Eti "Mi sitaki kuchezewa"

Eti "Mi sitaki kuchezewa"

Ni kweli dear..bora nusu shari kuliko shari kamili..bur serious mie sipendi kuchezewa...Na hawa wanaume usiwatete sana wanapenda sana kuchezea wanawake..nina ushahidi... Tatizo na sie wanawake ni wajinga sana sometimes..

Unaongea kama vile wanawake wote ni malaika na hawapo ambao wanachezea wanaume. SMH in disbelief!!!
 
Unaongea kama vile wanawake wote ni malaika na hawapo ambao wanachezea wanaume. SMH in disbelief!!!
Noop..Ndio maana nimesema mie sipendi...wapo wanawake wenzangu hata hapa jf wanawachezea wanaume mazoba..au tuseme wanachezeana...ngoma droo
 
tatizo wanaume wengi wanajua wakishakukwida huna ujanja hata akikunyea mdomoni uitakaa nae tu... Hawajui maisha ni zaidi ya hiyo k aloigusa! Ni ujinga kujilazimisha kwa mwanaume ambae hafai kimaisha kisa tu amekugusa! Sex ni kitu gani hata sisimizi wameguswa

hah..!!
 
Noop..Ndio maana nimesema mie sipendi...wapo wanawake wenzangu hata hapa jf wanawachezea wanaume mazoba..au tuseme wanachezeana...ngoma droo

Wanaume mazoba ndiyo wakoje na nini kinakufanya uwaite wao mazoba? Na kama wanachezeana itakuwaje mmoja awe zoba peke yake na mwenzake asiwe zoba?
 
kwa kweli kwenye mahusiano kuchezewa c lazima uwe umefanya mapenzi na mtu ishu kubwa ni comitment kwa mtu flani ukamwamini yeye kumbe bado yupo labaratory anaendelea test, hii inapendeza tuambiane mapema mwenzangu me hapa napita tu, kama shida ni sex muenjoy kila mtu aishie.
 
Nyani ngabu nawe mhanga nini, ila mi napenda nikute mwanaume amechezewa kwa kweli coz wamezidi
 
Katika vitu ambavyo huwa vinanipa shida kuvielewa ni hili neno la kuchezewa.
"
Binadamu mwenye akili timamu anachezewaje?
"
Kwanza kuchezewa ni nini?Ni kufanya nini?
"
Kama ni kufanya mapenzi,si mnafanya wote?Kwa hiyo mnachezeana.
"
Wanawake waache kuuendeleza msemo huu!


Eiyer ninapokosoana na wewe ni kwenye generalization tu, hivi kwann mdogoi wangu umekimbilia kusema wananwake waache kutumia msemo huu?? hiovi wanaume wanaolalamika kupotezewa muda naoa je utawasemaje?? ama wadada ambao walisain mkataba wa kuoana kisha wakamegwa na kuachwa nao pia wasemeje kama si kuchezewa huko?? to be fair kama mdada alikwambia anataka ndoa na ukamlala kisha kumuacha basi umemchezea tu manake ungemwacha angepata ambaye ange-bid kwa namna hiyo.

tatizo nilionalo hapa bidders wengi huja na document ambazo ziko kinyume na yule aliyetangaza tenda na hapo ndipo ishu za kuchezeana hutokea.
 
Last edited by a moderator:
Unaongea kama vile wanawake wote ni malaika na hawapo ambao wanachezea wanaume. SMH in disbelief!!!

Tena kwa staili za kutafuna mazawadi mengi ya gharama na outing za kutosha!akishakumaliza anaolewa na mwingine, baadae utasikie alinikuwa ananichezea tuu!
 
GAZETI inaonyesha we ni noma hapo mtaani na dada kakushtukia, if NOT mbona hujamfuat na badala yake umekimbilia huku JF.
 
Wanaume mazoba ndiyo wakoje na nini kinakufanya uwaite wao mazoba? Na kama wanachezeana itakuwaje mmoja awe zoba peke yake na mwenzake asiwe zoba?
Dah..dont tell me hujui kuna mazoba na mazombie....Ni wale ATMs..Baadhi ya wanawake huwa wanakuwa na wanaume kam 3 au 4..
1.. Sharobaro aka handsome muuza sura wa kujidai
2.. Atm aka provider aka mgodi
3.. Wa kumfikisha
4..Wa future kama kuoana nk
5 ...Kuna wengine wanao wa akiba kama plans nyingine zikifeli
 
my hubby wangu eiyer, kuchezewa kunakujaje, unapomuahidi mdada kuwa utamuoa (umemu-engage so umemfunga) na ukamuomba mfanye mapenzi (yeye akiwa hajaridhia) na akakubali kwa kuwa utamuoa; wakati from the very beginning unajua hutamuoa na kuja kumtelekeza baadaye. Huyo dada ana haki ya kusema amechezewa.
Kosa la huyo dada ni kutosimamia imani yake, kumbuka hakuwa radhi kufanya mapenzi ni umemshawishi kwa ahadi!

Lakini kwa scenario nyingine ambapo, mmepenndana na mdada na wote mmeridhia kufanya mapenzi na kwenye course ya mapenzi yenu mkaahidiana kuoana. Ukija kuacha kumuoa, au naye akibadili mtazamo mnakuwa mmepotezeana muda (kwani kutengeneza uchumba takes time), na hakuna mtu kamchezea mwenzake.

Wadada wengi huangukia kwenye kundi hilo la pili, lakini as you say wanasema wamechezewa which is very wrong imo; na kama alivyoshauri zion daughter kwenye uzi wake; kama wewe uko kwenye kundi la kwanza, dont give in (sex wise) kwa expectation za kuolewa. Ila kama unataka sex (uko kwenye kundi la pili) jua kuna kuolewa au kutoolewa, l am sure kuna wadada wengi tu wanawaacha wachumba zao (mifano mingi humu jf) mbona wanaume hawalalamiki kuchezewa?

Btw mimi nimechezea wa kutosha tu labda pengine wa kuzidi! Lol



well said,,
namimi nimependa hapo uliposema ya kwamba mbona wanaume hawalalamiki kwamba nao wanachezewa?

Pale tunakua tunachezeana jamani,,
 
Duh!Nimekuelewa sweetie!!
"
Wale wanaodhani wanachezewa wajitazame upya!
 
Dada yangu gfsonwin hivi ulishawahi kusikia mwanaume anasema amechezewa?
"
Kuna tofauti kati ya kuchezewa na kupotezeana muda!
 
Last edited by a moderator:
Wanaume mazoba ndiyo wakoje na nini kinakufanya uwaite wao mazoba? Na kama wanachezeana itakuwaje mmoja awe zoba peke yake na mwenzake asiwe zoba?

Nimeipenda sana hii?Ndege wanaofanana huruka pamoja!
 
wengine husema wamepotezewa muda wao. sasa sijui mwanaume nae hajapotezewa muda!!
 
kama ulikuwa na maongezi ya kawaida kwanini usingemfuata pale alipokuwa?


Kanishangaza sana huyu Dada wa saluni, nimemtuma
mtoto aniitie tuongee mambo mengine kabisa yeye anarudisha
jibu "Mwambie mi sitaki kuchezewa kabisaaa, kama anataka
aje nimuelekeze waliko wazazi wangu, nimechoka yaani
kila siku kuchezeana tu."

Waungwana kwani kuchezewa kunakuwaje?
Je huyo mtu akienda kwa wazazi wake ina maana
kwamba hatomchezea?

Hebu nipeni ufafanuzi wa huku kuchezea.
 
Hilo ndilo tatizo la mtu kujifanya anajua kila kipitacho akilini mwa mtu.Mtu hujaeleza shida yako yeye ameshatoa hitimisho.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom