1. Ukimsomesha Mchumba wako(Mwanamke), huta muoa. Akifika Chuo kikuu anachagua Mwanamme Mwingine.
2. Hata ukimsomesha Mkeo, akipata elimu atakufanyia vituko muacheni atafute Mume Mwengine.
3. Ukitaka kuoa Mwanamke msomi, Oa mwanamke alie someshwa na Wazazi wake.
Yani hapo sitii neno, kuna msanii mmoja aliyaona hayo!
Artist: Freshly Mwamburi
Song: Stella Wangu
nilikuwa na mchumba wangu
tulipendana kama nyama choma
alibahatika kwenda ng'ambo
chuo kikuu kwenda kusoma
miaka mitatu kule Japani
kusomea udaktari
Stella wangu eeh
nilivyompenda Stella jamani
nikajitolea kwa roho moja
nikauza shamba langu
sababu yake yeye
nikauza gari langu
sababu yake yeye
nikauza ng'ombe na mbuzi
sababu yake yeye
ili apate nauli
na pesa zingine za matumizi
huko Japani
ilikuwa tarehe kumi na saba
mwezi wa tano
ilikuwa tarehe kumi na saba
mwezi wa tano
mwaka elfu moja tisa mia
tisaini na mbili
ndio ilikuwa tarehe kamili
ya Stella kurudi Kenya
nilikwenda uwanja wa ndege
ndio kumlaki Stella
nilikuwa na Uncle Kilinda
kwa uwanja wa ndege
nilikuwa na Basilima Mulomba
na mkewe na mtoto wake
nilikuwa na Uncle Mjomba
mtoto wa Mombasa
ghafla ndege ilipotua tuliona vituko
Stella alishuka amebeba
mtoto mikononi
nyuma yake mchumba wake mfupi
futi nne Mjapani
nilisikitika ndani ya moyo
nikakosa la kufanya
nilitamani nilie kikamba
lakini sikijui
ilinibidi nilie kijaluo
amatima ngoa choa
Freshly
nilitamani nilie kihindi
lakini sikijui
ilinibidi nilie kitaita
lugha ya baba na mama
ilinibidi nilie kitaita
iki mwana niponye vala
Freshly
...