Lisa waswahili wana msemo wao maarufu kwamba penda unapopendwa, ukipenda usipopendwa utakufa kabla ya siku zako.Hiyo ni kweli kabisa kaka Mtambuzi, Ndiyo maana mm huwa nakataa moja kwa moja, maana kuna wanaume wengine ukimuonjesha tu , lazima ataulizia tena, na ukimwambia hapana Anakwambia mbona siku ile ulinipa, na ukimwambia nilikupa mara moja tu anakwambia anataka tena , Sasa ubaya awe ndiyo boss wako, ameitaka tena na wewe umekataa utaona Rangi zote hapo ofisini, atakufanyia visa mpk utampa tena. Ndiyo maana mm huwa nakataa kabisa tangu mwanzo kama ni hapana ni hapana na sibadilishi mtizamo.
MM NILIOLEWA NA MWANAUME AMBAYE SIKUMTEGEMEA KUWA MUME WANGU , ALIDAI YEYE ANATAKA KUONJA TU,KUMBE ALIKUWA AMENIPENDA ANATAKA KUNIACHANISHA NA MCHUMBA WANGU, BASI ALIFANYA HILA MPK YULE MCHUMBA AKAJUA. NDIPO NIKAWA SINA PA KUSHIKA IKABIDI NIMKUBALI YEYE AWE MUME.
Aliachana au aliachwa? Fafanua pls kwani hiyo ni muhimu sana; na inaweza kutupa picha kuwa alimpenda KWELI au aliFIKIRI anampenda.
Nina assume aliachwa na huyo mdada baada ya kusalitiwa.
haya anavyonisimulia hayo, na kutoonesha kutojuta ina maana 2 na naweza chagua nini cha kuamini inategemea ameuteka moyo wangu kiasi gani.
1. Hajutii mahusiano yake yote ya nyuma coz yuko na mimi and he is happy with me; na naweza chukulia cheating yake ilikuwa ni searching for something missing ambacho amekuja pata kwangu at last. AU
2. He is a self centered cheating bast.rd ambaye hajali feelings za wengine na hafai kuwa na mimi. (hii conclusion itakuwa supported na matendo yake na jinsi anavyonitreat na hata ile ya juu pia inakuwa supported and how he is now)
Nicole, naona kama hututendei haki maana kusema wanaume wote wa KiTZ mama yao mmoja ni kutukosea.mbona hizo kauli za kawaida sana kwa wanaume wa kitz??
mie nitaichukulia poa na wala sitoshangaa, kwani najua wanaume mama yao mmoja..............
kama aliweza msaliti mpenzi wake aliyempenda sana uwezekano wa kunisaliti hata mie upo kwa zaidi ya 200%...hilo liko wazi
uamuzi wa ama nijitoe ama niendelee na huo uhusiano unategemea na mtu mwenyewe kwa wakati huo na ni kipi hasa kilinifanya nikawa na relation naye........
Kaunga au umesoma kinyumenyume?
Hivi kama mwanaume anaku treat vizuri ina maana ndio hato cheat? (Hebu tuliache hili maana tutafungua mjadala mwingine)
Hapo juu nimeeleza wazi kwamba huyo mwanaume ni wa ndoto zako na ana karibu kila kitu ulichohitaji mwanaume wa ndoto zako awe nacho.
Sasa inatokea katika mazungumzo yenu ya kawaida siku moja anakusimulia kuhusu mahusiano yake yaliyowahi kuvunjika kutokana na kumsaliti huyo mpenzi wake aliyempenda sana. iwe ameachwa au amemuacha, bado haibadili ukweli kwamba alimsaliti huyo mpenzi wake.
Point yangu ni kutaka kujua maoni yenu baada ya kuwa umeshafahamu kuwa huyu mwanaume aliwahi kumcheat mpenzi wake anayedai alimpenda sana huko nyuma.
Je hii dhana ya muonja asali haonji mara moja ina nafasi kwako/kwenu ninyi kina dada/mama?
hahahahah Mtambuzi bana, niombe radhi kwa lipi?? kusema ukweli?? ukweli unauma siku zote.....men are the same all over the world hawana exception...
Ha ha ha ha haaaaaa........ Nicole lakini hao wanaume ndio wanaowaoeni.......
Naomba tu ukubali kwamba tunatofautiana sana, kwa hiyo kutupa sifa moja wote kwa ujumla wetu ni kumkosea heshima hata baba yako.
Hebu omba radhi bana.
:confused2::A S-confused1::A S check_03:mbona hiyo kauli nzuri sana nilishakutana nahuyu akaniambia hivi
1.nilishatembea na wanawake wasiopungua 100 na ushee ila katika wote hao nawapenda watano na katika hao watano jack na neema ndio naweza kuja kuwaoa alafu wewe uliyempenzi wake wa muda huo hajakutaja.
2 .unamwambia jamani mbona uko na mimi lakini bado unaendelea kuwasiliana na ma X -WAKO NA SIO MMJA AU WAWILI ANAKUAMBIA '',WANAMKE HAACHWI ILA ANAPUNGUZIWA MAWASILIANO TU''na kweli akienda popote anatembea na x-wake
3.Anakuwa na wanawake wengi kila kona inakuwa sio siri tena na wengine amezaa nao ni wengi kama kumi na wote anadili nao wazazi wanamkalisha nakumkanya anajibu''KHA SASA NIMEJITAHIDI SANA YAANI NIMEPUNGUZA IDADI YAO KUTOKA 20 SASA NIMEBAKI NA 12 TU AMBAO NAWAPENDA ''''' HAHAHAH Mtambuzi najua umenielewa sana.
Nyamayao hilo lililokukuta limewakuta wengi sana. Bila shaka baada ya kudakwa hukupoteza muda kuangalia yaliyopita bali ulijikita na huyo aliyekudaka.X alieniachaga alikuwaga busy sana na mawasiliano na x wake, nikamuulizaga hivi mbona upo busy sana na mawasiliano na huyo mdada wakati ulishaniambia hutaki hata kumsikia? nikaambiwa "nahisi kuna kitu namiss kwake" sikusomaga alama za nyakati,kumbe ndio nilikuwa naachwa hivyo,walisharudiana, mie nikamwagwa, mbeleni mdada akaja kummwaga akashika kitu kinachoeleweka, kurudi kwangu akakuta nshadakwa.