EWURA Kuondoa ushindani kwenye Petrol ni sawa?

Mparee2

JF-Expert Member
Sep 2, 2012
2,592
4,279
Binafsi sioni kama ni sawa kuondoa ushindani kwenye bidhaa (kibiashara)

Nilitamani EWURA watoe bei Elekezi ya juu, ila bei ya chini waache kila mtu ajipangie

Tumeona hii ikifanyika kwenye ada za Shule za private nk

Kuna vituo vya mafuta vyenye uwekezaji mkubwa na wanamitaji mikubwa hivyo wanaweza kuuza mafuta kwa bei rafiki ila wanalazimishwa na sheria wauze bei iliyopangwa lakini pia, unaweza kukutana na mafuta kwenye baadhi ya vituo sio ya kueleweka ila ndio hivyo tena wanatakiwa nao wauze bei hiyo hiyo.

Nafikiri pia bei elekezi ingetolewa kila baada ya miezi mitatu kwa wafanya biashara walioko pembezoni bei elekezi inayotolewa kila mwezi, sidhami kama inawasaidia; sana sana inawapa tu Changamoto kwani logistic ya kufanya manunuzi hadi mzigo uwafikie inawachukua pengine wiki mbili kwa hiyo inakuwa kama wametengwa au hawafikiriwi

"BIASHARA YENYE USHINDANI NDIO HULETA UNAFUU KWA MNUNUZI WA MWISHO/MWANANCHI"
 
Bei ya soda, vocha, bia, umeme nk una bei moja nchi nzima ingawa kampuni.za.huduma ni tofauti.
Namaanisha bei ya bidhaa hizo ni ile ile ama upo Dar, Tunduru, Muhambwe au Tanganyika jirani na Ziwa Tanganyika.

Ninachoshindwa kuelewa ni kwa nini Ewura ambayo imepanga bei moja umeme nchi nzima, imeshindwa kupanga bei moja ya mafuta nchi nzima.

Namaanisha kuwa, ni kwa nini sisi tulio wilaya za Kyerwa [Rubwera], Karagwe, Ngara na.nyingine za pembezoni tunauziwa mafuta bei kubwa kuliko wilaya zingine?

Mafuta yako juu lakini viwango vya nauli (LATRA) ni sawa nchi nzima.
Nauli hazipangwi kiwilaya/kimkoa.

Nashauri serikali.itafute namna ya kuweka bei moja ya.mafuta kwa nchi nzima.

Tunaumia sana.
Tupunguzieni maumivu haya.
 
Back
Top Bottom