Euro 2020 - Special Thread | Pata kujua yanayojiri katika Michuano hiyo

Naungana na ww, kiukwel huyo kocha anatukosea sana. Mchezo dhidi ya Hungary nilishangaa sana kile kikosi, Joao Felix hivi kwann hakupata nafasi ata ya kucheza? Kwann kocha alimkata Joao Cancelo kuelekea michuano hii?

Kiukwel Ureno wana kikosi kizuri mno kule mbele wana washambuliaji hatari sana. Cristiano Ronaldo, Joao Felix, Diogo Jota, Andre Silva na Bwana mdogo Pedro Goncalves. Huyo Andre Silva we msikie hivyo hivyo ila ana balaa lake. Kocha inabidi abadilike katika mbinu maana ana wachezaji wazuri shida ni namna ya kuwatumia.

Unajua Joao Felix msimu huu amekuwa na kiwango cha kupanda na kushuka, hata klabuni Atletico sio first choice!
 
Jamhuri ya Czech ya miaka ile ulitamba sana na ikawa timu tishio kwa vigogo mastaa kama Poborsky, Rosicky, Jan Koller, Petr Cech walikuwa moto wa kuotea mbali sana!!
 
Endapo England akifungwa na Czech Republic halafu kati ya Croatia na Scotland akashinda mmojawapo, England atakuwa best loser.

Ili kujiweka katika uhakika mzuri wa hatua inayofuata, England anatakiwa ashinde na wala asishindwe au kutoa droo.

Pia kusalimika kwake itategemeana Croatia na Scotland kutoka droo
IMG_20210619_004827_482.jpg
 
Back
Top Bottom