoja na mtapikwa kwa pamoja.

Ni kuinajisi nchi na kuinajisi serikali kuendelea kuwa na waziri mla rushwa wa kiwango cha January Makamba , ni makosa makubwa sana kukubali nchi kuingia kwenye shida kwa sababu ya mtu mmoja mla rushwa ambaye kadri siku zinavyozidi kwenda anaitumbukiza nchi kwenye majanga.
 
Dooo! Kama ni kweli utatokea uhaba wa mafuta Kwa sababu yake itabidi akae pembeni
Story ilinzia zia hapa

Tanzania inaingia kwenye uhaba mkubwa wa mafuta ya petroli kuanzia wiki hii. Vitendo vya rushwa vya waziri January Makamba kwenye kutoa vibali vya kuagiza mafuta ndivyo vimepekea hali hii ya sasa.

Gulf Petroleum waliomhonga bwana waziri January Makamba $ 2m ili waagize mafuta kwa kipindi cha April- June 2023 na sasa wameshindwa kuleta mafuta na leo tunajulishwa kuwa hakuna depot hata moja Dar Es Salaam yenye mafuta ya petrol kwa watumiaji wa Tanzania.

Tumekuwa tunasema sana matendo ya rushwa ya huyu waziri yanavyoharibu nchi na taswira ya serikali lakini wenye mamlaka wamekuwa viziwi na vipofu.

Kumlea kwenu ndiko kunaleta haya matatizo na sasa suala hili linakwenda kuichafua serikali nzima bila kuchagua kwa kuwa mnamlinda sana mtu huyu kwa sababu ambazo tunahisi kuna watu wananufaika na rushwa anazopokea kwenye haya mambo yake.

Waagizaji mafuta wamekwisha lalamika sana kuwa hata wawe na uwezo wa kimanunuzi mkubwa kiasi gani bila kumpa waziri huyu rushwa ya $1m - $2m hawapewi tenda ya kuagiza mafuta, lakini hakuna hatua zinachukuliwa.

January ni mla rushwa na hilo liko wazi ndiyo maana wakati nyie mnalalamika kuwa hakuna mafuta na watanzania wana hali ngumu yeye anaweza kwenda DT Dobie wiki iliyopita na kumnunua gari kwa $175,000 (cash). Hamjawahi kujiuliza anatoa wapi hizi hela? Sasa majibu yake ndiyi haya , huku ndiko anakotoa hela anazozichezea kwa kiwango hiki ndani ya nchi masikini kama Tanzania.

Ni aibu kwa serikali na EWURA kuanza kuomba mafuta ya transit wakopeshwe kwa ajili ya matumizi ya ndani.

Chanzo chetu ndani ya EWURA kimesema hali ni mbaya sana na hakuna meli yoyote ya mafuta inayokuja hivi karibuni hivyo ni wazi nchi inaingia kwenye upungufu na kutokuwapo kwa mafuta ya petroli kabisa.

Haya ndiyo mambo watanzania mnapaswa kuihoji serikali kwa nini mtu huyu analindwa na tunakubali kuiingiza nchi kwenye matatizo ya kiasi hiki kwa sababu ya mtu mmoja tu?
 
Una uhakika gani Kama Kuna Rushwa,Uhuni na Kiburi Cha mamlaka husika?

Hizi habari ambazo yule Jamaa wa twitani anazitoa dhidi ya wizara ya nishati Mara nyingi zinakuwa negative!!,yeye nadhani ana hasira na Mh.Makamba!!

Yeye kila tatizo ambalo linatokea kwenye hiyo wizara analipeleka kwenye mtazamo wa Upigaji na Rushwa!!
 
Ndio maana tumeomba EWURA waje watuambie ili kama uzushi tumpuzie
 
Mod usifute huu uzi na upaste kama ulivyo andikwa kigogo media

Kiburi cha rushwa ,uhuni na ujeuri wa EWURA na waziri wa nishati wafikisha mgogoro wa upungufu wa mafuta ngazi za juu serikalini, chanzo chetu ndani ya EWURA kinatujulisha asubuhi na mapema leo hii.

Baada ya kuona nchi inaingia kwenye uhaba wa petroli na bidhaa hiyo kuanza kuadimika ,EWURA kupitia mkurugenzi wake mkuu Dokta Andilile wamewaandikia barua ya vitisho chama cha waagizaji mafuta Tanzania (TAOMAC) na kuwatishia kuwafutia vibali kama wataendelea kukaidi kukutana na waziri January Makamba ambaye anahaha kutaka kukutana na wafanyabishara hao kwa siku tatu sasa lakini wamegoma kukutana naye katika jitihada za kunusuru nchi kukosa mafuta ya petroli baada ya muagizaji aliyepewa tenda hiyo kwa rushwa kushindwa kufanya hivyo mpaka sasa.

Madai ya TAOMAC ni kuwa hawawezi kukutana na waziri ambaye wamekuwa wanamuomba kukutana naye zaidi ya miezi mitatu lakini hataki kukutana nao na amefika hatua hataki kupokea simu zao.

TAOMAC wamekwenda mbali zaidi na kusema hawawezi kukutana na mtu ambaye ana kampuni yake na watu wake ambao ndiyo anawapa kazi ya kuagiza mafuta kwa makubaliano wanayoyajua wao , sasa iweje leo kampuni hiyo imekwama kuleta mafuta ndipo waziri aone umuhimu wa kukutana nao?

TAOMAC wameendelea kulalamikia uamuzi wa EWURA kuwaandikia barua za vitisho na kuwaambia watafutiwa vibali vya kuagiza mafuta kama hawatataka kukutana na waziri January Makamba ifikapo leo jioni.

Malalamiko ya rushwa na matumizi mabaya ya ofisi juu ya waziri January Makamba kwenye hii wizara hayajaanza leo na yamekuwa ni mengi sana. Ikumbukwe wakandarasi wa REA walishafikisha malalamiko ya kunyimwa tenda kwa kuwa wamekataa kutoa rushwa kwa waziri na TANESCO kitu ambacho kilikuja kugungulika na CAG kwenye ukaguzi wake kuwa makampuni yakikoseshwa tenda bila vigezo wala sababu za msingi na hii inaashiria rushwa.

Suala la uagizaji wa mafuta ni nyeti sana na linabeba hatma ya uchumi wa taifa na watu wake. Kitendo cha EWURA kutishia kufuta vibali kwa TAOMAC ni wazi kuwa wafanyabiashara hawa wamechoshwa na rushwa na matatizo January Makamba kama waziri wa hii sekta kwa matendo yake ya rushwa za waziwazi na dharau kwao kama wadau muhimu wa sekta ya mafuta nchini.

TAOMAC wamesema walikutana na mmoja ya kiongozi mkuu wa serikali wiki iliyopita kuelezea matatizo na shida wanazopata na vitisho kutoka kwa waziri January Makamba na hawako tayari kukutana naye kwa lolote kwa kuwa alishaonyesha dharau na kutotoka kuonana nao siku za nyuma hivyo hawaoni haja ya kuonana naye sasa kwa kuwa nchi iko kwenye shida ya kukosa mafuta ya petroli.

Tunajua na tunafahamu mamlaka husika zinajua haya yote na tunajua uongozi wa nchi unajua juu ya upungufu na kukosekana kwa mafuta ya petroli kulikosababishwa na waziri January Makamba na mkurugenzi wa EWURA kuipa kampuni isiyo na uwezo kuagiza mafuta lakini yenye uwezo wa kuwahonga $2m ili ilete mafuta. Rushwa za namna hii ni hatari sana kwa ustawi wa jamii na zinapokuwa zinakaliwa kimya ni hatari zaidi kwa kuwa watanzania wanakosa majibu jinsi mnavyowaona na kuwafikiria mwisho wa siku wataona mtu huyu anafanya haya kwa kuwa mnamtuma au mnagawana mapato ya rushwa hizi kubwa kiasi hiki.

Mambo haya inawezekana yanawafurahisha huko CCM na ndiyo maana ma " god father" wa January Makamba wanamlinda na kumtetea kwa kuwa ni sehemu ya wanufaika wa hizi rushwa. Lakini mtazamo huu si mwema sana kwa CCM na serikali kwa kuwa kuna siku watanzania watawaweka kwenye chungu kimoja na mtapikwa kwa pamoja.

Ni kuinajisi nchi na kuinajisi serikali kuendelea kuwa na waziri mla rushwa wa kiwango cha January Makamba , ni makosa makubwa sana kukubali nchi kuingia kwenye shida kwa sababu ya mtu mmoja mla rushwa ambaye kadri siku zinavyozidi kwenda anaitumbukiza nchi kwenye majanga.
CCM ni ukoo wa panya; kila mtu mwizi. Suluhisho la kudumu ni kuwaondoa hawa majizi madarakani moja kwa moja ifikapo 2025. La sivyo, hawa nyang'au watauza kila kitu kwa waarabu hadi wanatuuza na sisi kwa waarabu.
 
Unawaondoaje sasa?
 
Story ilinzia zia hapa

Tanzania inaingia kwenye uhaba mkubwa wa mafuta ya petroli kuanzia wiki hii. Vitendo vya rushwa vya waziri January Makamba kwenye kutoa vibali vya kuagiza mafuta ndivyo vimepekea hali hii ya sasa.

Gulf Petroleum waliomhonga bwana waziri January Makamba $ 2m ili waagize mafuta kwa kipindi cha April- June 2023 na sasa wameshindwa kuleta mafuta na leo tunajulishwa kuwa hakuna depot hata moja Dar Es Salaam yenye mafuta ya petrol kwa watumiaji wa Tanzania.

Tumekuwa tunasema sana matendo ya rushwa ya huyu waziri yanavyoharibu nchi na taswira ya serikali lakini wenye mamlaka wamekuwa viziwi na vipofu.

Kumlea kwenu ndiko kunaleta haya matatizo na sasa suala hili linakwenda kuichafua serikali nzima bila kuchagua kwa kuwa mnamlinda sana mtu huyu kwa sababu ambazo tunahisi kuna watu wananufaika na rushwa anazopokea kwenye haya mambo yake.

Waagizaji mafuta wamekwisha lalamika sana kuwa hata wawe na uwezo wa kimanunuzi mkubwa kiasi gani bila kumpa waziri huyu rushwa ya $1m - $2m hawapewi tenda ya kuagiza mafuta, lakini hakuna hatua zinachukuliwa.

January ni mla rushwa na hilo liko wazi ndiyo maana wakati nyie mnalalamika kuwa hakuna mafuta na watanzania wana hali ngumu yeye anaweza kwenda DT Dobie wiki iliyopita na kumnunua gari kwa $175,000 (cash). Hamjawahi kujiuliza anatoa wapi hizi hela? Sasa majibu yake ndiyi haya , huku ndiko anakotoa hela anazozichezea kwa kiwango hiki ndani ya nchi masikini kama Tanzania.

Ni aibu kwa serikali na EWURA kuanza kuomba mafuta ya transit wakopeshwe kwa ajili ya matumizi ya ndani.

Chanzo chetu ndani ya EWURA kimesema hali ni mbaya sana na hakuna meli yoyote ya mafuta inayokuja hivi karibuni hivyo ni wazi nchi inaingia kwenye upungufu na kutokuwapo kwa mafuta ya petroli kabisa.

Haya ndiyo mambo watanzania mnapaswa kuihoji serikali kwa nini mtu huyu analindwa na tunakubali kuiingiza nchi kwenye matatizo ya kiasi hiki kwa sababu ya mtu mmoja tu?

Hata mama anaweza kuwa beneficiary wa hii kitu, ndio maana January is untouchable
 
Back
Top Bottom