OFFICIAL THREAD: UEFA™ Champions League Competition Analysis And Statistics

Pionaire

JF-Expert Member
Oct 24, 2012
1,603
1,133
UEFA_Champions_League_logo_2.svg.png



* HISTORIA FUPI YA MICHUANO HII
Ni michuano ya soccer liyoanzishwa na mashirikisho ya mpira ya nchi wanachama barani ulaya(Union Of European Football Assocciations) miaka ya 1955 ikijulikana kama EUROPEAN COMPETITION CLUB'S CUP...hadi kufikia mwaka 1992 ambapo kombe lililokuwa likitolewa kwa mshindi wa michuano hiyo lilifanyiwa mabadiliko ya kimuundo(rebranded)...hii ilipelekea jina la michuano hiyo kubadilika na kuitwa UEFA CHAMPIONS LIGUE(LIGI YA MABINGWA BARANI ULAYA)...Hapo chini ni picha ya kombe ambalo lililokuwa likitolewa baada ya kufanyiwa mabadiliko anzia mwaka 1992 hadi Sasa...



12027782_988971374497713_5236862331586357253_n.jpg




*ZAWADI KWA WASHIRIKI
Katika michuano hii kila timu inayoshiriki hupata kitita cha pesa katika kila hatua ya ushiriki kama ilivyo hapo...
  • First qualifying round: €220,000
  • Second qualifying round: €320,000
  • Losers third qualifying round: €420,000
  • Losers play-off round: €3,000,000
  • Winners play-off round: €2,000,000
  • Base fee for group stage: €12,700,000
  • Group match victory: €1,500,000
  • Group match draw: €500,000
  • Round of 16: €6,000,000
  • Quarter-finals: €6,500,000
  • Semi-finals: €7,500,000
  • Losing finalist: €11,000,000
  • Winning the Final: €15,500,000
. Hiyo inamaanisha timu itakayoibuka kinara kwenye hatua zote hizo za michuano bila kupoteza itajinyakulia kitita cha €57,200,000.


* TIMU ZILIZOSHINDA TAJI HILO
Tokea kuanzishwa kwake michuano hiyo...Timu inayoongoza kutwaa taji hilo ni Real Madrid ikifuatiwa na nyingine kama ilivyo hapo...


FOOTBALL CLUBS THAT WON THE TITTLE

Real Madrid Imechukua Mara 12...Imepoteza Mara 3.
Milan Imechukua Mara 7...Imepoteza Mara 4
Bayern Munich Imechukua Mara 5...Imepoteza Mara 5
Barcelona Imechukua Mara 5...Imepoteza Mara 3
Liverpool Imechukua Mara 5...Imepoteza Mara 2
Ajax Imechukua Mara 4...Imepoteza Mara 2
Internazionale Imechukua mara 3...Imepoteza Mara 2
Manchester United Imechukua Mara 3...Imepoteza Mara 2
Juventus Imechukua Mara 2...Imepoteza Mara 7
Benfica Imechukua Mara 2...Imepoteza Mara 5
Nottingham Forest Imechukua Mara 2...Imepoteza Mara 0
Porto Imechukua mara 2...Imepoteza Mara 0


*WIMBO WA UEFA CHAMPIONS LEAGUE
Bila ubishi huu ni wimbo unaokonga sana Nyoyo za mashabiki Wengi wa soccer duniani,ulitungwa na mwanamuziki Mwingereza mwenye taaluma hiyo ya muziki anaitwa TONY BRITTEN mwaka 1992...mara tu baada ya mabadiliko ya kombe hilo kufanyika, Wimbo huo umetungwa kwa kutumia luga Tatu tofauti kwa pamoja zinazotumiwa rasmi na shirikisho la soka barani ulaya(UEFA) ambazo ni Kijerumani, Kifaransa na Kiingereza na maana yake In English ni kama ilivyo hapo chini...

Original song...
Champions League Theme

Ce sont les meilleures équipes
Es sind die allerbesten Mannschaften
The main event

Die Meister
Die Besten
Les grandes équipes
The champions

Une grande réunion
Eine große sportliche Veranstaltung
The main event

Ils sont les meilleurs
Sie sind die Besten
These are the champions

Die Meister
Die Besten
Les grandes équipes
The champions

Die Meister
Die Besten
Les grandes équipes
The champions


In English translation...
Champions league Anthem

They are the best teams
They are the best teams
The Main Event

The master
The best
Great teams
The Champions

A big meeting
A great sporting event
The Main Event

They are the best
They are the best
These are the champions

The master
The best
Great teams
The Champions

The master
The best
The Champions


#Mnaweza kuusikiliza Huo wimbo wote...Full version hapo...





*UPCOMING UEFA CHAMPIONS LEAGUE FINAL On 3rd June Of 2017 in CARDIFF



Ni Fainali ya 59 ya michuano hiyo barani ulaya, Ikiwakutanisha JUVENTUS(Mabingwa Wa Serie-A 2016/2017) Vs REAL MADRID(Mabingwa Wa LaLiga-Santander 2016/2017) itakayofanyika CARDIFF...tarehe 3 june.


RTS16BBO-1.jpg

18342306_1594241707267250_7859902669227826308_n.jpg

juve-real-ucl-final-2017.jpg
skysports-juventus-real-madrid-ronaldo-higuain_3966178.jpg

millennium-stadium_1232jjxiku02j1fl28v3uc21u4.jpg




#Mambo muhimu kwenye fainali hii...ambayo inahitajika kuyajua.
-Juve imefika Fainali za UEFA Mara 8...imeshinda 2 na kupoteza 6(Mara nyingi zaidi kuliko timu yeyote kweye michuano hiyo).
-Real imefika fainali Mara 14...imeshinda 11...na kupoteza 3(Mara chache zaidi ya Juve).

-Real Madrid inahitaji kuandika historia mpya kwenye michuano hiyo...kuwa ndiyo timu pekee barani ulaya kuchukua Taji hilo mara mbili mfululizo kama bingwa mtetezi.
-Pia Real Madrid inataka kuandika historia ya kuchukua mataji mawili yani LaLiga na UEFA Katika msimu mmoja...baada ya miaka 59 tokea msimu wa 1957/1958.

-Goli kipa Wa Juve ameruhusu magoli matatu tu kuingia wavuni tokea waanze michuano hii ya UEFA msimu huu.​
-Juve wameweza kutoka na Clean sheet 9(Hajafungwa goli ata moja kwenye mechi tisa za UEFA) katika mechi 12 za UEFA walizocheza msimu huu.
-Zidane anataka kuweka record ya kuwa kocha pekee barani ulaya aliyeweza kutetea taji lake la UEFA Champions League.
-Juve wameruhusu magoli 27 tu kwenye mechi zote za ligi walizocheza huku Madrid wameruhusu Magoli 41 kwenye mechi zote za Ligi walizocheza.
-Gianluigi Buffon anaelekea kustaafu Mpira kutokana na Umri wake...hivyo hii ni nafasi adhimu sana kwake kuchukua taji hili muhimu akiwa na Juve.
-Dani Alves anahitaji kuandika historia ya kuchukua Taji la UEFA na Juve katika msimu wake Wa kwanza.
-Cristiano Ronaldo anahitaji ashinde taji hili ili afikie record ya Mpinzani wake Wa soccer(Messi) Ya kutwaa mataji manne ya UCL.

-Real Madrid inahitaji kuwa timu ya kwanza na pekee kufikia record ya Magoli 500 katika michuano hiyo.

*ANALYSIS

dertu.png

juve-real-ucl-final-2017.png



#JUVENTUS FC
Juventus wanatarajiwa kutumia mfumo wa "4-2-3-1" au "3-4-2-1"...Juve hawatacheza mchezo Wa kushambulia muda wote Bali watatumia mashambulizi ya Counter dhidi ya Madrid,kwa mfumo Huo wa "4-2-3-1" utakaotumia Juve utamruhusu Higuain pekee kucheza mbele kama Forward huku Dyabala na mandzukich wakipandisha mipira kwa kujihami na wengine wakibaki nyuma Kwa tension ya kuzuia, Juve anajua wazi Madrid atashambulia sana kutafuta goli la mapema ili aweze kuumiliki mchezo na kujiamini...hivyo kipindi cha kwanza Juve hatoshambulia sana atajitahidi kulinda goli lisiingie ila kipindi cha pili atajaribu kushambulia kiasi akiona Madrid kacharuka sana atarudi kucheza kama first-half....na itakuwa bora sana kwa Juve kwenda Hadi extra-time ikiwezekana ata penalties wakijua Kipa wakueleweka wanaye kuliko kuruhusu goli dakika 90 za mchezo...na ikitokea wamefungwa mapema itawalazimu wafunguke ili wasawazishe...na hapa kuna mawili wanaweza wakafanikiwa ama wakaongezwa magoli.

#REAL MADRID C.F
Madrid wanatarajiwa kutumia mfumo Wa "4-3-1-2" au "4-3-3"...Madrid wanafahamu vyema ubora Wa defence ya Juve hivyo basi watahitaji goli la mapema ili waweze kuutawala mchezo...ukizingatia watakuwa na Full-backs wao wote wakupandisha mipira(Marcelo & Carvajal) ila watategemea sana mipira ya kupenyeza(penetrations) ili kuitoboa ngome ya Juve.

Note: Ifahamike mbali na uchambuzi Huo...Mpira ni dakika 90,na kuna ushindi wa magoli ya faulo na penalty pia...hivyo lolote litaweza kutokea mchezoni.​

Update nyingine tutaendelea kupeana Wadau...tukiwa tunausubiri huu [HASHTAG]#MTANANGE[/HASHTAG]!

FULL-TIME: JUVENTUS-1 Vs REAL MADRID-4

***REAL MADRID CROWNED THE EUROPEAN CHAMPIONS***
FOR THE 12th TIME!
Juventus-v-Real-Madrid-UEFA-Champions-League-Final (4).jpg

Real-Madrid-captain-Sergio-Ramos-lifts-t.jpg

Juventus-v-Real-Madrid-UEFA-Champions-League-Final (5).jpg
 
Cassemiro atakuwa anasumbuliwa na pijanic hapo tena na ambavyo hajui kupiga pass namuonea huruma sana
Hiyo umesema wewe kuwa hajui kupiga pasi ....kama hajui kupiga pasi angekuwepo pale Madrid..??..... Ungeniambia ni mtu wa fouls sana ningekuelewa. [HASHTAG]#forzajuve[/HASHTAG]
 
Hiyo umesema wewe kuwa hajui kupiga pasi ....kama hajui kupiga pasi angekuwepo pale Madrid..??..... Ungeniambia ni mtu wa fouls sana ningekuelewa. [HASHTAG]#forzajuve[/HASHTAG]
Duh!mwandiko wako unaonyesha ww ni sabiki mpuuzi wa Manchester maana mashabiki wa Madrid tupu huwa hawapanic kipuuz hivi
 
Hiyo umesema wewe kuwa hajui kupiga pasi ....kama hajui kupiga pasi angekuwepo pale Madrid..??..... Ungeniambia ni mtu wa fouls sana ningekuelewa. [HASHTAG]#forzajuve[/HASHTAG]

Mkuu Huyo anajua sana ukabaji Wa casemiro ila maigizo tu analeta hayo...dyabala hatotembea hata sentimeta moja yule.
 
Unaambiwa baba hakuna mbabe kwenye makutan ya vibibi vizeee na watukutu Madrid date wababe je nan mbabe
 
Sijui ni mimi tu, lakini fainali hii ya mwaka huu imekuwa na msisimuko wa aina yake, naifananisha na ile ya mwaka 2008 Man Utd vs Chelsea.

All in all, atakayekuwa kuwa mjanja wa kumsoma mwenzake vizuri ndiye atakaye shinda.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom