EU yaivimbia Marekani huku ikiilinda Irani kibiashara

EU yaivimbia Marekani huku ikiilinda Irani kibiashara

Mpaka Sasa kampuni kubwa za Ulaya zimesitisha kufanya shughuli na Iran mfano Total,Airbus(imesitisha Oda ya Ndege) na kampuni nyingine ya Italia nayo imesitisha oda ya Ndege (jina limenitoka). Hizo kampuni haziwezi kuacha soko kubwa la Marekani wakimbilie la Iran, HAIWEZEKANI.

Anachofanya EU ni kujaribu kuitia moyo Iran ila kiukweli hamna kikubwa watakachofanya kuizuia Marekani kuibinya Iran ukizingatia kwa Sasa chumi za EU haziko vizuri ukilinganisha na Marekani ambayo pia inajitegemea kwa nishati hivyo haitaathirika kwa kiasi kikubwa.
 
Mkuu Malcolm lumumba nimekuwa interested na hiyo SWIFT issue ya money transfer. Kuna mahali nilisoma kuwa China, anataka kuanza kununua mafuta bila kutumia dola za Marekani. Pia BRICS wana mpango Wa kuanzisha benki zao kushindana na IMF na Word bank ambazo ni himaya za Marekani. Naomba wewe au Mjuzi yeyote anielimishe, hivi hayo yakifanyka bado Marekani atakuwana mwanya Wa kuchezea wenzake? Hata Uingereza waligusia kusupport biashara bila kutumia dola ya Marekani, Hapo itakuwaje maana uchumi Wa Marekani sa sa hivi ni%22.5 hadi 25% ya uchumi wa dunia, atawezaji kuchezea 75% ya uchumi Wa wengine wrote wakiungana li dola lake waliache maananasikia dola inamiliki 75 % ya money international trade , Tafadhali tuelimishane hapo.
 
Mafuta marekani hawezi chimba Syria,kwa sababu Yale mapipeline yanaelekea maeneo alipo Assad,ndo sababu uchimbaji wa visima vya Der a zor ulisimama,hats wakisema waweke pipeline kuelekea Iraq,itachukua mda,halafu Iraq iko chini ya Iran.
Wakisema wapitie uturuki,waturuki hawatakubali kumnufaisha mkurdi
Deir Zur ipo Chini ya Asad, ila Abukamal (oil rich region north of Euphrate ) ipo chini ya marekani na wakurd. Ofcourse logistic ya kuexport yaweza kuwa shida ila hawa jamaa wanafighit zaidi makampuni yao yawe yanachimba huko!
 
Mpaka Sasa kampuni kubwa za Ulaya zimesitisha kufanya shughuli na Iran mfano Total,Airbus(imesitisha Oda ya Ndege) na kampuni nyingine ya Italia nayo imesitisha oda ya Ndege (jina limenitoka). Hizo kampuni haziwezi kuacha soko kubwa la Marekani wakimbilie la Iran, HAIWEZEKANI.

Anachofanya EU ni kujaribu kuitia moyo Iran ila kiukweli hamna kikubwa watakachofanya kuizuia Marekani kuibinya Iran ukizingatia kwa Sasa chumi za EU haziko vizuri ukilinganisha na Marekani ambayo pia inajitegemea kwa nishati hivyo haitaathirika kwa kiasi kikubwa.
EU chochote walichoamuaga ktk kuibana US walifanikiwa, chochote kile, Euro waliweza, mabank yatakayo pambana na IMF na WB ujenzi umeanza....ujenzi wa pipi line gas ulaya nzima kutokea URUSI, ujenzi ulikuwa unaendelea kwa Kasi ulisimamishwa na EU yenyewe baada ya Urusi kuchukua Jimbo la Cremea la Ukraine, Marekani Hana ujanja kwa EU....Nusu ya uchumi wake unamilikiwa na EU....kinachojitokeza kwa Sasa baina ya EU na US Ni ujinga binafsi wa Trump na Mabepari waliyomuweka madarakani....mshirika alobaki beneti na Marekani japo nae kaanza kamchoka Trump Ni canada, lkn wakiungana BRICKS na EU kwa pamoja ktk masuala ya kibashara Marekani miezi sita tu anaomba pooo....Irani kinachomlinda na EU mikataba na ulaya wanaheshimu mikataba Trump haeshimu mikataba.....anaivunja anavyotaka yeye ndo maana wachina washaanza kutafuta masoko mapya duniani....kutegemea soko moja mchina kashituka...
 
Haha...Mkuu unasema Ulaya nzima inataka kupitisha Bomba la Gesi la Urusi wakati nchi nyingi zinapinga ikiwemo UK maana wanasema Urusi inatumia Gesi Kama bakora ya kuwachapia Ulaya kiuchumi,Labda ungesema Ujerumani kidogo ningekuelewa nayo pia kuna upinzani mkubwa kuhusu hiyo project pia US pressure. EU wanataka kupunguza kutegemea Gesi ya Urusi kwa kutafuta muuzaji mwingine ndio maana Juzi Afisa Mkuu wa Biashara wa EU alikwenda Marekani kufanya mazungumzo kuhusiana na mzozo wa kibiashara na Washington na kuahidi kwamba wataongeza kwa kiasi kikubwa ununuzi wa LNG toka US na kupunguza kutegemea ya Russia. https://www.rt.com/business/434269-eu-buy-soy-lng/

Unasema EU iungane na BRICS kupambana na Marekani,mbona unafurahisha Mkuu wakati Ulaya walishaawaambia wachina kwamba wasahau kupata sapoti toka EU kwamba ipambane na US. US na EU ni waarabu wapemba wale wanagombana mchana usiku wanapatana. https://www.rt.com/business/431774-europe-china-trade-alliance/

Trump anavunja mikataba ambayo inaonekana inaionyonya Marekani kama ule wa TPP na mengineyo. Hata sisi tungeiga mfano wa Trump tungekua mbali,angalau tungeanza kuona faida ya rasilimali zetu mfano madini ambayo yananufaisha nchi nyingine. Leo hii mchango wa madini kwenye uchumi wetu haufiki hata 15%,hii ni sawa kweli wakati tuna kila aina ya madini. Leo hii Tanzania ndo mzalishaji mkubwa wa Tanzanite lakini muuzaji mkubwa wa Tanzanite kwenye soko la Dunia ni India ikifatiwa na Kenya. https://www.jamiiforums.com/threads...-local-currency-has-depreciated-by-22.915053/

Hahaha ati nusu ya Uchumi wa US unamilikiwa na EU[emoji3]

Lamwisho kwa Sasa China hana soko kubwa analolitegemea zaidi ya Marekani na hakuna nchi ambayo anafanya nayo biashara ya mabilioni ya Dola kuipita ama kuikaribia Marekani.
http://www.worldstopexports.com/chinas-top-import-partners/
 
Marekani ndiye anayetoa fedha nyingi kununua bidhaa za mchina. Wakisimamisha biashara Leo. Marekani atakosa 130 bln toka China na mchina atakosa 600 bln toka Marekani .Mchina anafaidika zaidi kwenye biashara yao. .

Hayo ni mambo ya kisiasa tuu, kutumia tarakimu kutunishiana misuli baina ya nchi hizi mbili lakini ukweli ni kuwa wananchi wa kawaida hapa Marekani wanaponea bidhaa za China (kuanzia nguo, viatu, iphone, vyombo vya nyumbani, vifaa vya ujenzi n.k). Biashara ikisimamishwa (haitatokea), hapata kalika hapa, gharama za maisha zitaruka mara dufu na makampuni mengi makubwa kama Walmart na Home Depot yatafilisika.
 
Atafilisika kivipi mkuu ???
 
Atafilisika kivipi mkuu ???

Kufilisika kwa kukosa faida.

Biashara ni kucheza na arithmetics, Walmart wanasera yao ya "low price" sasa kama mfanyabiashara anataka kuuza bidhaa zake kwenye masupermarket yao lazima ukubali kuuza kwa gharama ndogo. Sasa ili wafanya biashara wapate faida inabidi walete bidhaa za China ili angalau wapate faida.

Nike wanafanya design ya Jordan States na kupeleka michoro China kutengenezwa kwa gharama ndogo, isiyozidi $8 (uzalishaji na usafirishaji) na kuja kuuza kwa zaidi ya $100. Kama biashara kutoka China ikifa huoni kuwa Nike nayo itatetereka? Na hii model inatumiwa na makampuni mengi sana kama Rubbernaid, Apple, mpaka GE.

Gharama za uzalishaji US zimekuwa kubwa sana kwa bidhaa ndogo ndongo zisizokuwa na thamani kubwa kutokana na labor laws na unions . Wafanya biashara waliamua kuhamishia shughuli zao kwenye nchi zisizo na sheria kali za wafanyakazi ili kuongeza faida. Miaka kumi iliyopita ilikuwa bei rahisi kuagiza steel bar kutoka China kwenda California kuliko kununua iliyofuliwa Indiana. Ndiyo maana Trump alitumia kete hiyo kuombea kura katika maeneo yaliyo athirika kwa kufa kwa viwanda vya kufua makaa ya mawe na chuma.
 
Kufilisika kwa kukosa faida.
Nike wanafanya design ya Jordan States na kupeleka michoro China kutengenezwa kwa gharama ndogo, isiyozidi $8 (uzalishaji na usafirishaji) na kuja kuuza kwa zaidi ya $100. Kama biashara kutoka China ikifa huoni kuwa Nike nayo itatetereka? Na hii model inatumiwa na makampuni mengi sana kama Rubbernaid, Apple, mpaka GE.

Anheee kumbe tatizo ni cheap labour na production cost,
Mimi nina maswali mengine hapa nataka nieleweshwe zaidi.
Mosi: Je, Marekani anaweza akahamisha viwanda vyake na kuvipeleka nje ya uchina (Corporate Inversion) kama ambavyo alifanya nchini kwake kukwepa gharama za uzalishaji tokea miaka ya 70's ???

Pili: Biashara ya kimataifa ina sehemu kuu mbili (Production of Goods and Services). Wewe umeangalia kwenye moja tu (Trade in goods), uliyoyasema hapo ni biashara ya kuuziana bidhaa ambazo tunaziona. Je, vipi kuhusu biashara ya huduma (Trade in Services) ??? Marekani amejiimarisha kwenye vyote viwili (Trade in goods and services), vipi kuhusu Uchina kwenye Trade in Services ??? Siku vita ya kibiashara imewaumiza wote unadhani na viwanda vimegoma unadhani Uchina anaweza kuuza huduma nje ya mipaka yake kama Marekani na kuendelea kupata pesa ???

NB: Marekania anauza huduma (Trade in Services) kuliko nchi yoyote ile kuanzia Burudani, Habari, Mitandao ya Kijamii na Mitandano kwa ujumla, Huduma za kifedha n.k hivyo tusisahau kwamba biashara kwake ina sura mbili.

Tatu: Tukija kwenye swala zima la Nishati. Siku Mambo yameenda vibaya pale Ghuba ya Uajemi unadhania Uchina asiye na Ulinzi wa Kinishati (Energy Security) anaweza kuendesha nchi yake kirahisi ??? Maana ninavyofahamu mimi kwamba Uchina anategemea sana mafuta kutoka ghuba ya uajemi (The Persian Gulf) isitoshe yeye ndiyo nchi yenye Vifaa vya moto na viwanda vingi nyingi hapa duniani. Vipi mafuta yakipanda bei, nani ataumia sana ???

NB: Juzi amalalamika kwamba Saudi Arabia wanapandisha mafuta bei ya mafuta kiholela. Sasa itokee vurugu pale Mashariki ya Kati na mafuta yasizalishwe kama inavyotegemewa unahisi Uchina atapona kweli ??? Marekani mpaka mwaka jana ndiyo nchi ya kwanza kuzalisha mafuta hapa duniani kutoka ndani kwake. Unahisi hii vita atakayeumia sana ni nani labda ???
 
Kwa vyovyote Marekani bado ni mbabe in one way or another lakini tukubaliane kuwa hana uwezo Wa kununua dunia yote kama anavyotaka uliumwengu uamini. Sema tu BRICS hawajakaa sawa. Lakini wakianzisha benki zao na mrusi na Iran wakaiuzia China mafuta bila kutmia sarafu ya dola basi usishangae Marekani akayumba sana ..Kama ikitokea Saudi rabia akajiunga kuisusia dola ya Marekani isiwe ndio lazima wakuuzie mafuta basi haidhuru atashika adabu ,tatizo Saudia wafalme ni vibaraka mno Wa Marekani. Kitu ambacho sielewi Venezuela ameyumbaje mbona ana akiba kubwa ya mafuta kuliko hata Saudia au mchina ameshaambiwa usithubutu kununua mafuta uani kwetu tutasusia bidhaa zako,? Somo LA Venezuela mwenye reserve ya 300 bbl kushinda hata Saudia mwenye reserve ya 250 bbl oil. Naomba mwenye kujua anielimishe. Wakatiwingine najiuliza Venezuela ya Hugo Chavez ambaye nasikia walimpandkizia cancer baada ya kuwa ngangari. ( Castro kabla ya kifo chake aliwaambia Marekani siku hizi ana teknolojia ya kupandikza cancer kwa kumtarget kiongozi anapohutubia ndio maana south America wameishaugua cancer marais sits ndani ya miaka kumi na wotewalikuwa marais wazalendo wakipinga kuburuzwa na US. Hivi sisi wadogo tutafurukuta kweili? ) Venezuela inaweza kuwa a failed state kama somalia na utajiri ule ? Kwanini matafa kama China na mrusi hawamuokoi? Hivi ili mambo yako yawe mazuri shurti Marekani akusapoti? Tujadii tafadhali.
 
Kwa vyovyote Marekani bado ni mbabe in one way or another lakini tukubaliane kuwa hana uwezo Wa kununua dunia yote kama anavyotaka uliumwengu uamini.

Mkuu Myovozi huwezi kununua dunia nzima lakini unaweza ukawa mbele ya wenzako wote katika ushawishi. Unachohitaji ni kukamata vitu ambavyo dunia nzima inahitaji (Common Goods) pamoja na kujenga ushawishi katika maeneo muhimu ya kimkakati (Building Strategic Influence). Professor John Mearsheimer anasema hivi, chanzo cha nguvu ya Marekani kimkakati ni sehemu hizi zifuatazo, ambazo ukimpiga lazima atetereke:
1. The Western Hemisphere
2. The Persian Gulf
3. The European Continent
4. The Pacific

The Western Hemisphere ndiyo nyumbani kwa Marekani ambako anaishi. Tangia anapata Uhuru mwaka 1776 aligundua kwamba kama ataweza kuwafanya maadui wake wasifike kwenye huu ukanda basi atakuwa ana nafasi kubwa sana kupigana vita na adui huko mbali na hata kama atapigwa siku zote atakuwa salama nyumbani. Raisi James Monroe alifika hadi kipindi akasema kwamba nchi yoyote itakayopeleka pua kwenye ule ukanda basi Marekani itaitangazia vita. Akenda mbali zaidi akasema kwamba hata serikali za America Kusini zikiwa vibaraka wa mataifa adui atazivamia. Leo Marekani anaionea sana Venezuela kwasababu anajua dhahiri nchi hizo zitakapokuwa na uchumi mkubwa zitamsumbua sana na atakuwa na maadui mlangoni mwake.

Kama unakumbuka jinsi ambavyo alikuwa anapindua serikali za America kusini na kuzifanyia vurugu kuanzia Guatamela mwaka 1957, Cuba mwaka 1961 (Bay of pigs) na Nicaragua miaka ya 1980's kwenye The Nicaragua Contra affair. Hii yote ni sehemu ya Sera ya James Munroe (Munroe Doctrine) kupunguza upinzani nyumbani. Hivyo Uchina kukatazia kununua mafuta Venezuela na mkakati kwasababu mafuta yanalipa sana sanaa na Venezuela ikianza kuuza mafuta itakuwa tajiri ndani ya muda mfupi kweli.

The Persian Gulf (Ghuba ya Uajemi) ndiyo lilikuwa bakuli kubwa la uchumi wa Marekani kipindi chote cha Vita Baridi. Mafuta ya wale waarabu ndiyo yalifanya Marekani kuwa na sauti nzito hapa duniani pamoja na kueneza sera ya dola (The Dollar Diplomacy) ambayo ndiyo pesa inayotumiwa kama nyenzo kuu ya biashara za kimataifa. Mbali na kunufaisha uchumi wake Marekani pia alitumia ukanda huu kuharibu Uchumi wa Urusi ya Kisovieti baada ya Ronald Reagan kuwatia moyo waarabu wazalishe mafuta kwa wingi ili kushusha bei za mafuta katika soko la dunia. Ikumbukwe Urusi ailikuwa inategema asilimia 50% ya pato la nchi kutoka kwenye mafuta (Oil was a source of hard currency). Bei ilivyoshuka Urusi ikala kwake na nchi ikawa juu ya mawe. Upande mwingine Marekani anajua kabisa mataifa makubwa ya Ulaya na Asia (Uchina, Japan, India) yanategemea sana mafuta kutoka kwenye huu ukanda hivyo uwepo wake pale ni rungu tosha la kuweza kuzichezea hizi nchi atakavyo.

The European Continent (Ulaya Magharibi) hawa ndiyo waliokuwa matajiri wakubwa duniani kwa kipindi cha zaidi ya miaka 500. Baada ya vita ya pili ya dunia Marekani alijua kabisa kwamba wapinzani wake wakubwa kiuchumi ni Ulaya kwasababu wana teknolojia na makoloni ambayo ni chanzo cha rasilimali na pia masoko. Akaamua kuwaweka kwenye madeni mazito huku akiwaambia kwamba ili wapate mkopo lazima waacha ukoloni (The Marshall Plan and Open Door Policy). Akaenda mbali zaidi kusema kwamba mikopo yote na biashara ni lazima ziwe katika dola za kimarekani. Uingereza na ujanja wake wote ule amameliza kulipa awamu yake ya mwisho ya madeni ya vita ya pili ya dunia mwaka 2012-2013. Upande mwingine Ulaya anategemea sana Ulinzi wa Marekani kutoka kwa mataifa yenye nguvu kama Urusi. Katika matumizi (Military Expenditure) yeye ndiyo ana takwimu kubwa sana na kajaza kambi za jeshi kuanzia Ujerumani hadi Moldova (Full Spectrum Dominance).

The Pacific (Ukanda wa Pasifiki) kuna wapinzani wake wakubwa sana kibiashara na kiuchumi, isitoshe kuna masoko yake makubwa sana ambayo Uchina anayavizia. Usisahau kwamba huu ukanda ndiyo unaongoza kwa shughuli nyingi za kiuchumi majini hapa duniani ambapo takwimu za Umoja wa Mataifa zinasema zaidi ya Asilimia 50% ya bidhaa za dunia (Merchandise) hupita pale kutokea Ulaya. Meli zanaanzia Ulaya, Bahari ya Mediterania, Mfereji wa Suezi, Bahari ya Hindi, Mfereji wa Malacca, Bahari ya Uchina na kwenda Asia. Mwanajeshi moja wa Marekani alinukuliwa akisema hivi "We are obsessed with the Pacific and if the Chinese try something stupid we will fucking sail in those waters" Akasema kwamba Uchina akiwasumbua ile kambi yao ya Singapore inaweza ikatumika kufanya Blockade kwa bidhaa zinazoenda na kutoka Uchina (Very Dangerous) Kipindi chote cha Raegan Marekani alikuwa na manowari ndogo na kubwa kama 600 kwenye ule ukanda. Siku hizi anazo 300 za kisasa kabisa ambapo nyingine hazitumiki tena.

Hapa hoja ni kwamba Marekani ana msuli mkubwa kwasababu hajaujenga leo wala jana, ulijengeka kwa kipindi cha muda mrefu sana akianza na kutengeneza Uchumi kwanza. Marekani ananufaika na matumizi ya dola ya dunia kwasababu anaweza kuchapisha pesa na kujipa mikopo katika dola za Kimarekani kwa riba ndogo sana. Kama Chinese Renminbi ndiyo itaanza kutumia kama mbadala wa Dola basi nasema GOOD BYE AMERICA. Lakini mpaka Uchina afanikiwe kutupa kabisa dola ni lazima ajenge ushawishi mkubwa sana kisiasa na kiuchumi kitu ambacho bado ana safari ndefu sana kukifanya.

Kwanini inakuwa ngumu kufanya hivyo ???
Gideon Rachman anasema The Institutional Advantage of the Western Societies. Ambapo mbali na biashara kufanywa tu, huwa kunakuwa na taaisi na sheria maalumu za kimataifa ambazo zinalinda biashara hizo. Kuanzia World Trade Organisation (WTO) ambako Uchina na Marekani wote ni wanachama watiifu kabisa. Mbali na hapo kuna taasisi nyingine kubwa kama Bank ya Dunia au World Bank (Ambayo Raisi wake mara nyingi hupendekezwa na Marekani) na International Monetary Fund (Ambayo Raisi wake lazima atokee Ulaya). Sasa hivi vyombo hadi kufika hapo vilipo vilifadhiriwa na kutengenezwa na Marekani kwa makusudi ya kulinda maslahi yake binafsi. Maana hata upigaji wake kura mle ndani unalalamikiwa sana na Uchina na baadhi ya Mataifa.

Uchina ili kufanikisha mpango wake wa kutumia Chinese Renminbi itabidi atengeneze taarisi kubwa ambazo zitakuwa ambazo zitahusisha mataifa makubwa ambayo atayapa mikopo na kufanya uwekezaji kutumia sarafu yake. Amenza vizuri sana na Asia Infrastructure Investment Bank (AIIB) ambapo hadi Uingereza mwaka 2015 alijiunga nayo, kuna The Shanghai Cooperation, halafu kuna BRICS ambayo binafsi naamini inaweza kubadilisha mambo sana kama itahusisha nchi za Kiafrika na zile za Mashariki ya kati. Hivyo huwezi kuanza kutumia sarafu yako bila kuwa na taasisi Imara ambazo zitakuwa zinakushauri na pia zinawapa wadau wako wakubwa sauti ya kusema juu ya sheria na sera ambazo zinasimamia biashara na ugawanywaji wa mikopo ili kujenga Imani.

NB: Kubwa na la mwisho kuhusiana na taasisi za kimataifa, mfano mzuri ni Ufalme wa Uingereza ambapo hata baada ya kuanguka mwaka 1945-1957. Taasisi zake za kimataifa kama The Common Wealth ndizo zilimfanya awe na sauti juu ya makoloni yake na pia kwenye siasa za kimataifa. Ufalme wa Roma ulianguka lakini taasisi zake Imara zilikuwepo kuanzia The Vatican, The Holy See, The Sovereign Order of Malta zipo mpaka leo na ndiyo zimeshikilia nguvu ya Kanisa. Urusi yeye alikuwa anawaza vita tu na kufanya mapinduzi ya Kikomunisti dunia mbali na COMECON na WARSAW PACT hakujenga taasisi Imara za kiuchumi ambazo zingamsaidia kusambaza pesa yake hata baada ya yeye kuanguka kwasababu taasisi hizi zinaendeshwa kwa mikataba na siyo matakwa ya nchi peke yake.

CC: Nalendwa
 
Anheee kumbe tatizo ni cheap labour na production cost,
Mimi nina maswali mengine hapa nataka nieleweshwe zaidi.
Mosi: Je, Marekani anaweza akahamisha viwanda vyake na kuvipeleka nje ya uchina (Corporate Inversion) kama ambavyo alifanya nchini kwake kukwepa gharama za uzalishaji tokea miaka ya 70's ???

Kwa sasa hakuna nchi mbadala kama China yenye nguvukazi na teknolojia. Afrika kuna wafanyakazi lakini hamna miundombinu kama China.

Pili: Biashara ya kimataifa ina sehemu kuu mbili (Production of Goods and Services). Wewe umeangalia kwenye moja tu (Trade in goods), uliyoyasema hapo ni biashara ya kuuziana bidhaa ambazo tunaziona. Je, vipi kuhusu biashara ya huduma (Trade in Services) ??? Marekani amejiimarisha kwenye vyote viwili (Trade in goods and services),

Marekani imejikita zaidi kwenye utoaji huduma kuliko utengenezaji wa bidhaa (kama ilivyokuwa zamani ) kwasababu 'overhead' yake ni ndogo. Kwenye utoaji huduma kampuni inaweza kuongeza gharama mara dufu kuliko uhalisia na hivyo kupata faida kubwa zaidi. Hata hivyo watu bado watahitaji bidhaa kama vyombo vya nyumbani n.k. Vita ya uchumi italeta 'culture shock' Marekani kwa kuwa watu wamezoea kununua vitu kwa bei rahisi na kuvitupa (baada ya muda), sasa kama vitu hivyo vikitoka Ujerumani watu wengi watashindwa kuvinunua kutokana na gharama.

vipi kuhusu Uchina kwenye Trade in Services ??? Siku vita ya kibiashara imewaumiza wote unadhani na viwanda vimegoma unadhani Uchina anaweza kuuza huduma nje ya mipaka yake kama Marekani na kuendelea kupata pesa ???

Kampuni za China za utoaji huduma nyingi zipo China tuu japo kuwa wameanza kusambaza huduma zao za kibenki nje hasa Afrika na Asia lakini kama vita itazidi soko lao la ndani litasaidia kupunguza makali. Kumbuka China ina millionea wengi kuliko watu wote wa marekani.

NB: Marekania anauza huduma (Trade in Services) kuliko nchi yoyote ile kuanzia Burudani, Habari, Mitandao ya Kijamii na Mitandano kwa ujumla, Huduma za kifedha n.k hivyo tusisahau kwamba biashara kwake ina sura mbili.

Suala la huduma ni kweli Marekani inaongoza duniani ndiyo maana China mbali na "sensorship" wamezuia mitandao ( facebook na google ) kama njia ya kulinda makampuni yao ya utoaji huduma ndani ya nchi.

Tatu: Tukija kwenye swala zima la Nishati. Siku Mambo yameenda vibaya pale Ghuba ya Uajemi unadhania Uchina asiye na Ulinzi wa Kinishati (Energy Security) anaweza kuendesha nchi yake kirahisi ??? Maana ninavyofahamu mimi kwamba Uchina anategemea sana mafuta kutoka ghuba ya uajemi (The Persian Gulf) isitoshe yeye ndiyo nchi yenye Vifaa vya moto na viwanda vingi nyingi hapa duniani. Vipi mafuta yakipanda bei, nani ataumia sana ???

Nishati ni tatizo kwao ndiyo maana walikubaliana na warusi kujenga bomba la mafuta na juzi juzi warusi wameanza mpango wa kuleta LNG kupitia arctic kwa kutumia meli yao ya 'ice breaker' ambapo njia wanayo itumia ni fupi na kwa kiasi kikubwa inapita kwenye eneo lao (Urusi). Pia najua unafahamu vizuri kuhusu ugomvi wa 'south china sea' hiyo yote ni kujaribu kutanua wigo ili kulinda hizo trade routes.

NB: Juzi amalalamika kwamba Saudi Arabia wanapandisha mafuta bei ya mafuta kiholela. Sasa itokee vurugu pale Mashariki ya Kati na mafuta yasizalishwe kama inavyotegemewa unahisi Uchina atapona kweli ??? Marekani mpaka mwaka jana ndiyo nchi ya kwanza kuzalisha mafuta hapa duniani kutoka ndani kwake. Unahisi hii vita atakayeumia sana ni nani labda ???

Kwa hili la mafuta Marekani kapiga bao sana na hasa baada ya kugundulika kwa 'horizontal drilling', ni rahisi hata kukinukisha pale gulf ili mafuta yapande bei ili exxon mobile wafaidike. Hata hivyo kama nilivyosema hapo juu, China bado anaweza pata mafuta Urusi kwa bei nafuu.
 
Kwa sasa hakuna nchi mbadala kama China yenye nguvukazi na teknolojia. Afrika kuna wafanyakazi lakini hamna miundombinu kama China.
Hakuna mbadala wa Uchina kivipi wakati kwenye kumi bora kwa GDP kuna India ???
Halafu unavyosema hakuna mbadala wa Teknolojia, Nguvu kazi na Miundombinu unamaanisha nini ???
Kwani Uchina imeanza kuwa na miundombinu na teknolojia baada au kabla ya Marekani na mataifa mengine kuanza kuwekeza nchini mle mnamo miaka ya 1970's-1980's (Naomba jibu lenye takwimu)

Kwenye utoaji huduma kampuni inaweza kuongeza gharama mara dufu kuliko uhalisia na hivyo kupata faida kubwa zaidi.

Kwani kwenye uuzaji wa bidhaa kampuni haliwezi kuongeza gharama mara dufu kuliko uhalisia ili kupata faida zaidi ??? Au hufahamu kwamba Ubepari ni faida (Capitalism=Maximization of profit)?? Au labda mimi ndiyo sijakuelewa hapa labda ???

Kampuni za China za utoaji huduma nyingi zipo China tuu japo kuwa wameanza kusambaza huduma zao za kibenki nje hasa Afrika na Asia lakini kama vita itazidi soko lao la ndani litasaidia kupunguza makali. Kumbuka China ina millionea wengi kuliko watu wote wa marekani.

Tafadhali naomba unipe mfano wa hayo makampuni mengi ya Uchina ambayo yanafanya kazi Afrika na dunia nzima kwa ujumla. Unisaidie na idadi za wateja wake pamoja na faida wanazopata, halafu na mimi nitakueletea takwimu zangu za makampuni ya Marekani, wateja wake na faida zao.

Suala la huduma ni kweli Marekani inaongoza duniani ndiyo maana China mbali na "sensorship" wamezuia mitandao ( facebook na google ) kama njia ya kulinda makampuni yao ya utoaji huduma ndani ya nchi.

Kitendo cha kuzuia makampuni ya Marekani (Protectionism) ni kukubali kabisa kwamba makampuni ya Marekani yana nguvu na yanatoa huduma nzuri kuliko yale ya Uchina. Mbona Marekani hajakataza makampuni ya Uchina kuuza huduma nchini kwake ??? (Hili umejiuliza kweli ???)

Nishati ni tatizo kwao ndiyo maana walikubaliana na warusi kujenga bomba la mafuta na juzi juzi warusi wameanza mpango wa kuleta LNG kupitia arctic kwa kutumia meli yao ya 'ice breaker' ambapo njia wanayo itumia ni fupi na kwa kiasi kikubwa inapita kwenye eneo lao (Urusi). Pia najua unafahamu vizuri kuhusu ugomvi wa 'south china sea' hiyo yote ni kujaribu kutanua wigo ili kulinda hizo trade routes.

Hivi unajua Uchina amenunua gesi ya Urusi kupitia GAZPROM chini ya bei ya sokoni (Below the Market Price) ??? Umejiuliza kwanini Urusi amekubali baada ya vikwazo na hukukubali miaka yote ya nyuma ambapo Uchina alikuwa anaomba auziwe gesi ??? (Kunani hapa ???)

Kwa hili la mafuta Marekani kapiga bao sana na hasa baada ya kugundulika kwa 'horizontal drilling', ni rahisi hata kukinukisha pale gulf ili mafuta yapande bei ili exxon mobile wafaidike. Hata hivyo kama nilivyosema hapo juu, China bado anaweza pata mafuta Urusi kwa bei nafuu
.

Unafahamu madhara ya kisiasa (Political Implications) yanayoweza kutokea endapo Uchina atakuwa tegemezi kwa mafuta na gesi ya Urusi ??? Au unasahau ambacho Ulaya wanafanywa na Urusi linapokuja suala la mafuta na gesi ???
 
Mkuu Malcolm lumumba nimekuwa interested na hiyo SWIFT issue ya money transfer. Kuna mahali nilisoma kuwa China, anataka kuanza kununua mafuta bila kutumia dola za Marekani. Pia BRICS wana mpango Wa kuanzisha benki zao kushindana na IMF na Word bank ambazo ni himaya za Marekani. Naomba wewe au Mjuzi yeyote anielimishe, hivi hayo yakifanyka bado Marekani atakuwana mwanya Wa kuchezea wenzake? Hata Uingereza waligusia kusupport biashara bila kutumia dola ya Marekani, Hapo itakuwaje maana uchumi Wa Marekani sa sa hivi ni%22.5 hadi 25% ya uchumi wa dunia, atawezaji kuchezea 75% ya uchumi Wa wengine wrote wakiungana li dola lake waliache maananasikia dola inamiliki 75 % ya money international trade , Tafadhali tuelimishane hapo.

Mkuu Muyovozi sikuuona huu uzi, lakini yote nimeshakujibu kwenye uzi wangu namba #51. Kama Uchina akifanikiwa kutumia Chinese Renminbi kama International Currency Reserve basi Marekani itakula kwake kwa kiasi kikubwa sana. Lakini bado mpaka Uchina kufika huko inabidi ajenge taasisi za kimataifa Imara sana zenye kuaminika kama zile za mabepari (Bretton Woods Institutions) za IMF na WB.

Japo sasa, Marekani hata kama akianguka kitakachomtesa sana ni madeni kwasababu deni lake halilipiki kirahisi na itambidi abane sana matumizi ili kufanikisha kulipa madeni ya nje kama ambavyo anafanya Japan leo hii. Lakini hata akianguka bado anaweza kuwa taifa tajiri sana sana hapa duniani kwasababu yeye ni nchi ya pili kuwa na rasilimali nyingi baada ya Urusi. Ana rasilimali zenye thamani ya Trillion 45 USD: Hapo hujagusia idadi ya watu na teknolojia.

Ndiyo maana Professor Alisson Graham aliwahi kusema kwamba Marekani ili ibaki pazuri inahitaji sana kukaa mezani na Uchina na kukubaliana sehemu gani washirikiane na sehemu gani washindane. Maana mpaka Uchina ilipofika sidhani kama kuna mtu anaweza kuwazuia wasipande na kuwa wa kwanza kiuchumi. Maana mpaka mwaka 2014 IMF iliwatangaza kwamba wao ndiyo nchi yenye Uchumi mkubwa katika nguvu ya ulinganifu wa manunuzi (Purchasing Power Parity A.K.A PPP) nafasi ambayo Marekani aliishikilia tokea mwaka 1872 (This is just dangerous kwa Marekani)
 
EU imekataa kuidhinisha vikwazo dhidi ya Irani vilivyowekwa kibabe na US. Na EU imesema makampuni yake hayataguswa na mashinikizo ya vikwazo vya US kwa mwamvuli wa EU. Kuonyesha wameivimbia kweli kweli wame'washa' na wataanza ku'puliza' kitu kinaitwa 'Blocking Statute' kesho. Hii kitu inakinga makampuni ya EU na bughudha za Marekani katika biashara zao. Maelezo ya Kina haya hapa chini
====
The European Union is enforcing the so-called Blocking Statute to protects its firms operating in Iran from the looming US sanctions against the country.
The first round of renewed US sanctions will take effect on Tuesday after midnight US Eastern time with the harshest sanctions expected to return in early November.
The European Commission has stated that despite US sanctions, European companies will continue doing legal business in Iran under the protection from Brussels.
“The lifting of nuclear-related sanctions is an essential part of the deal – it aims at having a positive impact not only on trade and economic relations with Iran, but most importantly on the lives of the Iranian people. We are determined to protect European economic operators engaged in legitimate business with Iran, in accordance with EU law and with UN Security Council resolution 2231,” the European Commission stated on Monday.
"This is why the European Union’s updated Blocking Statute enters into force on 7 August to protect EU companies doing legitimate business with Iran from the impact of US extra-territorial sanctions," it added.
Brussels announced back in May that it would enable the Blocking Statute starting from August. The law was first adopted in 1996 and forbids EU companies from complying with the extraterritorial effects of US sanctions. It allows companies to recover damages arising from such sanctions, and nullifies the effect in the EU of any foreign court judgements based on them.

EU blocking US sanctions against Iran to protect European companies
---
Update
====
Kumetokea mlipuko mkuwa Bologna, Italy. Italy ni mwanachama wa EU

https://www.rt.com/news/435214-bologna-airport-explosion-videos/
https://www.rt.com/business/435306-eu-us-iran-sanctions/
 
Mchambuzi wa maswala ya Uchumi umoja wa ulaya.EU amesema ulaya haina ubavu wa kupinga vikwazo vya marekani.ulaya inabidi ichague faida kubwa iko wapi.kufanya biashara na Iran au marekani.
IMG_20180806_064322_273.JPG
 
Kwa vyovyote Marekani bado ni mbabe in one way or another lakini tukubaliane kuwa hana uwezo Wa kununua dunia yote kama anavyotaka uliumwengu uamini. Sema tu BRICS hawajakaa sawa. Lakini wakianzisha benki zao na mrusi na Iran wakaiuzia China mafuta bila kutmia sarafu ya dola basi usishangae Marekani akayumba sana ..Kama ikitokea Saudi rabia akajiunga kuisusia dola ya Marekani isiwe ndio lazima wakuuzie mafuta basi haidhuru atashika adabu ,tatizo Saudia wafalme ni vibaraka mno Wa Marekani. Kitu ambacho sielewi Venezuela ameyumbaje mbona ana akiba kubwa ya mafuta kuliko hata Saudia au mchina ameshaambiwa usithubutu kununua mafuta uani kwetu tutasusia bidhaa zako,? Somo LA Venezuela mwenye reserve ya 300 bbl kushinda hata Saudia mwenye reserve ya 250 bbl oil. Naomba mwenye kujua anielimishe. Wakatiwingine najiuliza Venezuela ya Hugo Chavez ambaye nasikia walimpandkizia cancer baada ya kuwa ngangari. ( Castro kabla ya kifo chake aliwaambia Marekani siku hizi ana teknolojia ya kupandikza cancer kwa kumtarget kiongozi anapohutubia ndio maana south America wameishaugua cancer marais sits ndani ya miaka kumi na wotewalikuwa marais wazalendo wakipinga kuburuzwa na US. Hivi sisi wadogo tutafurukuta kweili? ) Venezuela inaweza kuwa a failed state kama somalia na utajiri ule ? Kwanini matafa kama China na mrusi hawamuokoi? Hivi ili mambo yako yawe mazuri shurti Marekani akusapoti? Tujadii tafadhali.
Venezuela ilichosababisha ianguke ni Sera mbaya kwa mujibu wa watu wa magharibi. Kipindi cha Chavez alikuwa ameweka bei ndogo kwa huduma za afya na chakula. Kwa hiyo wote waluokuwa wanafanya biashara venezuela wakalazimishwa kufuata ivo. Ikapelekea makampuni kupata hasara. Wakaondoka. Ikapelejea uhaba wa bidhaa. Uhaba wa bidhaa ukaleta mfumuko wa bei.

Pia kipindi hicho hicho bei ya mafuta ikawa imeshuka. Serikali ikawa imekosa mapato yake muhimubya kuweza kuendesha serikali.
Ikabidi serikali ichapishe pesa nyingi ili kuweza kuendesha serikali na kulipa madeni.
Hii ikasababisha mfumuko mkubwa wa bei maana kulikuwa hakuna uzalishaji na uhitaji wa bidhaa ni mkubwa kukiko upatikanaji wake.
Uchumi wa venezuela unategemea mafuta na Sasa amewekewa vikwazo.
 
Hakuna mbadala wa Uchina kivipi wakati kwenye kumi bora kwa GDP kuna India ???
Halafu unavyosema hakuna mbadala wa Teknolojia, Nguvu kazi na Miundombinu unamaanisha nini ???

Kwani Uchina imeanza kuwa na miundombinu na teknolojia baada au kabla ya Marekani na mataifa mengine kuanza kuwekeza nchini mle mnamo miaka ya 1970's-1980's (Naomba jibu lenye takwimu)

Nilimaanisha kwa sasa hakuna nchi nyingine yenye advantage ya vitu vyote hivyo kwa mpigo kama viwanda, miundombinu na cheap labor kama China. Marekani ina vyote hivyo kasoro cheap labor.

Kwani kwenye uuzaji wa bidhaa kampuni haliwezi kuongeza gharama mara dufu kuliko uhalisia ili kupata faida zaidi ??? Au hufahamu kwamba Ubepari ni faida (Capitalism=Maximization of profit)?? Au labda mimi ndiyo sijakuelewa hapa labda ???

Ni vigumu kumshawishi mteja kulipia gharama kubwa kwa bidhaa ndogo kuliko kufanya hivyo kwenye kutoa huduma. Mfano, ni vigumu kumwambia mteja alipie bidhaa ya simu kila mwezi lakini ni rahisi kufanya hivyo kulipia huduma ya bando. Bidhaa usiyoishika (huduma) inakuwa ni mystery hivyo unaweza weka bei yoyote na mtu akaikubali.

Tafadhali naomba unipe mfano wa hayo makampuni mengi ya Uchina ambayo yanafanya kazi Afrika na dunia nzima kwa ujumla. Unisaidie na idadi za wateja wake pamoja na faida wanazopata, halafu na mimi nitakueletea takwimu zangu za makampuni ya Marekani, wateja wake na faida zao.

Hapa hujanisoma vizuri, nilisema makampuni yao ya huduma yapo China japokuwa wameanza kutoa huduma za benki nje, mfano Bank of china kule J'berg.

Kitendo cha kuzuia makampuni ya Marekani (Protectionism) ni kukubali kabisa kwamba makampuni ya Marekani yana nguvu na yanatoa huduma nzuri kuliko yale ya Uchina. Mbona Marekani hajakataza makampuni ya Uchina kuuza huduma nchini kwake ??? (Hili umejiuliza kweli ???)

Hakuna mahali nimekataa nguvu ya makampuni ya Marekani, nafahamu pia nguvu ya petrodollar ambayo inayapa makampuni hayo nguvu kubwa indirectly. Japokuwa kuna uhuru wa kibiashara lakini siasa bado inashika hatamu, siyo makampuni yote ya nje yanaruhusiwa kuleta bidhaa, mfano makampuni ya magari ya china hayaruhusiwi kuuza Marekani.

Hivi unajua Uchina amenunua gesi ya Urusi kupitia GAZPROM chini ya bei ya sokoni (Below the Market Price) ??? Umejiuliza kwanini Urusi amekubali baada ya vikwazo na hukukubali miaka yote ya nyuma ambapo Uchina alikuwa anaomba auziwe gesi ??? (Kunani hapa ???)

Bei ya mafuta ilishuka sana na hivyo demand kupungua sasa hawa jamaa wakakubaliana kuuziana kwa kutumia petroyuan ili kuanza kupunguza nguvu ya petrodollar.
Unafahamu madhara ya kisiasa (Political Implications) yanayoweza kutokea endapo Uchina atakuwa tegemezi kwa mafuta na gesi ya Urusi ??? Au unasahau ambacho Ulaya wanafanywa na Urusi linapokuja suala la mafuta na gesi ???
Naelewa sana Kuhusu hilo lakini Urusi na China ni washirika na wanahistoria ndefu tofauti na ilivyo kwa nchi za Ulaya magharibi.
 
Back
Top Bottom