ndetichia
JF-Expert Member
- Mar 18, 2011
- 27,769
- 6,585
Its Me Sir...
Hands shakes.
Still ilikuwa ni Game ngumu kwa pande zote mpaka dakika ya 59 but kupata Jeraha Thiago Motta kumepelekea timu ya Italy kupwaya na pia Spain kutumia upungufu huo wa wachezaji 10 uwanjani kuutawala mchezo kwa ujumla na kupata magoli mawili ya ziada.
Kwa yoyote mwenye utimamu kichwani atagundua tofauti ya Italy walivyokuwa 11 na walivyobaki 10.
pia Italy tuliweza kutengeneza nafasi lakini tukashindwa kuzitumia.
Nimesikitika kusoma kauli za ndugu zangu ambao huwa nawaamini sana ktk maswala ya uchambuzi wa mambo mbalimbali eti leo hii wameandika ''BORA WANGEINGIA FAINALI UJERUMANI''...
Dah kauli hiyo imenisononesha sana na kuamini kuwa sio woote watakaoita ''BWANA'' basi watauona ufalme wa Mbinguni...
All in all Hongera Gutierez hongera Mamammia na washabiki woote walioanza na Spain na wamemaliza na Spain...
Hakika mmenishikisha Adabu.
Kwa niaba ya fundi mitambo Obby Mwambungu... Ndugu zangu Companero na Myao wa Tunduru tunasema hongereni Spain, mmecheza vizuri na mmestahili ushindi.
Kutoka hapa somewhere unknown ni mimi Shabiki nguli na muumini wa Soka la Italia Gang Chomba sina la ziada nawarudisheni Studio Pugu Road kwake Nadhir Mayoka kwa ajili ya matangazo Mengine.
well said GC forza Azzuri