Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,809
- 15,441
Upo msemo kuwa muonja asali haonji mara moja, na msemo huo hutumiwa sana kuwaelezea wanaume wanaowasaliti wenzi wao kwamba, hata wakifumaniwa, ipo siku watarudia tena.
Niliwahi kujadili jambo hilo humu wakati fulani, kama ungependa kujikumbusha unaweza kubofya hapa chini:
https://www.jamiiforums.com/mahusia...waonji-mara-moja%85%85%85%85%85%85%85%85.html
Leo nina swali kwa dada zangu wa hapa JF:
Tuchukulie kwamba, unaye mpenzi ambaye mmependana sana, ni mwanaume wa ndoto zako, ana karibu sifa zote za mwanaume uliyekuwa unamuhitaji.
Inatokea siku moja katika mazungumzo yako na huyo mwenzi wako kuhusu mahusiano yake ya nyuma anakiri kwamba, wakati fulani aliwahi kuachana na mpenzi wake aliyempenda sana baada ya kumsaliti huyo mpenzi wake na mwanamke mwingine. Anazungumza hivyo bila kuonyesha hisia za kujutia kitendo chake hicho.
Hebu niambie,
1. Je utaichukuliaje kauli yake hiyo?
2. Kama aliweza kumsaliti mpenzi wake aliyempenda sana, je hudhani kuwa hata wewe anaweza kukusaliti siku moja?
3. Je utaamua kujiondoa mapema katika huo uhusiano au utaendelea na uhusiano huo kwa ile dhana kwamba yaliyopita si ndwele?
Hebu kina dada fungukeni hapa.............